Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Haya nyumba hii hapa 83 SQm ,ni matumizi mabaya sana ya akili na pesa kujenga nyumba ya vyumba 3 kwa SQM 150 ama 200 ni poor mind!,mwisho wa siku unatumia gharama kubwa pesa ambayo ilitakiwa uwekeze sehemu nyingine![emoji276],ni maaajabu sana tena sana kwa mtu mwenye kipato cha kati kujenga nyumba ya SQM 150 yenye vyumba 3,kuanzia SQM 150 kuendelea hiyo ni Guest house View attachment 2468926
We Mnyiramba vipi unataka tujenge nyumba kama mabada ya njiwa aisee 😁
 
Tatizo kubwa tunalofeli watanzania ni upangiliaji wa vitu,sasa mtu unakuta kijiko chumbani ama jembe sebuleni linafanya nini!,jenga nyumba ndogo pangilia vitu vizuri utaondoa fikra za kujenga magodauni kwa kudhani ni nyumba

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa hiyo kila chumba kinatakiwa kiwe na ukubwa wa hatua ngapi?
 
Siriazi vyumba vitatu sqm 76!! Hapo sasa utakua umejenga nini!!,Hio nyumba itakua haina hewa kabisa na imebanana kila kona.standard vyumba vitatu ni sqm 150 ikiwa spacious inafika 200sqm,hii inaitwa medium size house.

Lakini kila mtu ana mapenzi yake ,kiukweli sipend nyumba yenye vyumba vidogo sana hii ni kutokana na nyumba niliyokulia kwa wazee,kipind hicho nipo form 6 naona kabisa chumba ni kidogo hakina hewa vitu vimebanana nikawa najisemea ikitokea nimefanikiwa kujenga yangu huko badae ntaongeza kidogo ukubwa.ila sio mita 5 hizo ni nyingi labda kwa masta.

Asikuambie mtu kuna raha ya kulala kwenye chumba kikubwa chenye hewa .
Uko kama mimi ...yaan sipendi nyumba iwe na vyumba vidogo
 
Kama unauwezo wa kujenga nyumba ya ghorofa 1 mfano, uwe na master bedrooms mbili. Moja juu na moja chini.
Ukizeeka au kupata changamoto ya kiafya una hamia master bedroom ya chini.
Yeah ni wazo zuri mkuu
 
Kujenga kighorofa.
Jameni, hii shughuli si yakitoto. Ningejenga nyumba ya chini ya vyumba viwili, ningesha hamia kitambo!
Kwa kweli sio jambo la kitoto. Ni kwamba unajenga nyumba mbili kwa wakati mmoja, na kipato chenyewe cha kuunga unga. Mpaka sasa sijapaua, ila nimeshahamia nakaa kwenye andagraundi, japo jasho linanitoka sana kumaliza jengo.
 
Nimejenga underground iliyofanywa na fundi wa mtaani (local fundi), wakati wa kumwaga slab, kwenye wiring map ya umeme hawakuweka zile hook za feni (pangaboi), sasa baada ya kumiminwa slab juu hakuna mahali pa kufunga feni au la niweke mbao za dari ili nipate mbao ya kufungia hook, kitu ambacho ni hasara, maana nitakuwa na slab na bado nimeweka dari.

Ninalazimia kutumia feni za kusimama ambazo sizipendi na zinaleta ghasia tu, sijui kama inawezekana kudrill ili tuweke hook ya feni ili nifunge pangaboi.
 
Back
Top Bottom