Ni kwa kiasi gani Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu imefanikiwa kutokomeza umasikini na kuinua hali bora za maisha ya Watanzani?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
kwa kiasi kibuwa Tanzania imepiga hatu za kimaendeleo chini ya serikika sikivu ya CCM ya awamu ya sita kwa kuinua vipato na hali bora sana za maisha ya waTanzania,

kwa kuzingatia uhakika wa hali ya ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, watu na makazi yao, kazi na na biashara zao,

Lakini pia, kwa kuzingatia uhakika katika huduma za umeme, usafishaji angani, majini na ardhini, afya na maji ya kutosha, mijini na vijijini,

Na tena,kwa kuzingatia mapinduzi makubwa katika kilimo, ufugaji, uvuvi, na mageuzi katika sekta ya maliasili, utalii, historia na uhifadhi wa tunu za Taifa,

Kwa kutilia maanani hali bora iliyoimarishwa sana kisheria, ya shughuli za kisiasa nchini, Uhuru wa Habari na maoni, hali bora ya mifumo ya utoaji haki, Uchaguzi Huru na usawa katika kupata huduma muhimu za kijamii na maendeleo.

Je,

ni kwa kiasi gani Rais na Kipenzi cha wananchi wengi wa Tanzania amefanikiwa kupunguza umasikini na kuinua hali zilizo bora zaidi za Maisha ya waTanzania?

elezea kwa kifupi kwa mifano...🐒
 
Je, ni kwa kiasi gani Rais na Kipenzi cha wananchi wengi wa Tanzania amefanikiwa kupunguza umasikini na kuinua hali zilizo bora zaidi za Maisha ya waTanzania?

elezea kwa kifupi kwa mifano...🐒
Alichofanikiwa huyo kipenzi chako ni kwenye teuzi na tenguzi. Hakika amefanikiwa kuhakikisha wateule wanaondokana na umaskini
 
Imetokoneza umasikini gani? Siku umasikini ukiisha na ndio mwishi wa CCM, umasikini ukiisha wakina Lukuvi hawataweza kuhonga wapiga jura Viberiri kule Isiman, kule Kanda ya ziwa wale wasukumu hawatahongwa chumvi.

Hakuna namna CCM inaweza ondoa umasikini, umasikini ni mtaji wao mkuu.
 
ama kwa hakika,
teuzi na tenguzi za mara kwa mara, ni katika kuimarisha utendaji kazi wa serikali, na kuchochea ufanisi wa kazi za serikali katika kuinua maisha, kuboresha maisha na kuwaletea wananchi maendeleo na kutokomeza umaskini kwa waTanzania 🐒
 
Tanzania bado Ni nchi maskini ya wakulima na wafanyakazi . Haijawa ya matajiri
tuko pazuri sana na tunaelekea pazuri zaid kiuchmi, chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan kipenzi cha wananchi na Rais wa Tanzania.

hali ya maisha ya waTanzania imeimarika zaid ya kipindi kilichopita, vipato vya waTanzania vimeongezeka maradufu, lakini pia utoaji wa huduma muhimu za kijamii umeboreka mno 🐒
 
Umasikini ni mtaji mkuu wa CCM, masikini ndji wanao hongwa kofia, kanga na tshirt,
huwenda unazungumzia umaskini wa hoja, kufilisika ushawishi, mawazo mapya na fikra mbadala kwa vyama vya kisiasa nchini...

maana hawana mipango, hawana dira, wala uelekeo wa kueleweka kisiasa licha ya uhuru, haki na mazingira sawa waliyowekewa na serikali sikivu ya CCM chini ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan 🐒
 
Imetokoneza umasikini gani? Siku umasikini ukiisha na ndio mwishi wa CCM, umasikini ukiisha wakina Lukuvi hawataweza kuhonga wapiga jura Viberiri kule Isiman, kule Kanda ya ziwa wale wasukumu hawatahongwa chumvi.

