Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Duuh pole sanaa... Huyo jamaa yako mwizii naee kweli anashirikiana na mafundi
 
Ukitaka maisha yasiokua na mawazo tumia wiring mbili kwenye nyumba.
 

Kuhusu hii kitu, nina ushuhuda wa wazee wangu wawili waliostaafu jeshi.

Walifanya huo ujinga.
 
comment #98 imejibu vizuri, pasi, jiko na vifaa vyenye Watts Nyingi (300W au zaidi) ni msala kwa Solar ( japo kama uko vizuri kifedha inawezakana )

Solar hasa inahitaji vifaa laini (Watts Ndogo) kama taa, friji, TV, nk

ukiweka Inverter utatumia vifaa vyote vile vinavyoendeshwa na tenesco isipokua vile vikubwa pasi, jiko, nk

fundi anaweza weka udhibiti kwenye mfumo wa Solar ( mbele ya Inverter ), mathani fyuzi ambayo itakata pale mtu atakapochomeka vyombo vizito kama pasi kwenye soketi wakati mfumo wa Solar ukiwa unaopareti

kuhusu size ya mfumo weka vifaa ulivyonavyo, mie au mtu mwingine anawezasaidia pia

ila kwa ushauri tu juu ya tech ya vifaa (ni swala la ufanisi) nashauri hivi:

1. Solar Panel, chagua ya panel ya Mono badala ya Poly , soma zaidi hapa, bei zimechangamka

2. Charge Controller, chagua MPPT badala ya PWM, soma zaidi hapa , bei zimechangamka

3. Battery , wanasema zile za Minara ziko poa

3. Inverter, chagua yenye kutoa Pure Sine Wave, hii itaendesha vizuri ile vifaa vya umeme vyenye mota ndani kama friji, feni, mashine ya kunyolea, nk



 
Kujenga nyumba sehemu yenye water tables bila kutumia dawa za kuta matokeo yake fungus ukutani. Nilipata hasara isiyomithilika. Ilikua ujenzi wa kwanza.

Nilitumia fundi wa slope kitonga kama waswahili wanavyopenda duka linalozidisha chenji.
 
Though sijawahi kuwa na nyumba wala kujenga ila kosa ambalo siwezi kufanya ni kuachia upenyo wowote, nitajipanga vizuri na hela yao yote cash na nitakuwa nao site kufuatilia kila hatua huku nikiwa na nguo za kazi ikibidi kusaidiana nao kabisa.
Kushinda site ni muhimu sana mkuu
Mafundi wengine wanaenda nje kabisa ya makubaliano,, anaamua kukujengea atakavyo yeye kama anajenga kibanda cha kuku nyumbani kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…