Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

AlhamduliLlah Hahitaji kaimu wala msaidizi, anajimudu mwenyewe tena sana, atakuja kwa wakati wake.
MaalimFaiza,
Hawezi kufanya mjadala na wewe.
Hana uwezo huo.

Si na wewe wala yeyote yule.

Anasema alikuwapo Evenston Northwestern University kaniona naingia Ukumbi wa Eduardo Mondlane kuzungumza nimefatana na Wapakistani.

Akili yake inakataa kuamini kuwa naweza kualikwa Northwestern University.

Akili yake inamwambia huyu Mohamed Said si lolote.

Hii ndiyo sababu ya hayo matusi anayoyarudia kila mara kiasi mimi nikiona post yake najua nini kaandika.

Hataki hata mtu mwingine achangie mjadala huu.

Anaogopa wataingia wajuzi wa matusi kumshinda.

Chicago nzima nilikuwa najuana na watu watatu tu: Jonathon Glassman, Nathaniel Mathews (niko nae kwenye picha hapo chini) na James Brennan ambae alinichukua kwa gari yake kutoka Iowa City hadi Chicago.

Hata ule ujanja wa kuniambia kuwa nilikuwa nakutania hana anataka uaminike uongo wake.

1679588350299.jpeg
 
Barafu,
Umeandika maneno mengi na mengine umeyarejesha kwangu kama ndiyo
nimeyasema wakati sijapatapo kufanya hivyo.

In Shaallah nitajitahidi kukujibu kadri Allah atakavyoniwezesha.

Umeanza na swali la ''ujanja,'' kuwa Nyerere aliwazidi ujanja na umesherehesha
kwa maneno mengi ya ''gwiji,'' ''born town,'' ''mvaa kaptula,'' nk.

Kwa bahati hizo si lugha zangu mimi.

Si lugha zangu kwa kuwa ndani ya maneno hayo kuna kebehi na ukipenda matusi ya rejereja.

Kwa bahati hizi si lugha zangu. Labda nikufahamishe.

Itabidi endapo utapenda tufanye mjadala unieleze khasa umekusudia nini kwa neno, ''ujanja.''

Baba yangu katika miaka ya 1950/60 akivaa kaptula na stocking kazini.

Halikadhalika Abdul Sykes akivaa kaptula na shati jeupe pale ofisini kwake akiwa Market Master, Kariakoo Market.

Nimeandika kitabu cha Abdul Sykes na sasa ni kitabu maarufu.

Maneno yangu yote niliyotaka kusema kuhusu historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika nimeyasema mle.

Niliandika kwa Kiingereza na kikachapwa London mwaka wa 1998 na tafsiri yake ikachapwa Nairobi mwaka wa 2002.

Kitabu hiki kilifanyiwa, ''serialisation,'' tatu na The East African mwezi December, 1998 na ''review,'' na wanahistoria mashuhuri katika African History kama John Iliiffe, Jonathon Glassman na James Brenan na hizo ''review,'' kuchapwa katika ''journals,'' maarufu mojawapo ikiwa Cambridge Journal of Africa History.

Kitabu hiki kimepata heshima yake na hivyo mwandishi kapewa hadhi aliyostahili
kwa kitabu hicho.

Umetumia neno, ''kusahau,'' kuwa Nyerere amewasahau wazee waliopigania uhuru.
Sijui kwa nini umeamua kuwataja wazee peke yao katika hili.

Sijui kwa nini hukuwataja na vijana ila wawili Dossa na Tewa na kusema kuwa nimesema
''hawakufaidi matunda ya uhuru.''

Sijapatapo popote kuzungumza kuhusu Dossa au Tewa na matunda ya uhuru.
Labda utanijibu kuhusu haya.

Mimi nimetaja neno ''kusahau,'' katika kitabu cha Abdul Sykes na kwengineko katika
maandishi yangu mengi.

