Lada wewe ni mkweli na sio mpiga
"propaganda pumbazo" kama wale chawa wengine..
Kama ndiyo hivyo, basi pole sana na mimi nakuchukulia hivyo kuwa hujui na Kwa maana hiyo najitolea kukupa shule/ tuition isiyo na malipo kabisa hapa hapa..
Na nakuunganisha na ndugu huyu aitwaye
Binadamu Mtakatifu Kwa sababu comment yake hapo juu kama si Kwa makusudi, basi inaonesha hata yeye haelewi chochote kiasi cha kulinganisha mambo ya U.S.A na Tanzania kwa kuwa tu anasikiaga watu wakisema au kuona kwenye TV au kusoma mahali..
SASA TUANZE TUISHENI YETU KWA NAMNA HII;
Kwamba, ili ujue uhusiano wa
KATIBA YA NCHI na maisha ya kila siku ya wananchi hao, sharti kwanza uelewe "
Nini maana ya Katiba"
KATIBA YA NCHI NI NINI?
JIBU: Ni sheria mama ya nchi (makubaliano ya wananchi wenyewe) yanayoweka
misingi mikuu ya
kisiasa,
madaraka,
wajibu na
majukumu ya serikali. Aidha, katiba huonesha na kuainisha bayana
HAKI na
WAJIBU wa raia wa nchi hiyo
kwao wenyewe,
kwa nchi yao na
kwa serikali yao inayowaongoza ambao kimsingi wao wananchi ndiyo wameiweka kwa njia ya uchaguzi ulio
HURU, wa
WAZI na wa
HAKI..
KATIBA YA NCHI HUPATIKANAJE?
Kama inavyoelezwa katika maana ya Katiba, Kwamba ni makubaliano ya watu wenyewe jinsi watakavyojiongoza na kusimamia mambo yao, basi jibu la swali hili moja kwa moja ni kuwa, KATIBA hupatikana Kwa makubaliano ya wananchi wenyewe kwa umoja wao Kwamba, hiki kiwe/kitakuwa hivi, na kile hivi nk nk..
KATIBA YETU YA TANZANIA (JMT) YA MWAKA 1977 ILIPATIKANAJE?
Haikupatikana Kwa njia kama inavyoelezwa hapo juu. Ni kikundi tu cha watu wachache tu chini ya
Baba wa Taifa hili hayati Mwl. Julius K. Nyerere kilikaa na kuamua nchi hii iongozwe vipi. Na kimsingi hiki ndicho chanzo kikuu cha matatizo ya nchi hii mpaka leo na ukielewa hili, utakuwa mwanzo mzuri kwako kuanza kupata majibu ya maswali yako..
Ili uelewe zaidi, nikuulize swali moja rahisi sana.
Kwamba, assume kuwa wewe ni baba wa familia. Kisha ukawa unajifanyia tu mambo yako bila kuwashirikisha watoto wako na mke wako ndani ya nyumba. Unadhani nyumba hiyo itakuwa ya namna gani?
Bila shaka, watasema Duuh, Dingi huyu ni dikteta sana. Ndivyo ilivyo Tanzania ya leo..!
NINI UHUSIANO WA SI TU KUPANDA AU KUSHUKA KWA BEI VYAKULA NA VITU VINGINE, BALI UHUSIANO WAKE KATIKA MFUMO MZIMA WA MAISHA YA KILA SIKU YA WATU KATIKA NCHI?
Kwa ufupi sana;
✓ Katiba ndiyo imeweka utaratibu wa kuweka na kuwatoa (kuwawajibisha) viongozi wanaoongoza serikali kwa niaba ya wananchi..
✓ Katiba kupitia serikali yao waliyoiweka madarakani ndiyo inayotoa mwelekeo wa
KISERA,
KISHERIA,
MIPANGO ya
kiuchumi na
kimaendeleo ya nchi..
KWANINI MAMBO YAKO HIVI? KWANINI MATATIZO HAYA YANAHUSIANISHWA NA KATIBA HII ILIYOPO? JE, KWELI KATIBA MPYA ITKUWA TIBA YA CHANGAMOTO HIZI?
1. Nimekupa historia ya katiba ya Tanzania ya 1977 Kwamba, si makubaliano ya wananchi wote. Utaratibu uliowekwa na watu wachache kwa ajili ya wengi siku zote hupingwa na huwa haukubaliki. Labda katiba hii ya 1977 ilifaa kwa wakati ule wakati nchi ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja na population isiofika hata 10M leo tuko zaidi ya 60M na nchi iko chini ya mfumo wa vyama vingi.
KWA HIYO JIBU LA SWALI #1 NI:
✓ Mambo yako hivi Kwa sababu walioitengeneza katiba hiyo ndiyo walio na serikali tangu wakati huo hadi sasa.
✓ Katiba hiyo kwa kifupi haiwapi wananchi mamlaka ya kuchagua na kuwajibisha viongozi wa serikali yao. Yaani viongozi wa serikali wana nguvu ya maamuzi kisiasa na kiuchumi kuliko wenye nchi yaani umma..
