Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Sina neno na wewe.
Nipo hapa kwa minajiri ya Mzee Mohamed Said.
Asante sana kwa kunivumilia.
Sema ukweli, tupe historia ya babu yako alikuwa wapi wakati babu yake Mohamed Said anapigania Uhuru.

Bila shaka alikuwa kilabuni anakunywa juisi inayoitwa mataputapu.
 
Sema ukweli, tupe historia ya babu yako alikuwa wapi wakati babu yake Mohamed Said anapigania Uhuru.

Bila shaka alikuwa kilabuni anakunywa juisi inayoitwa mataputapu.
MaalimFaiza,
Katika kitabu hiki: Tandau, A. C. A., Historia ya Kuundwa Kwa TFL (1955-1962) na Kuanzishwa kwa NUTA, Dar es Salaam, Mwananchi Publishing Company, 1964, mwandishi anaeleza historia ya vyama vya wafanyakazi.

Ndani ya kitabu hiki hamna kitu.

Chanzo kikubwa cha Nyerere kutaka kuwe na chama kimoja cha wafanyakazi wote wa Tanganyika chini ya TANU ni mgomo wa 1960 uliodumu siku 82 (miezi mitatu).

Katika viongozi wa mgomo ule alikuwa babu yangu Salum Abdallah na Kassanga Tumbo wote viongozi kutoka Tanganyika Railways African Union (TRAU).

Mgomo huu ulikuja miezi michache kabla ya Tanganyika kupata madaraka ya ndani.

Nchi ilisimama hadi pale walipokubaliana na wafanyakazi wakarudi kazini.

Nyerere aliingia hofu kuwa iko siku katika Tanganyika huru atapambana na Salum Abdallah na Kassanga Tumbo.

Ukisoma kitabu cha Tandau historia hii haipo.
Babu yangu mbali ya siasa alikuwa bingwa wa kucheza bao.

Babu yangu alikuwa akija Dar es Salaam kutoka Tabora mimi mtoto mdogo nikimsindikiza Mtaa wa Mafia na Congo pale kulikuwa na barza kubwa ya wazee wa Dar es Salaam wakicheza bao.

Barza hii sisi tumezaliwa tumeikuta pale.
Barza hii ilikuwa barza ya wazee wa TANU wapigania uhuru.

Leo wakiwa na hamu ya kutukana wanawatukana wazee hawa na kukejeli bao.

Mimi sishangai kwanza kwa kufutwa historia ya wazee hawa na pili wala sishangai mimi kutukanwa kwa kuandika historia hii.

Maalim umeuliza swali zuri sana.
Babu yake alikuwa wapi?

Hakika sisi hatuwezi kuwalaumu kwa nini hawakuwa mstari wa mbele wala wala hatuwezi kuwatukana na kuwakejeli.

Sisi tumeleleka makwetu.
Mama zetu wametufunza adabu.

1679563915851.jpeg

Viongozi wa TRAU
Kassanga Tumbo kulia ya Salum Abdallah (mshale)​
 
IMG_7996.jpg

Bila juhudi za huyu mwamba sijui uhuru tungepata wapi. Kama sio juhudi zako myerere na uhuru tungepata wapi. Uhuru, umoja na amani ndio ngao hayati mwalimu aliotuachia. hakika mtu huyu atadumu moyoni mwa vizazi na vizazi.
 
Sema ukweli, tupe historia ya babu yako alikuwa wapi wakati babu yake Mohamed Said anapigania Uhuru.

Bila shaka alikuwa kilabuni anakunywa juisi inayoitwa mataputapu.
Sina wakati nawe kwa sasa hivi. Huu ni wakati maalum kwa mzee Mohamed Said.

Jaribu tena siku nyingine.
 
Sina wakati nawe kwa sasa hivi. Huu ni wakati maalum kwa mzee Mohamed Said.

Jaribu tena siku nyingine.
Sema huna babu au baba mwenye lolote katika historia ya uhuru.

alama Mohamed Said amekufanya uwe na roho ya kuchukia kupenda (hate to love) , yaani unachukia kwanini unaipenda historia yake. Hivi ubangoja nondo zake kwa hamu kubwa.
 
Narudia, lete maombi siku nyingine. Sasa hivi ninayo kazi tayari niliyopewa na mzee.
 
