Ni kosa kubwa sana kisiasa kwa Wananchi kuona mikutano ya Lissu mitandaoni halafu mikutano hiyo haionekani kwenye Television na Media zingine

Ni kosa kubwa sana kisiasa kwa Wananchi kuona mikutano ya Lissu mitandaoni halafu mikutano hiyo haionekani kwenye Television na Media zingine

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Moja ya mambo yatayoigharimu CCM hii ya Magufuli, ni hiki kitendo cha mikutano ya Lissu inayovuta maelfu ya Wananchi kusambaa mitandaoni huku kwenye mainstream Media kama vile tv na redio mikiutano hii hairipotiwi wakati wananchi wanategemea kuiona ikiripotiwa katika vyombo hivi vya habari lakini inakuwa kinyume chake.

Hali hii inazidi kumfanya Lissu akubalike zaidi, huku wale wanaotuhumiwa kuzuia Media zisiripoti habari za Lissu, wakiendelea kupoteza mvuto mbele ya wananchi na hili jambo halina tofauti kabisa na kile kitendo cha kuzuia mikutano ya siasa ya vyama vya upinzani kwa miaka mitano huku CCM wakiwa wako huru kuendesha siasa, ambapo leo hii, wameanza kuvuna walichopanda kwa kuzuia mikutano ya siasa ya wapinzani na kama ambavyo watavuna wapandacho sasa kwa kuzuia habari za Lissu.

Na Lissu mjanja sana kwani ameshajua jambo hili linakera Wananchi hivyo analitumia kisiasa na ndio maana hivi karibuni alitamka wazi kuwa media haziripoti habari za mikutano yake kwasababu media zinamuogopa "mtu mmoja"(hakumtaja ila anaelewaka na ndio maana hata wananchi walishangilia kauli hiyo).

Kutotangaza habari za Lissu, ni hatari kisiasa, na kuzitangaza pia ni hatari kisiasa kwa wahusika.Sasa najiuliza, wanachomokea wapi wenzetu hawa?

Mwaka huu wataomba poa.
 
Ukiona mgonjwa amegoma kula ujue mtoa roho yuko mlangoni, ccm ni sikio la kufa........
 
Sasa kwanini unazindua usingizini? Wakijirekebisha Lissu atashindwa kwa hivyo bora uwaache wafanye hivi hivi.
 
Back
Top Bottom