Lakini nimetaja ''kusahau,'' pale Nyerere katika kueleza historia yake alipofika Dar es
Salaam aliposahau Abdul alikuwa na cheo gani katika TAA yeye alipopokelewa ndani
ya TAA na Abdul Sykes mwaka wa 1952.

Haya yalitokea mwaka wa 1985 Ukumbi wa Diamond siku alipokuwa anaaga.

Ikiwa kuna wazee ambao wewe umezungumzanao na wakakuambia, ''wamesahauliwa,''
mimi siwezi kuwajibia.

Naomba nimalize kwa kukueleza wazee wangu mimi walimaliza vipi maisha yao ya siasa.

Wazee wangu baada ya Nyerere kuvunja Baraza la Wazee wa TANU mwaka wa 1963
wao hawakutia tena mguu pale Ofisi ya TANU wala hawakugombana na yeyote yule.

Wazee hawa walikufa majumbani mwao na heshima zao na kuzikwa kimya kimya na
ndugu zao.

Hapakuwa na mizinga, bendera kufunikwa majeneza yao na wala watoto
wao hawakusikitika kwa wazee wao kukosa hayo.

Hayo mengine siwezi kuyajibu kwa kuwa wenyewe wapo na ikiwa watakusikia na
watapenda kukujibu watakujibu.
Kusema ukweli, Nyerere mnamuonea. Hana nguvu hizo za kuwarudi wote hao waliomsaidia. Kila mtu akijiangalia kwenye kioo, atajigundua kama bado anazidi kuwa kijana au anazeeka.
Kuongoza nchi sababu umezaliwa Kariakoo ukawahi kuanza harakati za kutafuta uhuru? Hata Mandela alikuwa mshamba Johanesburg alipoenda kuanza kazi ya uwakili akitokea kijijini kwao Qunu.
Nyota ya mtu ni Mwenyezi Mungu peke yake anayeilinda na kuifanya ing'ae. Kama ilikuwa inang'aa, hapa wa kumpiga mawe sio Kambarage. Mnamuonea tu
 
Mnataka kujirithisha nchi kama ni yenu peke yenu, na muachwe hivi hivi? Never on earth. hata leo, mkileta mbambamba, hayo mambo yatawakuta
Rogo...
Waliofanya njama kujirithisha nchi iwe yao peke yao historia yao imeandikwa katika kitabu hicho hapo chini.

Je unao ujasiri wa kuwaambia hawa maneno uliyoandika hapa kuwaonya Waislam?

Au hukijui kitabu hiki?
''Mnataka kujirithisha nchi kama ni yenu peke yenu, na muachwe hivi hivi? Never on earth. hata leo, mkileta mbambamba, hayo mambo yatawakuta.''
1679601208443.jpeg

Rogo...
Waliofanya njama kujirithisha nchi iwe yao peke yao historia yao imeandikwa katika kitabu hicho hapo chini.

Je unao ujasiri wa kuwaambia hawa maneno uliyoandika hapa kuwaonya Waislam?

Au hukijui kitabu hiki?

Kwenye nchi kubwa kama hii, haitawezekana kupata kiongozi anayeridhisha kila mtu. Kitabu kilichoandikwa nchi hii si kimoja. Tena kuna mambo ukiyasikia yatazibua ngoma za masikio, na hayakufanywa na Nyerere.
Hatuishi duniani miaka 200. Tusijisahau. Kila kitu tunachojaribu kujenga kwa misingi ya uongo, hakitaweza kusimama. Ipo siku kitaanguka chali. Nchi yetu ni changa. Nakushangaa unapotaka kufanya dini moja ndio muhimu kuliko zingine.
Hata macruseder hawakuweza. Mpaka leo, kuna dini zote. Naangalia maarifa, utashi na hekima ya watu wanaofanya hivyo, nashangaa.
Mfupa uliomshinda fisi, mbwa labda awe wa kichina!!!!
 
Rogo,
Umesoma kitabu hiki?
Soma upya post yangu.