Ukipenda usipende lazima utaipenda kazi ya "mzee".
Najuwa kuna mfanano wa karibu sana kati yako na mzee. Mzee 'boss', kama ni wewe unakuja kivingine, niwie radhi, mimi nakusubiri wewe tu!
 
Najuwa kuna mfanano wa karibu sana kati yako na mzee. Mzee 'boss', kama ni wewe unakuja kivingine, niwie radhi, mimi nakusubiri wewe tu!
Muite tu kwa jina lake atakuja kukupa vitu, usione haya.
 
Tunataka Historia ya Tunduru, Namtumbo, Sumbwanga, Njombe, Mara, Geita, Karatu, Loliondo, Mwandiga n.k. Tunataka historia ya zamani ya wazee wote wa nchi hii, sio kutujazia historia ya wazee wako wa Kariakoo tu.
Soph...
Hupendi kusoma historia ya Dar-es-Salaam ya zamani?

Inaelekea watu wengi wanavutiwa.
Tuko 8K ...and counting...
 
Tunataka Historia ya Tunduru, Namtumbo, Sumbwanga, Njombe, Mara, Geita, Karatu, Loliondo, Mwandiga n.k. Tunataka historia ya zamani ya wazee wote wa nchi hii, sio kutujazia historia ya wazee wako wa Kariakoo tu.
Yoda,
Huko ulikotaja ilichukua muda TANU kuingia na kukubalika.

Nakupa mfano wa Southern Province.

Lindi akina Masudi Mnonji walifungua tawi la TANU tatizo lililowakuta lilikuwa kutoka Misheni ya Peramiho.

Propaganda ilikuwa inaenezwa kuwa Waislam wanataka kuanzisha Maji Maji nyingine dhidi ya Waingereza.

Salum Mpunga na Ali Mnjawale wakatumwa Dar-es-Salaam kuja kuonana na uongozi wa juu wa TANU wamlete Julius Nyerere kupambana na propaganda hizi.

Nyerere alikwenda Lindi akifuatana na Rajab Diwani na Ali Mwinyi Tambwe.

Kisa hiki ni kitamu sana ikiwa utapenda nitakiweka hapa kutoka kitabu cha Abdul Sykes.

Hawa ndiyo wazee wangu na ndiyo waliyofanya haya.

Ikiwa wewe historia hii inakuchukiza unataka ya wazee kutoka hizo sehemu ulizotaja ukweli ni kuwa huko hapakuwa na kitu.

Lindi wamempa Sheikh Mohamed Yusuf Badi Mtaa kwa mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika:

1679583499398.jpeg

336912184_1207764543441023_4470879998552687397_n.jpg

Rajab Diwani​
 
Au tuseme basi kakutuma wewe ukaimu nafasi yake?
Sitaendelea nawe hapa, mpaka aje mwenyewe.
AlhamduliLlah Hahitaji kaimu wala msaidizi, anajimudu mwenyewe tena sana, atakuja kwa wakati wake.
 
Ukipenda usipende lazima utaipenda kazi ya "mzee".
MaalimFaiza,
Mwenyezi Mungu ana njia za ajabu sana anapotaka jambo lake liwe.
Leo hapa huyu bwana kanipa nafasi ya kuisomesha historia ya TANU.

Yeye anakuja na maneno hayana maana yoyote.

Mimi namjibu kwa picha za historia ya TANU na maneno zaidi ya 300 yenye historia ya uhuru wa Tanganyika.

Atajibu ukipenda kutukana kwa maneno yale yale hayabadiliki.
Nitamjibu kwa kutoa darsa pamoja na picha.

Atatukana matusi yale yale na mimi nitarejea tena na historia nyingine.

Huyu ni mtu wa kuengwa tuwe na yeye hapa hadi kitabu changu cha kurusa 415 kikamilike.

Insha Allah tutakuwa na kitabu kizima hapa ambayo ni rejea kwa yeyote anaetaka kusoma historia ya TANU ambayo ndani yake kuna wazalendo wote pamoja na picha za nyakati hizo.
 
Kakutukana kasemaje? Bado unaleta tena porojo
Marashi,
Kanitukana mara nyingi siwezi kurejea matusi yake si adabu wala ustaarabu.
Soma post zake angalia anavyoandika.

Soma post zangu angalia majibu yangu kisha rejea hapa unifahamishe kama unaona anafanya sawa.
 
Back
Top Bottom