Sema ukweli, tupe historia ya babu yako alikuwa wapi wakati babu yake
Mohamed Said anapigania Uhuru.
Bila shaka alikuwa kilabuni anakunywa juisi inayoitwa mataputapu.
MaalimFaiza,
Katika kitabu hiki: Tandau, A. C. A.,
Historia ya Kuundwa Kwa TFL (1955-1962) na Kuanzishwa kwa NUTA, Dar es Salaam, Mwananchi Publishing Company, 1964, mwandishi anaeleza historia ya vyama vya wafanyakazi.
Ndani ya kitabu hiki hamna kitu.
Chanzo kikubwa cha Nyerere kutaka kuwe na chama kimoja cha wafanyakazi wote wa Tanganyika chini ya TANU ni mgomo wa 1960 uliodumu siku 82 (miezi mitatu).
Katika viongozi wa mgomo ule alikuwa babu yangu Salum Abdallah na Kassanga Tumbo wote viongozi kutoka Tanganyika Railways African Union (TRAU).
Mgomo huu ulikuja miezi michache kabla ya Tanganyika kupata madaraka ya ndani.
Nchi ilisimama hadi pale walipokubaliana na wafanyakazi wakarudi kazini.
Nyerere aliingia hofu kuwa iko siku katika Tanganyika huru atapambana na Salum Abdallah na Kassanga Tumbo.
Ukisoma kitabu cha Tandau historia hii haipo.
Babu yangu mbali ya siasa alikuwa bingwa wa kucheza bao.
Babu yangu alikuwa akija Dar es Salaam kutoka Tabora mimi mtoto mdogo nikimsindikiza Mtaa wa Mafia na Congo pale kulikuwa na barza kubwa ya wazee wa Dar es Salaam wakicheza bao.
Barza hii sisi tumezaliwa tumeikuta pale.
Barza hii ilikuwa barza ya wazee wa TANU wapigania uhuru.
Leo wakiwa na hamu ya kutukana wanawatukana wazee hawa na kukejeli bao.
Mimi sishangai kwanza kwa kufutwa historia ya wazee hawa na pili wala sishangai mimi kutukanwa kwa kuandika historia hii.
Maalim umeuliza swali zuri sana.
Babu yake alikuwa wapi?
Hakika sisi hatuwezi kuwalaumu kwa nini hawakuwa mstari wa mbele wala wala hatuwezi kuwatukana na kuwakejeli.
Sisi tumeleleka makwetu.
Mama zetu wametufunza adabu.
Viongozi wa TRAU
Kassanga Tumbo kulia ya Salum Abdallah (mshale)