Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

We Mnyiramba vipi unataka tujenge nyumba kama mabada ya njiwa aisee 😁
 
Tatizo kubwa tunalofeli watanzania ni upangiliaji wa vitu,sasa mtu unakuta kijiko chumbani ama jembe sebuleni linafanya nini!,jenga nyumba ndogo pangilia vitu vizuri utaondoa fikra za kujenga magodauni kwa kudhani ni nyumba

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa hiyo kila chumba kinatakiwa kiwe na ukubwa wa hatua ngapi?
 
Uko kama mimi ...yaan sipendi nyumba iwe na vyumba vidogo
 
Kama unauwezo wa kujenga nyumba ya ghorofa 1 mfano, uwe na master bedrooms mbili. Moja juu na moja chini.
Ukizeeka au kupata changamoto ya kiafya una hamia master bedroom ya chini.
Yeah ni wazo zuri mkuu
 
Kujenga kighorofa.
Jameni, hii shughuli si yakitoto. Ningejenga nyumba ya chini ya vyumba viwili, ningesha hamia kitambo!
Kwa kweli sio jambo la kitoto. Ni kwamba unajenga nyumba mbili kwa wakati mmoja, na kipato chenyewe cha kuunga unga. Mpaka sasa sijapaua, ila nimeshahamia nakaa kwenye andagraundi, japo jasho linanitoka sana kumaliza jengo.
 
Nimejenga underground iliyofanywa na fundi wa mtaani (local fundi), wakati wa kumwaga slab, kwenye wiring map ya umeme hawakuweka zile hook za feni (pangaboi), sasa baada ya kumiminwa slab juu hakuna mahali pa kufunga feni au la niweke mbao za dari ili nipate mbao ya kufungia hook, kitu ambacho ni hasara, maana nitakuwa na slab na bado nimeweka dari.

Ninalazimia kutumia feni za kusimama ambazo sizipendi na zinaleta ghasia tu, sijui kama inawezekana kudrill ili tuweke hook ya feni ili nifunge pangaboi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…