Cobrahypnosis
JF-Expert Member
- Jul 28, 2021
- 362
- 676
Ujamaa...
Salum Abdallah babu yangu hakuwa manamba.
Sisemi kuwa manamba ni watu duni la hasha ili hakuwa manamba.
Kazi yake ilikuwa mfua chuma.
Aliajiriwa kwa kazi hiyo na Tanganyika Railways katika miaka ya 1920.
Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walijuana Makerere.
(Ukiandika uhuni ''babu yake Dully Sykes'' kadha wa kadha unanipa shida kwani huu kwangu ni mjadala wa kistaarabu si mjadala wa kejeli).
Angalia post yangu ya mwisho vipi ninavyoandika na kueleza historia ambayo haikuwa inafahamika kabla.
Kwa nini Hamza Mwapachu hakutakiwa kuchukua uongozi wa TAA na kuunda TANU au kwa nini Abdul Sykes hakuchukua au kwa nini Chief Kidaha Makwaia hakuchukua hizi zote ni historia za kusisimua.
Historia hii hakuna aliyepata kuandika ila mimi baada ya kusoma Nyaraka za Sykes na kuandika kitabu.
Kuhusu NECTA nina mengi ambayo naweza nikayaweka hapa kwa ushahidi na sote tukanufaika kwa taarifa hizo hata kama wewe hutoamini.
Lakini ili tufanye mjadala wenye tija muhimu kwanza tukaheshimiana.
Swali langu lilikua ni Kwanini viongozi wasiwe babu zako maana unasema walikua wengi je ni nini kiliwafanya wampe mwalimu uongozi. Inamaana kwa kipindi hicho hawakua na uwezo. Unasema Nacte ilikuwa inahujumu shule zenu na ushahidi unao, sasa unasita nini kuuweka hapa ili watu waone, umesema kulikua na hujuma basi unalojukumu la kudhibitisha hizo hujuma hapa. Leo ni 2023 bado mnahujumiwa kama mnavyo dai ni juzi tu matokeo yametoka bado mnashika mikia mixa mizero kibao kwene shule zenu na majina yenu.