Hakuna namna CCM inaweza ondoa umasikini, umasikini ni mtaji wao mkuu.
imetokomeza umaskini wa kipato, imetokomeza umaskini wa fikra kwa kutoa elimu bure, imetokomeza maradhi kwa kuimarisha huduma muhimu za afya kwa uhakika zaidi n.k

hata hivyo licha ya dosari na kasoro ndogo ndogo katika harakati za kutokomeza umaskini huo, bado serikali inaendelea kufanya kazi kubwa zaidi katika kujenga mazingira mazuri zaidi ya biashara, masoko, uwekezaji, kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuzalisha ajira nyingi zaidi kwa vijana...

vilevile,
kazi kubwa zaidi inaendelea katika kuimarisha umoja, amani na utulivu wa wanainchi na kuboresha mazingira yao ya kazi za uzalishaji na kujiongezea kipato 🐒

shukrani za kipekee sana zimuendee Dr.Samia Suluhu Hassan kwa matokeo yake uwekezaji wake kwenye kilimo na kusababisha mavuno mengi ya kipekee mno kwa mwaka huu wa kilimo 🐒

Tunashukuru Mungu kwa Zawadi ya huyu Dr.Samia Suluhu Hassan 🐒
 
Elimu bure ya wajinga, wewe hapo mtoto wako anasoma kwenye elimu bure?
 
Ndio maana wazungu wanaitaga waafrika nyani kwa mawazo mgando kama haya.
hata wakituita zaidi ya hapo,
ile muhimu zaidi ni kuchapa kazi kwa bidii bila kuchoka wala kukata tamaa kujikomboa kutoka katika lindi la umaskini wa kutupwa kwa muda mrefu sana,

hii ni fursa na wakati muafaka sana, tukiwa chini ya kiongozi wetu makini, shupavu na kipenz cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha na kuboresha mazingira ya uzalishaji katika kilimo, ufugaji, biashara, utalii n.k ili kujiongezea vipato vya kutupatia maisha bora zaidi kijamii, kisiasa na kiuchumi 🐒
 
Utachapa kazi bila kuchoka kama unapata kitu je wajua biashara zimedolora saaaana hapa nchini Kama wajua tuanzie hapo.
 
hata wakituita zaidi ya hapo,
ile muhimu zaidi ni kuchapa kazi kwa bidii bila kuchoka wala kukata tamaa kujikomboa kutoka katika lindi la umaskini wa kutupwa kwa muda mrefu sana,

hii ni fursa na wakati muafaka sana, tukiwa chini ya kiongozi wetu makini, shupavu na kipenz cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha na kuboresha mazingira ya uzalishaji katika kilimo, ufugaji, biashara, utalii n.k ili kujiongezea vipato vya kutupatia maisha bora zaidi kijamii, kisiasa na kiuchumi 🐒
Kuchapa kazi!!!

Watanzania wanachapa kazi gani zaidi ya uvivu, wizi na umbea huko makazini?

Mtu anatega kazini haji hata mwezi.

Ukitaka kujua maana ya uchapa kazi fanya kazi na wazungu au kaishi nchini mwao ndio utaelewa nini maana ya kuchapa kazi.

Wabongo wanachoweza ni kuchapa umbea na gambe.
 
acha dharau gentleman,

wavivu ni kweli wapo Lakini wachache sana, hata huko kwa wazungu wamejazana pia kwa kiasi chao na wengine wamo humu nchini...

kazi ni kipimo cha utu, uoga wako katika kazi umaskini wako..

ni muhimu kutokukata tamaa, Dr Samia suluhu Hassan amefungua nchi, fursa zimetapakaa kila mahali, ni uamuzi na uthubutu wako tu wa kuchagua cha kufanya iwe ni biashara, kilimo ufugaji, usafirishaji n.k kutoboa maisha ni uhakika, na ndio maana kiwango cha umasikini kinatokomea kila uchwao, maisha ya waTanzania yanaimarika, kipato cha waTanzania kinaongezeka 🐒
 
Back
Top Bottom