Kuna ufafanuzi unaohitajika kwa wanaoyaelewa vizuri haya maswala ya Katiba na sheria. Ni matumaini yangu kwamba baada ya uchangiaji wa mada hii wengi wetu ambao hatuna ufahamu vizuri juu ya mambo yahusuyo kazi hii inayokusudiwa kuanza, sote tutakuwa tumepata uelewa wa kutosha, na haitakuwa tena kama swala zima linatumika kuwachanganya wananchi wasijue kinachofanyika.
Kuna habari kwamba pesa inawekwa, kiasi cha Tsh 9 bilioni kiasi kitacho ombwa na Wizara ya Sheria katika Bajeti ya 2023/2024 ili pesa hiyo itumike katika kuandaa Katiba Mpya, na kurekebisha sheria kadhaa zihusuzo maswala ya uchaguzi, kama vile Tume Huru, na chaguzi za serikali za mitaa (2024) na ule wa 2025.
Hili linachanganya kidogo kwa tusioelewa hizi taratibu za kisheria.
Nidhanivyo mimi, ni kwamba jambo muhimu linalotakiwa kufanyika kwanza ni kuandika Katiba Mpya, ambayo, hiyo Katiba Mpya, ndiyo itakayoweka mwongozo wa kupata sheria zitakazoshughulikia maswala ya Uchaguzi na mambo mengine.
Kinachonichanganya sasa hivi, ni hili la kusema fungu hilo la pesa litatumika pia, mbali ya kutengeneza Katiba Mpya, litarekebisha sheria zihusuzo maswala ya uchaguzi.
Mtu anaweza kudhani hakuna mkanganyiko, kwa sababu Katiba Mpya ndiyo itakayotengenezwa kwanza, lakini ukiangalia vizuri, hili siyo linalonuiwa kufanyika mara moja. Ni "urekebishaji wa sheria" ndilo nuio la kwanza.
Mkanganyiko huu unaongezeka, pale inapokumbukwa kwamba kuna ile Tume iliyotoa mapendekezo yake kwamba Katiba Mpya itaanza kushughulikiwa baada ya 2025, na CCM inaliafiki hilo lilivyo.
Hapa nadhani kuna kuvungavunga kwa maksudi kunakofanywa na serikali. Lengo la fungu hili, siyo Kuandika Katiba Mpya; bali ni kurekebisha sheria zilizopo sasa hivi zinazolenga Tume ya Uchaguzi na maswala mengine ya uchaguzi, ambayo bado yanatokana na Katiba hii iliyopo sasa.
Kwa nini pawepo na ubabaishaji katika swala kama hili? Akina Zitto walishaafiki swala hilo, wanaogopa kuwauza CHADEMA walioapa kwamba bila Katiba Mpya hakuna uchaguzi?