Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Nilikuta kila kitu kiko vizuri. Hooks ni lazima
 
Nilimpa Fundi ramani akaanza (akaseti) msingi nikiwa sipo.

Kurudi nakuta nyumba ameisogeza sana nyuma. Means makaro ya choo na sehemu ya kuanikia vitabanana upenuni (pembeni). Wakati kama msingi angesogeza mbele hayo makaro (sewage) yangekaa nyuma.

Madai yake anaacha parking kwa mbele.
 
Kujenga kighorofa.
Jameni, hii shughuli si yakitoto. Ningejenga nyumba ya chini ya vyumba viwili, ningesha hamia kitambo!
Mi ilinitia wazimu nilinyanyua cha kishikaji... cement ikala mifuko 1160 nondo mchanganyiko tani 7 unusu tofali 11,700 nilijuta bado kifusi na mawe, marine board 78, kokoto 80qm, mchanga 100qm mbao , mirunda uwii... bado mzigo wa fundi ilikuwa shida...finishing ndio nilikaa na bank ili niwe na nyumba
 

Tofauti Elfu 11700 ni uwanja wa mpira wa miguu ulikuwa unajenga?
 
Tofauti Elfu 11700 ni uwanja wa mpira wa miguu ulikuwa unajenga?
Hujui ujenzi ukiingia utaelewa...

Ngoja nikusaidie msingi tu wenye mzunguko wa tofali 400 mara kozi 7 ni tofali 2800 za kulaza. Boma ni idadi hiyo hiyo ya mzunguko wa msingi yaani 400Γ— kozi 17 = 6800 mpaka kufikia slab/ renta ukumbuke zote zimelazwa then juu mzunguko ni huohuo tena ila hapa ni za kusimama nchi 5 kama ni ghorofa moja ila kozi zinakuwa 10 piga hesabu na huku nilipunguza idadi ya kuta kupata nachotaka zilitumika 2100+ bado kuna vitu vingi sana sijagusia... ukiona mtu kaweka floor kadhaa mpe heshima yake.
 
Wee jamaa huenda hata sqm 20 inakutosha nyumba ya familia.
 
Bro angu mmoja kaamua harakaharaka kununua kiwanja cha mbele yake maana kahofia akili ya ambaye angepachukua ingekuwaje?

Na hata sio lazima akose ustaarabu, ni kwamba asipokubali kukuhurumia tu umekwisha. Ukienda kihaki humshindi.
kabisa, mwenyewe niliwahi kununua kiwanja cha mbele
 
Kuwa na slab haina maana hutafunga ceiling, washua wanafunga ceiling vizuri sana
Your browser is not able to display this video.
 
Kwahiyo sebule unataka iwe mita kumi utakuwa unafuga mbuzi sebuleni ama unafanya mikutano ya kuunga mkono hoja?[emoji851],sebule iwe kubwa kwa matumizi yapi?
Kuna kibanda, kijumba, nyumba, jumba na majumba ya kifahari. Ukiweza kutofautisha hutapiga kelele kulalamika. Chagua panapokufaa kwa mujibu wa utashi ( na bajeti yako).
 
Fuatilia mapema usilaze damu
 
Hata hivyo nyumba yako inaonekana ni kubwa
 
Kuwa na slab haina maana hutafunga ceiling, washua wanafunga ceiling vizuri sanaView attachment 2500021
View attachment 2500024
Ni kweli uwezekano upo, ila unakuwa umefanya jambo mara 2, yaani umejiongezea gharama pasipo sababu ya msingi. Maana hizo ceiling zilivyodizainiwa zinarembeshwa ili zionekane kama ni ukuta, halafu sasa imajini una ukuta kabisa halafu uje kuweka ceiling board.
 
Kujenga nyumba kwenye ardhi yenye kichunguu bila kutreat udongo au msingi wake na madawa ya kuua na kutokomeza kabisa mchwa, matokeo yake pamoja na kuweka tiles full lakini mchwa wanapenya kwenye vishimo na wanajenga ndani mixer kula mpaka vitanda na masofa ukishtuka na kuziba unakuta sehemu nyingine wanaibuka, na kwenye milango ndio kabisa frame ya mlango zinatafunwa ndani kwa ndani kama mikate,

sipati picha wakipenya ndani kwa ndani kwenye kuta na wafike juu darini, naogopa ipo siku gypusm board litanishukia maana wana njaa hao, kuna siku nilichelewa kusogeza kochi nikakuta wamelitafuna mpaka basiπŸ˜₯
 
Hata hivyo nyumba yako inaonekana ni kubwa
Sio sana wastani... inategemea pia na mtazamo wa mtu kuhusu ukubwa wa jengo na anachohitaji. Napenda niwe na study/pray room, Niwe na home mini theatre wengine wanaita recreation room na kila chumba kiwe na ukubwa 4.5m with toilet. So wapo wanaopenda ndogo na wakubwa zaidi.
 
ina sqm ngapi katika kila floor?
 
Yes ni mara mbili, na ndio maana nikasema wanaofanya sio wote ni wale washua ( wenye kipato kikubwa) kiasi cha kuafford seemingly kitu kilekile kurudiwa.

Hata hivyo nadhani Ceiling zina kazi katika nyumba mkuu, ni zaidi ya marembo nadhani ni ishu ya heat conduction and insulation inaingia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…