Nimekuuliza vitisho ulivyotupa Waislam unaweza kuwapa na wale waliojirithisha nchi?

Ikiwa hujakisoma kitabu hiki nieleze nikuambie kinasema nini.
 
Huyo kwene picha ni kobazi nini!! Dizaini kama anakula kipondo vile, ukileta vurugu utapigwa tu namimi nasema wapigwe tu maana hakuna namna.
IMG_8010.jpg

Uhuru, umoja, mshikamano ndio jadi yetu watanzania.

Hizo propaganda za huyo mwene bando la boksi mwambie alete mpango wa kuwajengeeni vyuo na mashule kama zilivyo parokia. Msitaabike na parokia, mda huu SAUT wameshaanza ujenzi wa campus yao huko Rukwa. hatujasimama hilo mlijue.
IMG_8011.jpg

Baba wa taifa kamwe huwezi kumuweka mtu huyu kwene kapu la wapuuzi walio wengi, ni yeye pekee anaefahamika afrika katika hatakati zake za ukombozi. Hawezi kaa kapu moja na mtu yeyote yule. Mtaongea weee ila baba wa taifa ni mmoja.
 
Huyo kwene picha ni kobazi nini!! Dizaini kama anakula kipondo vile, ukileta vurugu utapigwa tu namimi nasema wapigwe tu maana hakuna namna.View attachment 2563830
Uhuru, umoja, mshikamano ndio jadi yetu watanzania.

Hizo propaganda za huyo mwene bando la boksi mwambie alete mpango wa kuwajengeeni vyuo na mashule kama zilivyo parokia. Msitaabike na parokia, mda huu SAUT wameshaanza ujenzi wa campus yao huko Rukwa. hatujasimama hilo mlijue.View attachment 2563833
Baba wa taifa kamwe huwezi kumuweka mtu huyu kwene kapu la wapuuzi walio wengi, ni yeye pekee anaefahamika afrika katika hatakati zake za ukombozi. Hawezi kaa kapu moja na mtu yeyote yule. Mtaongea weee ila baba wa taifa ni mmoja.
Ujamaa...
Mimi siko hapa kwa kufanya kejeli na kutoleana maneno yasiyopendeza.

Mimi ni katika watu watatu wenye maktaba yenye taarifa za Mwalimu kushinda maktaba zote nazo ni maktaba ya: Dr. Salim Ahmed Salim, Brig General Hashim Mbita na Maktaba yangu.

Haya yameelezwa katika "Nyerere Biography," (2020) na nilihojiwa na jopo la waandishi wa kitabu hicho kuhusu maisha ya Mwalimu alivyopokelewa na watu wa Dar-es-Salaam kupitia akina Sykes.

Hii ilikuwa mara yangu ya pili kushirikishwa katika kitabu cha maisha ya Julius Nyerere.

Ningeweza kukueleza mengi.

Sijapata kumdogosha Nyerere katika sifa zake anazostahili na zinafahamika dunia nzima.

Labda usilolipenda wewe na kwa hakika hili limeshtua watu wengi ni kule kueleza historia ya Nyerere kwa ukweli.

Mathalan vipi harakati za kuunda African Association zilianza na Kleist Sykes mwaka wa 1929 na vipi Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walivyomwingiza Nyerere katika uongozi wa TAA mwaka wa 1953.

Historia hii inakwenda na mengi ambayo yalifutwa katika historia ya TANU.

Katika hali kama hii mimi siwezi kujihusisha na mjadala ambao ndani yake kuna kila dalili ya kukosa heshima.
 
