Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Pia kununua kiwanja karibu na mchaga yaani ni shida wao wanachokijua ni kuongeza mipaka hata kama viwanja vimepimwa, hapa nina majirani wawili wote wachaga wote wakati wanajenga ukuta wameongeza mipaka kwa makusudi, kwanza wameng'oa beacons ili kupoteza ushaidi alafu wakajiongezea mipaka.
Point za beacons zipo hata kwa wizara ya ardhi kwa sababu kiwanja kilipimwa tayari, mwenyewe akitaka ukuta unavunjwa tuu.
 
Pia mkumbuke kuzingatia uelekeo wa kuchomoza na kuzama kwa jua wa eneo husika sio kujenga tu kama ramani ilivyo.
Kuna block yangu ipo shambani hapo Mkuranga master bedroom ipo upande jua linapozama kwahiyo lile jua la jioni lote linatandika chumbani hivyo kama unataka kulala vizuri nasubiri hadi saa nne usiku ndio room inakua imepoa.
Tunaoishi maeneo ya Barid hii sasa ndio nzuri..
 
Tofauti Elfu 11700 ni uwanja wa mpira wa miguu ulikuwa unajenga?
Bei ya tofari ni 1,200
Screenshot_20230612-111446_Calculator.jpg
 
Katika ununuzi wa vifaa kwa ajili ya ujenzi ,simenti ndio itakuwa ya mwisho au itanunuliwa siku hiyo hiyo.

Nilijikuta namwaga zege mara mbili baada ya kwanza kuharibika. Kumbe nilinunua simenti muda mrefu na sikuitunza vizuri ikaharibika.

Siku tunaenda kutoa mbao tulikutana na mchanga almanusra imwangukie fundi.Nyingine tulikuta imeganda, nyingine iko kawaida lakini kumbe ilisha-expire.

Hii hali ya kununua vifaa kidogo kidogo inahitaji umakini sana katika uhifadhi wake.
Ulitakiw u mix na mpya . Mfano hio ilioatik mifuko miwili mipya mitano mpak sita
 
Kwa wale wanaojenga gorofa nakup hii isikukute km ilivyonikut mim. Gorofa Huw ili litimie linahusisha fundi tofali Yan kujenga I mean . Fundi mbao. Fundi nondo na Engineer au msimamiz . Kamwe hiz kaz usimpe MTU mmoja Nd ukapatana nae fundi au jamaa Tu akakakwmbia Mie ninauzoef nitafny vyot au Nina watu we nilipe mim kila kit. USIFANYE HIVO KABS YAN. Yaliyonikut nimejifunza maan nilimpa kaz MTU mmoj mwsh WA siku kumb alikuw anawabana San wenzie inapelekea kaz haifanyw kw hark na kw ustaz Yan na kingn hat chin ya kiwng mwsh ikakutia hasar mar mbil
 
Back
Top Bottom