Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

UMejenga nyumba kwanini usiwe na plan ya tanki la maji? Lita 5,000 ama 10,000 linatosha kusukuma maisha kwa week nzima, ambapo inakuvusha hadi dawasco ama mamlaka ya maji ya mji wako watakapo toa maji tena in case kuna mgao.
 
Naona ishu sasa sio vyoo bali matumizi makubwa tu ya maji kwa familia yako.
 
Vyumba viwili..cha master na Cha wa watoto..Bila jiko wala stoo..yaani najuta japo nilikuwa nilikuwa nabana matumizi kipindi najenga..
Nimeamua kujenga kajumba kengine kadogo nje kawe ka wageni au watoto wa kiume
nafikiri ulikua sahihi mwanzo kwakua nia nikukimbia nyumba zakupanga ukiwa kwako unaweza jiendeleza taratibu kulingana na mahitaji.
 
Kujenga nyumba sehemu yenye water tables bila kutumia dawa za kuta matokeo yake fungus ukutani. Nilipata hasara isiyomithilika. Ilikua ujenzi wa kwanza.

Nilitumia fundi wa slope kitonga kama waswahili wanavyopenda duka linalozidisha chenji.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umenichekesha..
 
Ili kutibu hili tatizo ni vyema sana kwenye mkataba wa mauziano ya ardhi kwa maeneo ambayo hayana hati rasmi/kupimwa mkaweka na barabara tena yenye maelezo ya vipimo urefu na upana na inatokea upande gani wa eneo na ametoa nani.

Hii itawasaidia sana nimeona migogoro ya hivi n nimefanya mikataba mingi inayotoa sehemu ya bara bara.

Bila eneo la bara bara kutolewa kwenye mkataba wa mauziano aise hata ukienda Baraza la ardhi bado utalazimika kutumia nguvu kubwa sana na bado matokeo yakawa 50/50.

Pole sana Mkuu na fikiria namna bora ya kisheria kutatua hii changamoto, zaidi ya yote husisha wakili akusaidie usilichukulie kama ni swala rahisi unaweza uka haribu zaidi.
 
Hapa jirani yangu Dodoma Kuna jmaa anafunja nyumba yake kwani alimpa fundi kila kitu ili yeye aje achukue funguo tu nyumba ikisha jamaaa kufika kuchukua fungu akakuta sebule Ni ndogo kuliko choo na jiko Ni kubwa kuliko master

Na nyumba ikisha pauliwa kila kitu na kupigwa plaster
Hasra aliyopata hatokah hasau jamaa amemua kufunja baadh ya kuta na room ili kubalance ukubwa wa sebule iliyo ndogo Kama choo na choo kiko kikbwa kuliko sebule

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Pumbavu snaaa huyo fundi ingekuta mnnamfungulia kesi ya wizi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
kujenga mjengo mkubwa wenye complication kibao za rooms ambao haukuwa na ulazima sana hadi majirani mtaani na wapita njia walijua lodge, pia kuamini dawa ya mbao niliyopakiwa pale niliponunua mbao nikapaua hivyo hivyo. Next time mafumdi mjipange, ela mtakula ila kwa jasho na mtafanya kazi huku mnanielekeza hatua kwa hatua na mimi nitakuwa nachangia.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…