Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Msingi 7m, huu utakuwa wa ghorofa!
Nyumba msingi... mfano nyumba ya 104.5 sqm (9.5mx11m) inaweza kutumia tofali 3500 za 6" kwa maana ya kozi 7 za kulaza mzunguko wa nje na kuta za ndani. Kokoto 25qbm hii ni kuanzia kizege cha chini na kumwaga jamvi mchanga 20qbm bado simenti ya kujengea si chini ya mifuko 35 bado jamvi kama mifuko 220 uweke marine bodi ni kama 15 zitazo chanywa, misumari, nondo, mbao za setting na mirunda ya kushikia marine. Hela ya mafundi, maji nk ....ukiviweka vyote 7m ni kawaida sana.
 
Kuanza kujenga kwa pesa za pension baada ya kustaafu.
Mzee wangu baada ya kustaafu alifanya hicho kitu. Ni hatari kupita maelezo. Kwanini?

1. Mhusika hashauriki, anataka tu kujenga kwa sababu ana pesa mfukoni.

2. Anachokijenga huwa hakieleweki au hakikamiliki. Anaamini pesa yake ya pension inatosha kufanya chochote au kila kitu kitawezekana. Anaokota ramani popote anataka kujenga.
Mbona baba ako anatabia ka za Baba angu aisee😂😂,..au wamesoma wote nn?
 
Hivi humu jf hakuna mafundi au ndo wanakausha nao wanajifanya wajengewa....mje mafundi mjitete uuku?
 
Kwa tunaoanza kujenga kwa mara ya kwanza...anza kwa kujenga kakibanda chako ishi humo then unaanza kujenga kile unachotaka (nyumba ya ndoto yako) polepole unakuwa umetuliza akili.

[emoji3][emoji3] ukishajenga kakibanda chako hautakaa ujenge nyumba ya ndoto yako tena,anza mdogo mdogo na nyumba ya ndoto yako finishing utakamilisha ukiwa humohumo ndani
 
Habari wana JF

Ni kosa gani ulilifanya kipindi unajenga na ungependa wengine wajifunze ili lisitokee kwao?
Usiwaamini sana mafundi wa kitaa. Kama una hela tumia professional fundi au engineer. Napambana na sisimizi haijawahi tokea. Marumaru hadi natamani nibomoe nianze upya space kati ya tile na tile walibana sana kiasi kwamba grout haikai matokeo yake space ni nyingi na sisimizi wanatokea humu. Fundi rangi pia naye ni shida pia nilimwamini sana fundi wangu lakini nimekuta baadhi ya vitu hajui. Kama issue za Marumaru, rangi, furniture nk.

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
 
Kukagua kazi ya upauaji usiku au jioni sana baada ya mafundi kukamilisha kazi makosa niliyaona kesho yake asubuhi wakati tayari nimewaruhusu mafundi wameshaondoka kurudi mkoani, kuamini ushauri wa fundi mara baada ya kugundua kosa la ukuta kupinda kwa kusema utaonyooshwa na plaster! Kazi ilikuwa ngumu sana kipindi cha plaster asikwambie mtu. Nashauri tuwe tunatembelea saiti zetu mara kwa mara na kama utagundua hitilafu ikemee mapema wala usiiache hadi ifike mwisho itakusumbua kwenye finishing japo jambo hili mafundi hawalipendi sana kwa kuhitaji Uhuru.
 
Hii ni sawa kwa kipindi hiki zamani kidogo uaminifu na watu wa maduka ulikuwa mdogo sana,unaona bora vitu vyako ujitunzie mwenyewe.
Ni njia nzuri sana nimeitumia kwenye material ya dukani kwa hapa Moro kuna duka la Kilosa hardware jamaa yuko poa alikaa na pesa yangu almost mwaka mzima nikijipanga muda ulipofika yaani hata hakuwa na shida kabisa kikubwa uwe na vikaratasi vyake alivyokuandikia kama lisiti kipindi unalipia na upande wa matofali nilifanya hivyo hivyo kule Pangawe jeshini. Utaratibu huu ulinifanya nijenge nyumba faster sana from september 2022 na mwezi May mwaka huu (2023) nimehamia kwangu japo sijaikamilisha baadhi ya mambo. Kiukweli namshukuru Mungu nainjoi upepo wa milima ya uluguru nikiwa kwangu view nzuri ya mji kasoro naifaidi vilivyo hasa kipindi cha usiku kwani saiti yangu ipo kwenye mwinuko.

Ni nyumba ndogo ya kawaida yenye vyumba viwili kimoja master, choo kikubwa cha public, jiko, sebule na vibalaza viwili.

Imetumia matofali 2840, inchi 6 kwa ajili ya msingi 900 yalibaki kidogo, inchi 5 kwa boma 1940, mabati ya migongo mipana 80 yalibaki 6, mabati ya migongo midogo kwa ajili kofia 11 na mbao 360 nazo zilibaki kidogo nazitumia kwa ajili ya majukwaa kwenye plaster n.k
 
Fanya quotation atleast kwa mafundi wawili watatu kupata bei elekezi kwa ubora uleule.
 
Back
Top Bottom