umenikumbusha kitu hapa
nilipanga pahala, maji ni dawasco na kila mtu mita yake
nilikua nalipa 40k kila mwezi, baada ya miezi 5 nakuja kustuka kuna leakage, tena sehem ya outlet ya bomba bafuni, na ni ngumu kugundua, maji yana 'chururu' kimya kimya mno yakiambaa ukutani mpaka chini , inaambaa na kona za sakafu, yalee mpaka kwenye kashimo, yaani chururu huioni mpaka uweke macho karib kabisa na ukuta(una tiles), nikapata jibu kwanini ukuta wote wa upande wa pili(kuna room) ulikua unapukutika
nikafunga koki kubwa ya nje, ikawa nikitaka kuchota najaza jaba na ndoo then nafunga koki, bili ya maji ilikuja 8000 kwa miezi iliyobaki