Utajibiwa kadri ulivyo jibu. Ukijibu kwa masihara utajibiwa kipuuzi vilevile. Swala hapa ni hoja za Nyerere wewe unaleta mtu anapigwa mala mwananchi wa hadhi ya kawaida kashika bango la Parokia. Sikuona umuhimu wa hilo bango ndio maana nikakwambia parokia ni swala zito usichukulie kimasihara maana na mikwara yako yote lakini ulisoma kwene hizo hizo shule za parokia. Wazee wa kaliakoo na wengine wengi bado sana kwa baba wa taifa ndio maana kwa uwingi wao waliona umuhimu wa mtu huyo. Ni jukumu lako unaesema unaijua historia kusomesha hapa pia ni jukumu letu kusoma, kuuliza na kukosoa. Wapo wengi sana mzeee sio hao tu ambao awafahamiki. Endelea kushusha nondo ila Jina ka baba wa taifa Hayati Julius kambarage nyerere litaishi miaka na maelfu Dunia hii.
IMG_8019.jpg

IMG_8018.jpg
 
Utajibiwa kadri ulivyo jibu. Ukijibu kwa masihara utajibiwa kipuuzi vilevile. Swala hapa ni hoja za Nyerere wewe unaleta mtu anapigwa mala mwananchi wa hadhi ya kawaida kashika bango la Parokia. Sikuona umuhimu wa hilo bango ndio maana nikakwambia parokia ni swala zito usichukulie kimasihara maana na mikwara yako yote lakini ulisoma kwene hizo hizo shule za parokia. Wazee wa kaliakoo na wengine wengi bado sana kwa baba wa taifa ndio maana kwa uwingi wao waliona umuhimu wa mtu huyo. Ni jukumu lako unaesema unaijua historia kusomesha hapa pia ni jukumu letu kusoma, kuuliza na kukosoa. Wapo wengi sana mzeee sio hao tu ambao awafahamiki. Endelea kushusha nondo ila Jina ka baba wa taifa Hayati Julius kambarage nyerere litaishi miaka na maelfu Dunia hii.View attachment 2564366
View attachment 2564367
Ujamaa..
Mimi sina tatizo kujibu maswali kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kote nilikoalikwa toka kitabu changu kichapwe naulizwa na najibu maswali.

Bango la Parokia picha hiyo nimepiga katika maandamano ya Waislam dhidi ya NECTA mwaka 2012.

Nimeweka hilo bango kueleza kuwa nchi yetu ina matatizo.

Wewe hukuona umuhimu wa bango hilo lakini Waislam wameona umuhimu wa kulibeba serikali ilisome na itambue nini kinalalamikiwa.

Ikiwa hujui historia ya haya maandamano nifahamishe nikueleze.

Mimi nimeeleza historia ya kweli ya Nyerere kuliko mwandishi yeyote kabla yangu ingawa watu kama wewe wanaona tabu na sababu ya dhiki hii inafahamika.

Wanaumizwa na ukweli kuwa kwa nini Nyerere alibebwa katika mabega ya Waislam wakati wa kupigania uhuru.

Picha za kudai uhuru ni shahidi wa hili.

Kwa nini Mufti Sheikh Hassan bin Ameir aliuza kadi za TANU misikitini.

Kwa nini Kadinali Rugambwa hakuuza kadi za TANU kanisani.

Kwa nini hafla ya kumuaga Mwalimu safari ya kwanza UNO 1955 ilifanyika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

Kwa nini haikufanyika Parish Hall St. Joseph's Cathedral?

Kwa nini mkusanyaji fedha za safari hiyo alikuwa Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul na ndiye pia alikuwa Mweka Hazina wa TANU kadi yake no. 24 na ya nduguye Iddi Tosiri kadi no. 25.

Hawa walihuidhuria mkutano wa kwanza za TANU August 1954 Ukumbi wa Arnautoglo na ndugu hawa wawili ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo kwa Sheikh Mohamed Ramiyya.

Ndugu hawa walikuwapo pia katika uchaguzi wa mwaka wa 1953 wa kuchagua President wa TAA uliofanyika hapo hapo Arnautoglo Hall kati ya Abdul Sykes na Julius Nyerere na Nyerere akachaguliwa President na Abdul Sykes Vice-President.

