Ujamaa..
Mimi sina tatizo kujibu maswali kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kote nilikoalikwa toka kitabu changu kichapwe naulizwa na najibu maswali.
Bango la Parokia picha hiyo nimepiga katika maandamano ya Waislam dhidi ya NECTA mwaka 2012.
Nimeweka hilo bango kueleza kuwa nchi yetu ina matatizo.
Wewe hukuona umuhimu wa bango hilo lakini Waislam wameona umuhimu wa kulibeba serikali ilisome na itambue nini kinalalamikiwa.
Ikiwa hujui historia ya haya maandamano nifahamishe nikueleze.
Mimi nimeeleza historia ya kweli ya Nyerere kuliko mwandishi yeyote kabla yangu ingawa watu kama wewe wanaona tabu na sababu ya dhiki hii inafahamika.
Wanaumizwa na ukweli kuwa kwa nini Nyerere alibebwa katika mabega ya Waislam wakati wa kupigania uhuru.
Picha za kudai uhuru ni shahidi wa hili.
Kwa nini Mufti Sheikh Hassan bin Ameir aliuza kadi za TANU misikitini.
Kwa nini Kadinali Rugambwa hakuuza kadi za TANU kanisani.
Kwa nini hafla ya kumuaga Mwalimu safari ya kwanza UNO 1955 ilifanyika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?
Kwa nini haikufanyika Parish Hall St. Joseph's Cathedral?
Kwa nini mkusanyaji fedha za safari hiyo alikuwa Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul na ndiye pia alikuwa Mweka Hazina wa TANU kadi yake no. 24 na ya nduguye Iddi Tosiri kadi no. 25.
Hawa walihuidhuria mkutano wa kwanza za TANU August 1954 Ukumbi wa Arnautoglo na ndugu hawa wawili ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo kwa Sheikh Mohamed Ramiyya.
Ndugu hawa walikuwapo pia katika uchaguzi wa mwaka wa 1953 wa kuchagua President wa TAA uliofanyika hapo hapo Arnautoglo Hall kati ya Abdul Sykes na Julius Nyerere na Nyerere akachaguliwa President na Abdul Sykes Vice-President.
Huu ndiyo ukweli wa historia yetu na sababu kwa nini ilikuwa hivi unafahamika na wala hakuna anaelamu kwa nini hawa waliukabili ukoloni kwa nini wale walikuwa pembeni.
Muhimu ni historia isibadilishwe kwa kuhofia ukweli kuwa Waislam wataonekana sana katika historia ya kupigania uhuru.
Kwa nini historia ya mchango huu wa Waislam ulifutwa katika maisha ya Nyerere?
Kwa nini, kwa nini, kwa nini?
Hivi ndivyo vilivyofanya kitabu changu kipate umaarufu kikatiwa pamoja na mwandishi katika Cambridge Journal of African History 1989 na katika Dictionary of African Biography (DAB) 2011.
Huu ni mwaka wa 11 niko JF nasomesha historia hii na sijamtukana mtu wala kughadhibika na sijamkejeli yeyote.
Ila ninachokiona mimi ni ghadhabu kwa nini nasomesha historia hii?
Leo tunasoma upya historia ya Mwalimu Nyerere na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
View attachment 2564494
Kushoto: Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Dodoma Train Station 1955
View attachment 2564495
Kushoto: Rashid Sisso, Robert Makange, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafongo,, John Rupia, Bi. Titi Mohamed