Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Wakuu naomba msaada hii inshu mashimo sewage system ya vyoo yasiyojaa au wanasema hayana harufu sana. Haya mashimo ynayopigiwa pambio kila sehemu mitandaoni. Naomba experience ya aliyejenga.
Nasubr wajibu
 
Kwa upande wangu, najuta kutozingatia uhalisia wa mahitaji Vs. Ujenzi wenyewe. Naomba kutoa mifano:

1. Umuhimu wa swimming pool Vs. Uhalisia. Vilinganishi vya uhalisia:

a. Utitiri wa swimming pools, at your own choice,
b. Privacy, swimming pools za nyumbani ni changamoto hasa kama una familia,
c. High cost of maintenance etc.

2. Kujenga jengo kubwa Vs. Savings ambazo zingeenda kwenye uwekezaji mfano UTT,

3. Kujenga eneo ambalo barabara ni mbovu hasa kipindi cha mvua, eti kwa hoja; mji unakuwa.

4. Kutozingatia umbali toka kwenye kazi ya kudumu hadi nilipojenga. Hii ni issue.

5. Kuchelewa kupiga fensi kubwa ya ukuta.

6. Kujifananisha na mfadhili kwa mafundi au watu wanaofanya kazi site. Hii ni mission impossible: utaonekana bwege fulani tu mwishoni.

Mambo ni mengi ...
 
Kujenga kwa kugeuza nyumba uso wa nyumba ukaangalia kushoto na kusho kukaangalia mbele ya barabara[emoji22][emoji22]
 
Kuweka nyumba ya wageni, kila shemeji zangu wanapokuja kutoka Usukumani-Mwanza lazma wakaniseme wanalaza kwenye "mabanda ya Uani"
Hahahahaa nahisi wewe nyumba kubwa umeezeka kwa vigae halafu hiyo ndogo umeezeka kwa mabati.
 
Kwa milioni mwanza msinunue tofali za Mzuma hapo nyamhongoro ni matapeli na tofali zao sio imara
 
Kwa milioni mwanza msinunue tofali za Mzuma hapo nyamhongoro ni matapeli na tofali zao sio imara
Elezea utapeli wao vizuri, usije kuharibia vijana ajira zao mkuu.
 
Wakuu naomba msaada hii inshu mashimo sewage system ya vyoo yasiyojaa au wanasema hayana harufu sana. Haya mashimo ynayopigiwa pambio kila sehemu mitandaoni. Naomba experience ya aliyejenga.
harufu ipo bana kwani umeweka ubwabwa kwamba utanukia?

niliambiwa haitakiwi mtu atupie tishu, matambara au kitu chochote umo
kwa maana iyo haufai kuweka kwa nyumba unayoipangisha maana utaishia kugombana na wapangaji kila leo
 
Mwisho wa siku kiinua mgongo kikaisha na jengo halijapauliwa au?
 
Ungemtimua shenzi kabisa huyo!!
 
Ujenzi unaanza na uchaguzi wa sehemu sahihi yani kiwanja utakapoweka iyo nyumba. usinunue tu kiwanja almradi ni kiwanja. kuna mambo muhimu madogomadogo ya kuzingatia kwa mfano namna eneo lenyewe lilivo-Je ni sehemu tambarare au miinuko. Hii ishu ni muhimu kwa sababu inaathari kwenye gharama ya ujenzi. Ujenzi wa kwenye miinuko una gharama zaidi kulinganisha na ule wa eneo tambarare na wkt mwingine mwinuko unaweza kukulazimisha ujenge basement au pengine kigorofa kabisa!

Ishu ingine ndogo lakini ya muhimu ni aina ya watu wanaokaa hapo (majirani). Hili wengi wanalifumbiaga macho lakini bdae linagharama zake. Wewe ni mtu wa kupenda utulivu lakini unajichomeka mitaa yenye watu wa kupenda vigoma/sherehe na matukio kila uchao, hapo lazima utakereka tu.

Kibaya zaidi majirani hawakwepeki, njia pekee ya kuwakwepa ni kuuza nyumba au kuipangisha hlf wewe utafute kwingine kwa kukaa, nje ya apo ukae kwa utulivu uku ukiwavumilia na kuwazoea!
 

"You cant choose a neighbor but u can choose neighborhood "
 
Amenunua bati za ALAF kwa wakala (katoro) lakini zimepauka hat mwaka hazina. Anaomba msaada nini akifanye!
 
Pole sana kaka,, ila kwa sasa hv nashauri kabla hujanunua kiwanja pia angalia ukubwa wa viwanja vya eneo husika, ukiona viwanja ni square mita ndogo mfano 400 jua kabisa ilo eneo makazi yake yatabanana tu, so ni bora kutafuta eneo lingine, tena kwa sasa hv makampuni yakuuza viwanja yalivyo mengi makazi yambeleni yakuwa yakubanana sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…