Huu ndiyo ukweli wa historia yetu na sababu kwa nini ilikuwa hivi unafahamika na wala hakuna anaelamu kwa nini hawa waliukabili ukoloni kwa nini wale walikuwa pembeni.

Muhimu ni historia isibadilishwe kwa kuhofia ukweli kuwa Waislam wataonekana sana katika historia ya kupigania uhuru.

Kwa nini historia ya mchango huu wa Waislam ulifutwa katika maisha ya Nyerere?

Kwa nini, kwa nini, kwa nini?

Hivi ndivyo vilivyofanya kitabu changu kipate umaarufu kikatiwa pamoja na mwandishi katika Cambridge Journal of African History 1989 na katika Dictionary of African Biography (DAB) 2011.

Huu ni mwaka wa 11 niko JF nasomesha historia hii na sijamtukana mtu wala kughadhibika na sijamkejeli yeyote.

Ila ninachokiona mimi ni ghadhabu kwa nini nasomesha historia hii?

Leo tunasoma upya historia ya Mwalimu Nyerere na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

1679714043239.png

Kushoto: Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Dodoma Train Station 1955
1679714212971.jpeg

Kushoto: Rashid Sisso, Robert Makange, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafongo,, John Rupia, Bi. Titi Mohamed​
 
View attachment 2564494
Kushoto: Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Dodoma Train Station 1955
View attachment 2564495
Kushoto: Rashid Sisso, Robert Makange, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafongo,, John Rupia, Bi. Titi Mohamed​

Kuuza kadi za tanu misikitini hakumfanyi mtu kuwa shujaa. wapigania uhuru hawakupigania uhuru wa nchi hii kwa minajili ya sura za udini bali kwa ajili ya amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu. Kwamba ulitaka kadi za Tanu ziuzwe kanisani!! Ili iwaje kwanza? maana unapiganiwa uhuru wa nchi na sio kanisa. Sisi tumetenga kanisa na siasa wenzetu mnataka misikiti na siasa ndio maana unasema nyerere alibebwa mabegani mwa waislam, Ndio alibebwa ila mbinu zake ndio zimelikomboa taifa na kutoa dira wazee wengi kutoandikwa kwao hakuwafanyi wao wasiwe sehemu ya wapigania uhuru Mbona hata wazee wa kikristo wengi atukuwafahamu? kwamba nao ni wazee wa kariakoo!! Abdul sykes alilitambua uwezo wa hayati baba wa taifa mwalimu nyerere. Hayo maandamano ya maamuma wa kishia hio 2012 ni utoto why iwe parokia isiwe madrasa. Eti waislam wanajua ? Kwamba nchi hii Ina matatizo ya waislam tu au!!. Hoja hujibiwa na hoja sio vibwagizo vya mabango ya kejeli. Watu wanajenga mavyuo kila leo na mashule unaibuka mtu huna hata cheti cha kidato cha nne unaanza kuropoka hovyo. Njoo na mbinu na mikakati ya kutokomeza zero za waislam.
IMG_8032.jpg

IMG_8031.jpg

Ningefahamu kama wazee wa kawaida sana wa kariakoo kama nao waliweza pata fursa za kukaa kitako na watu wene historia za kutukuka Dunia hii.
 
