KATIBA mpya yenye kukidhi haja hizo ulozitaja ndio suluhisho. Sio ile ilopitishwa na na ccm au hata ile ya warioba bado ina mwanya wa kufanya maonevu.
Katiba ni sharia mama ya namna nchi ilivo jiamulia kujiendesha.
Ukiweka kifungu kuwa Rais wa nchi yupo Juu ya sharia na hawezi kushtakiwa basi uovu hauwezi kuondoka
ukiiwacha katiba kuwa kuishtaki serikali ni mpaka upate kibali cha mwanasheria wa hio hio serikali basi mwananchi hawezi kupata haki
ukiwa na katiba inayo ruhusu Wakuu wa Mikoa na Wilaya wana ruhusa ya kuweka watu ndani hovyo basi hakai haitakuwepo
- Tunatakiwa tuwe na Katiba ambayo Rais hayupo Immune na makosa yake ya Kuvunja Katiba au mateso alofanya dhidi ya wananchi
- inatakiwa katiba ambayo majaji wetu watapitishwa na bunge na wasio weza kuingiliwa na rais au kiongozi mwengine
- tunatakiwa tusiwe na wakuu wa mikoa au wilaya badala yake mameya wanao chaguliwa na wananchi
- tuwe na katiba inayo guarantee uhuru , ulinzi wa raia
- jeshi la polisi liwekewe sharia ngumu dhadi ya uonevu na raia awe huru kulishtaki na kudai fidia anapo vunjiwa haki zake za kikatiba. Pia waweze kushtakiwa kwa jinai zao dhidi ya watuhumiwa
- itatakiwa katiba inayo define nani Mtanzania ukizingatia makabila na asili zetu
- katiba ambayo itapiga marufuku wanajeshi na polisi kuchagua viongozi wa kisiasa. hii kuwatoa katika kugemea uoande mmoja.
- katiba ambayo itakataza kabisa kulingiza jeshi katika mambo ya kisiasa hata akiwa amestaafu bado kuwe na kikwazo kwa rank Fulani kutumikia vyama....
Tukiweka vipengele kama hivi kila mmoja ataheshimu madaraka yake..kila mmoja hataigusa katiba na haki itarudi.
USA sio nchi ambayo kuna haki...katiba yao ni ya kulinda nchi yao na serikali ... ni katiba ilio pitishwa wakati wa civil war ..ni katiba inayo tokana na wababe wa kuvamia maeneo ya nchi nyengine. bado nchi ile juu ya maendeleo makubwa lakini watu wake wanatokana na kizazi cha wababe wahuni na wauaji. ...hawana any type ya civilization wao sio mfano Bora.
Europe nao baada ya WWII hasa zile za West zimejitahidi kuweka misingi madhubuti haki za raia.
nchi kama Ujerumani, UK ni za kupigiwa mfano. Raia wao kwao ni KWANZA