barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,880
Ni wapi Julius Nyerere aliwazidi "ujanja" wazee wa mjini,born town na Watoto wa K'koo? Wazee wake na gwiji wetu wa historia Mohamed Said
Ukifuatilia historia na harakati za Uhuru,unaona kuwa huyu kijana wa Kizanaki,mtoto wa Chief na "mvaa kaptula" alikuja baadae sana Dsm wakati wenzake wakiwa mjini kitambo na harakati za kumuondoa Mkoloni.Wakati Julius anakuja DSM tayari harakati za Uhuru zilikuwa zimepamba moto.
Maelezo mengi ya Wazee yanaonyesha Julius aliaminiwa mapema sana na kupewa madaraka ndani ya chama na hatimaye baadae kuja kuwa Rais wa TAA/TANU na hatimaye nchi.Vijana wenzake waliompokea mjini wakebaki kuwa wao wao watoto wao na wajukuu wao kuwa Julius baada ya Uhuru "aliwasahu"
Wazee wengi wanahisi Julius aliwazidi ujanja na kuwaweka kando baada ya kuchukua nchi.Mitaa ya Kata ya Ng'ambo Tabora,miaka kumi iliyopita nilipata kuwaona wazee wawili,wajanja wa mjini waliompokea Nyerere ktk harakati zake mkoa wa Tabora.Mzee mmoja akiitwa Pacha,akiishi eneo la "filter" pembeni ya kilabu moja maarufu ya pombe mjini Tabora.Mzee mwingine akiitwa Rehani.Huyu kwa heshima kuna mtaa Tabora uliopewa jina lake.Unaitwa mtaa wa Rehani.Kuna Rehani A na Rehani B.
Hawa wote ukikaa nao watakuambia "Julius ni mjanja sana,alituzidi maarifa".Ukija K'koo kuna wazee wengi wapo na malalamiko na wengine wamekufa nayo.Sikumbuki ni Sykes yupi kati ya hao naowasikia.Lkn miaka miwili au mitatu iliyopita...Jijini Nairobi,kwenye Uwanja mdogo wa ndege wa maarufu kama "Wlison Airport" majira ya adhuhuri kuelekea alasiri.Nakutana na Wanawake wawili.Moja Mama wa makamo na mwingine mdada wa umri wa juu kidogo.Huyu Mama bila shaka ni mke wa marehemu na huyu wa pili bintiye.
Hawa wanajiandaa kupakia mwili wa ndugu yao,ni marehemu.Maafisa wa Uhamiaji wanatazama passport zao za kusafiria na kuona ni pass za kidiplomasia. Wanatakiwa kuusafirisha mwili wa ndugu yao kuja Dsm.Wamekodi ndege ndogo aina ya C208. Yenye uwezo wa kubeba watu wanne tu.Lakn wale wanawake wakiwa na ndugu wengine wanakubaliana kubeba maiti na wao kuja DSM.
Ndege ndogo,ktk ubanano na majonzi ya msiba wale wamama wanabanana na maiti ikiwa ndani ya mkeka kuileta Dsm.Ndege ya C206 ni ndogo sana kwa umbali wa Nairobi to Dsm, tena ukiwa na maiti,na hasa kwa wanawake.Kuuliza kwa ndugu waliobaki pale Uwanjani kufanya mpango wa kwenda Jomo Kenyatta ili waje Dsm,wanasema huyo alipata kuwa mpigania uhuru wa Tz,balozi mashuhuri na mwanadiplomasia mbobezi.
Pale pale wanaanza kung'aka kuwa hawa ni wapigania uhuru waliosahaulika na nchi,ndio maana wanabebwa na ndege ndogo aina ya C206 kurudi kwao.Ni malalamiko tu ya "kusahauliwa" muda wote wa maongezi yao.
Akija humu Mzee wangu Mohamed Said, atakutajia kina Mshume Kiyate(?), atataja kina Dosa, mara kina Tewa Said Tewa na wengine wengi kuwa hawa nao hawakufaidi matunda ya Uhuru. Hivi kwani huyu Julius alikuwa na ujanja kiasi gani hawa wote akawaingiza "mjini" wakati wao ndio waliompokea?
Nilitembelea Kilwa,kule kuna Kilwa ya Kivinje na Kilwa Kipatini. Huku Kilwa Kipatini ndio kwao na Kingunge.Huku kuna Kanisa kongwe sana la miaka mingi walijenga Wajerumani. Kanisa hili ndipo alibatizwa Kingunge N. Mwiru. Wengi hudhanj Kingunge hakuwahi kuwa na dini kabisaaa. Kumbe huyu ni mbatizwa ktk Kristo, kabla ya kwenda Usoviet na kuachana na dini.Lkn kwa kubatizwa huyu anaitwa "Ambrose Ngombare Mwiru".
Huku Kivinje kuna watu nao wanasema "Julius alituzidi ujanja". Hivi huu "ujanja" waliozidiwa hawa wote ni kwa sbb ya nini? Ni kwanini walimpokea na kumpa uongozi halafu baadae walalamike?Kwanini wasingemnyima?Je baada ya Uhuru hawa "walalamishi" wote walitaka Julius afanye nini ili walidhike?
Leo ninaomba majibu, nijue, ni wapi Julius, kijana wa Kizanaki aliwazidi "ujanja" hawa vijana wa mjini wa K'koo?
Cc Ngongo UncleBen Barbarosa Ritz