Kuuza kadi za tanu misikitini hakumfanyi mtu kuwa shujaa. wapigania uhuru hawakupigania uhuru wa nchi hii kwa minajili ya sura za udini bali kwa ajili ya amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu. Kwamba ulitaka kadi za Tanu ziuzwe kanisani!! Ili iwaje kwanza? maana unapiganiwa uhuru wa nchi na sio kanisa. Sisi tumetenga kanisa na siasa wenzetu mnataka misikiti na siasa ndio maana unasema nyerere alibebwa mabegani mwa waislam, Ndio alibebwa ila mbinu zake ndio zimelikomboa taifa na kutoa dira wazee wengi kutoandikwa kwao hakuwafanyi wao wasiwe sehemu ya wapigania uhuru Mbona hata wazee wa kikristo wengi atukuwafahamu? kwamba nao ni wazee wa kariakoo!! Abdul sykes alilitambua uwezo wa hayati baba wa taifa mwalimu nyerere. Hayo maandamano ya maamuma wa kishia hio 2012 ni utoto why iwe parokia isiwe madrasa. Eti waislam wanajua ? Kwamba nchi hii Ina matatizo ya waislam tu au!!. Hoja hujibiwa na hoja sio vibwagizo vya mabango ya kejeli. Watu wanajenga mavyuo kila leo na mashule unaibuka mtu huna hata cheti cha kidato cha nne unaanza kuropoka hovyo. Njoo na mbinu na mikakati ya kutokomeza zero za waislam. View attachment 2566373
View attachment 2566376
Ningefahamu kama wazee wa kawaida sana wa kariakoo kama nao waliweza pata fursa za kukaa kitako na watu wene historia za kutukuka Dunia hii.
Ujamaa...
Kuuza kadi za TANU misikitini tulia ujiulize kwanini hazikuuzwa kanisani.

Ukiijua sababu itaondoka ajabu.

Lakini hata kama huwezi kutambua si neno.

Nyerere hakuwa peke yake katika historia ya uhuru.

African Association imeasisiwa na Kleist Sykes baada ya kukutana na Dr. Kwegyir Aggrey kutoka Achimota College Ghana mwaka 1924.

Dr. Aggrey ndiye aliyemtia hima Kleist aasisi African Association.

Unaweza kusoma historia hii katika "Modern Tanzanians," Iliffe (Ed) 1973.

(Halikadhalika katika Dictionary of African Biography (DAB) 2011).

Kleist anaeleza katika kitabu hicho kuwa Kanisa liliwaonya wafuasi wake kujiingiza katika siasa.

Angalia majina ya waasisi wa AA: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Kuiweka AA mbali na siasa za Waislam kwani AA ilikusudiwa kuwa chama cha wote, Kleist Sykes na Mzee bin Sudi wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.

Ziko wapi hapa hizo mbinu za Nyerere?

Sikatai mchango mkubwa wa Nyerere katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini mbona hujamtaja Hamza Mwapachu?

Au hujui mchango wake?

Mbonank hujamtaja Schneider Abdillah Plantan aliyesimama kidete kuwaingiza katika TAA Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes uongozi wa vijana ili waibadili TAA?

Huu ulikuwq mwaka wa 1950 na ikaundwa TAA Political Subcommittee wajumbe wakiwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir,Sheikh Said Chaurembo, John Rupia na Steven Mhando.

Ziko wapi hapa hizo mbinu za Nyerere?

Aliyemleta Nyerere TAA Dar-es-Salaam kwa kutambua uwezo wake si Abdul Sykes ni Hamza Mwapachu.

Abdul Sykes yeye alimtaka Chief David Kidaha Makwaia ndiye aongoze harakati za kudai uhuru.

Nakueleza haya babu yangu Salum Abdallah yumo katika harakati za kupambana na ukoloni toka enzi za AA hapa Dar-es-Salaam ya 1920 akiishi Mtaa wa Kipata sasa Mtaa wa Kleist Sykes.

Naijua historia historia hii kwani ni historia ya wazee wangu.

Umeweka picha ya Mao na Mandela wakiwa na Mwalimu.

Wakati wa miaka ya 1920 wakati wazee wetu wanaanza kujikusanya kupambana na wakoloni Mao hata hajafikia The Long March wala Mandela hajaanza harakati.

Lakini Afrika ilikuwa ikijifaharisha na Dr. Aggrey na Kleist alikutananae hapa Dar-es-Salaam.

Afrika ya Mashariki Kenya Jomo Kenyatta tayari alikuwa kiongozi wa watu wake.

Abdul Sykes alikutananae katika mkutano wa siri Nairobi 1950.

Ally Sykes alikuwa na mawasiliano na Kennett David Kaunda wa African National Congress (ANC) ya Northern Rhodesia toka 1953.