✓ Ushahidi ni uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na ule wa Rais, wabunge na udiwani mwaka 2020. Na Ushahidi mwingine ni kauli za kubeza na kutweza wananchi zinazotolewa na viongozi dhidi ya wananchi.
Mfano, kauli waziri wa fedha
Mwigulu Nchemba ya "
asiyetaka kulipa tozo na KODI za serikali ahamie nchi ya Burundi".
Kwanini alitoa kauli hii?
Ni kwa sababu tu wananchi walilalamikia mzigo wa tozo na kodi mwaka jana 2022!!
Lakini mpaka leo hii mtu huyu yupo na anashikilia madaraka ya uwaziri wa fedha na wananchi hamna lolote la kufanya Kwa sababu hamkumpa ninyi cheo cha uwaziri wa fedha!!
JIBU LA SWALI #2 NI;
Kila kitu kinahusiana na katiba.
Ukiwa na kiongozi mwenye maamuzi na mamlaka na hatumii mamlaka yake kuja na maamuzi sahihi ya SERA ZA KIUCHUMI RAFIKI (bei za bidhaa na huduma), SERA za kijamii na SERA za maendeleo na huku akiwa anajua kabisa wananchi hawawezi kumwajibisha Kwa vyovyote, tegemeeni maumivu na kilio..!
Angalia serikali yote iliyopo sasa. Anzia Kwa wenyeviti wa serikali za vitongoji/vijiji/mitaa, madiwani, wabunge na Rais. Nani aliwachagua mwaka 2019 na 2020?
JIBU NI: Walijichagua wenyewe kwa msaada wa dola chini ya Rais Magufuli wakati huo. Hawapo Kwa ridhaa ya wananchi!!
Na kama ndiyo hivi, ni obviously, hawa hawawajibiki Kwa wananchi, wanawajibika kwa Rais aliyewaweka na serikali yake...
Na mtalia na kupiga kelele sana juu ya
kupanda kwa gharama za maisha tokana na sera mbaya za kifedha na uchumi, lakini hakuna wa kuwasikiliza na hamuwezi kuwatoa kwenye nafasi zao Kwa njia za kikatiba Kwa sababu hazipo na kama zipo ni ngumu kwelikweli...!
JIBU SWALI #3 NI;
Yes, suluhuhisho ni
katiba ya nchi iliyo bora inayowapa mamlaka kamili wananchi ya kuchagua viongozi na kuwatoa iwapo wanaboronga na wanaposhindwa ku - meet matarajio Yao bila sababu za msingi kama ilivyo leo..
Hebu angalia bunge hili la sasa. Lina tija yoyote kweli au wapo pale kwa maslahi yao tu? Lilifanya Nini kiasi cha Mafuta ya petrol kufikia karibu TZS 4,000 Kwa Lita Kwa interval ya mwaka mmoja tu toka March, 2021 ambalo bei ilikuwa TZS 1,800 Kwa Lita?
Unajua kisingizio kilikuwa Nini? Vita ya Ukraine na Urusi..!!
Haya, leo VYAKULA kama mahindi, Mchele, Maharage bei haishikiki, iko juu na maisha ya watu mijini na vijijini ni magumu. Je, kisingizio ni vita ya Ukraine na Urusi tena?
JIBU NI HAPANA...
Tatizo liko Kwa vyombo vya kuisimamami serikali kama Bunge nk kushindwa kufanya kazi na WAJIBU wake wa kikatiba kwa sababu hawawajibiki kwenu wananchi maana hamkuwachagua nyie...!!
TUFANYEJE SASA?
1. NDIYO. Kwa sbb ya kelele za kina Tundu Lissu na CHADEMA zinazoendelea kupigwa, serikali na CCM wameshahituka na kuona hatari iliyopo mbele yao iwapo hawatachukua hatua. Na ni kweli kwa sababu wananchi wengi wameshaanza kuamka na kuona tatizo lilipo..
Kwa hiyo, tayari tumeshaanza kudanganywa na kupumbazwa na "mikakati ya muda mfupi" tu ya kukabiliana na hali ngumu ya kiamisha.
Kuwa na mikakati ya muda mfupi (Short terms strategies/solutions) ni sawa na siyo mbaya kabisa. Lakini tunahitaji suluhisho la kudumu...
2. Suluhisho hili ni
KATIBA MPYA YA WANANCHI inayorekebisha kasoro zote zilizo kwenye katiba tuliyonayo ya 1977. Katiba itakayowapa wananchi mamlaka kamili ya KUWAWEKA na KUWAWAJIBISHA viongozi wao. Na pia kuondoa kimrundikia mamlaka mtu mmoja tu aitwaye "
RAIS" anayeweza kufanya lolote bila kuulizwa wala kuwajibishwa na sheria yoyote..
Natumai umeelewa sasa. Kama una swali, uliza tu