Nacho kiona kwenye hizi harakati za katiba mpya, ni maswala ya madaraka tu. Kwamba wapinzani wameshagundua hawawezi kushika dola kama katiba itaendelea kua hii, hivyo wanajaribu kahakikisha tunaichukia hii katiba tuliyo nayo ili tupate hiyo nyingine itakayo wapa wao mwanya wa kupenya kwenye dola.
Ila kiukweli harakati hizi sio kwa maslahi ya wananchi, hawa watu hua wanatanguliza maslahi yao mbele tu sikuzote. Hata ukichunguza kilicho sababisha mchakato wa kwanza kutofikia muafaka utakuta changamoto ilikua ni maslahi ya upinzani hayakutimizwa.