Nahitimisha.

NECTA ilikuwa inahujumu shule za Kiislam.

Tunao ushahidi.
 
Kwamba bwana salum abdallah nae alikuwa mpigania uhuru ?. Manamba nao kumbe walikua wanapigania uhuru. Hamza mwapachu alimtoa mwalimu wapi akamleta AA, why muongoza harakati asiwe babu yake dulli Sykes aka Abdul Sykes au huyo hamza mwapachu au dossa aziz au sheikh takadir why awe mwalimu afu kwa picha naona president walikua majina ya kikristu hapo hata aliemfungua kreist sykes nae ni mkatoliki, hapo kwa picha naona waasisi wa kupigania uhuru ni wakristu. Nacte haijawahi asilani kuhujumu shule za waislam, mlilalamika majina zikaja namba napo mkaendelea kuburuzwa, zimepita awamu kibao mpaka leo hii shule zenu zinaendelea kuburuzwa, si shule tu mpk watoto wa kiislam wanaendelea kushika mikia. Vipi mnahujumiwa bado??. Karibuni parokiani mpewe ushauri ili kuongeza ufaulu wa shule zenu.
 
Salum Abdallah babu yangu hakuwa manamba.
Sisemi kuwa manamba ni watu duni la hasha ili hakuwa manamba.

Kazi yake ilikuwa mfua chuma.
Aliajiriwa kwa kazi hiyo na Tanganyika Railways katika miaka ya 1920.

Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walijuana Makerere.

(Ukiandika uhuni ''babu yake Dully Sykes'' kadha wa kadha unanipa shida kwani huu kwangu ni mjadala wa kistaarabu si mjadala wa kejeli).

Angalia post yangu ya mwisho vipi ninavyoandika na kueleza historia ambayo haikuwa inafahamika kabla.

Kwa nini Hamza Mwapachu hakutakiwa kuchukua uongozi wa TAA na kuunda TANU au kwa nini Abdul Sykes hakuchukua au kwa nini Chief Kidaha Makwaia hakuchukua hizi zote ni historia za kusisimua.

Historia hii hakuna aliyepata kuandika ila mimi baada ya kusoma Nyaraka za Sykes na kuandika kitabu.

Kuhusu NECTA nina mengi ambayo naweza nikayaweka hapa kwa ushahidi na sote tukanufaika kwa taarifa hizo hata kama wewe hutoamini.

Lakini ili tufanye mjadala wenye tija muhimu kwanza tukaheshimiana.
 
Kwamba bwana salum abdallah nae alikuwa mpigania uhuru ?. Manamba nao kumbe walikua wanapigania uhuru. Hamza mwapachu alimtoa mwalimu wapi akamleta AA, why muongoza harakati asiwe babu yake dulli Sykes aka Abdul Sykes au huyo hamza mwapachu au dossa aziz au sheikh takadir why awe mwalimu afu kwa picha naona president walikua majina ya kikristu hapo hata aliemfungua kreist sykes nae ni mkatoliki, hapo kwa picha naona waasisi wa kupigania uhuru ni wakristu. Nacte haijawahi asilani kuhujumu shule za waislam, mlilalamika majina zikaja namba napo mkaendelea kuburuzwa, zimepita awamu kibao mpaka leo hii shule zenu zinaendelea kuburuzwa, si shule tu mpk watoto wa kiislam wanaendelea kushika mikia. Vipi mnahujumiwa bado??. Karibuni parokiani mpewe ushauri ili kuongeza ufaulu wa shule zenu.
 
"Kuhusu NECTA nina mengi ambayo naweza nikayaweka hapa kwa ushahidi na sote tukanufaika kwa taarifa hizo hata kama wewe hutoamini. "

Mzee Mohamed Said ningependa kama utaweza utuwekee hapa hizo taarifa tupate kujua tusiyoyajua [emoji120]
 
Back
Top Bottom