Jimmywatanzania
JF-Expert Member
- May 8, 2015
- 514
- 274
Atalipwa mbinguni na Allah!Kwa bahati nzuri nilibahatika kuhudhuria maziko ya dosa pale mlandizi,nilisikitika kwa mengi lakini kubwa hata kula na vaa yake ilikuwa shida mno.alisahaulika kabisa.huyu hakuna dereva bali mtu mwenye uwezo wake,enzi hizo alimiliki malori kadhaa,alijitoa kifedha mno mpaka kuuza baadhi ya mali zake ili kusaidia uhuru.
Cc Mohamed said.Ni wapi Julius Nyerere aliwazidi "ujanja" wazee wa mjini,born town na Watoto wa K'koo? Wazee wake na gwiji wetu wa historia Mohamed Said
Ukifuatilia historia na harakati za Uhuru,unaona kuwa huyu kijana wa Kizanaki,mtoto wa Chief na "mvaa kaptula" alikuja baadae sana Dsm wakati wenzake wakiwa mjini kitambo na harakati za kumuondoa Mkoloni.Wakati Julius anakuja Dsm tayari harakati za Uhuru zilikuwa zimepamba moto.
Maelezo mengi ya Wazee yanaonyesha Julius aliaminiwa mapema sana na kupewa madaraka ndani ya chama na hatimaye baadae kuja kuwa Rais wa TAA/TANU na hatimaye nchi.Vijana wenzake waliompokea mjini wakebaki kuwa wao wao watoto wao na wajukuu wao kuwa Julius baada ya Uhuru "aliwasahu"
Wazee wengi wanahisi Julius aliwazidi ujanja na kuwaweka kando baada ya kuchukua nchi.Mitaa ya Kata ya Ng'ambo Tabora,miaka kumi iliyopita nilipata kuwaona wazee wawili,wajanja wa mjini waliompokea Nyerere ktk harakati zake mkoa wa Tabora.Mzee mmoja akiitwa Pacha,akiishi eneo la "filter" pembeni ya kilabu moja maarufu ya pombe mjini Tabora.Mzee mwingine akiitwa Rehani.Huyu kwa heshima kuna mtaa Tabora uliopewa jina lake.Unaitwa mtaa wa Rehani.Kuna Rehani A na Rehani B.
Hawa wote ukikaa nao watakuambia "Julius ni mjanja sana,alituzidi maarifa".Ukija K'koo kuna wazee wengi wapo na malalamiko na wengine wamekufa nayo.Sikumbuki ni Sykes yupi kati ya hao naowasikia.Lkn miaka miwili au mitatu iliyopita...Jijini Nairobi,kwenye Uwanja mdogo wa ndege wa maarufu kama "Wlison Airport" majira ya adhuhuri kuelekea alasiri.Nakutana na Wanawake wawili.Moja Mama wa makamo na mwingine mdada wa umri wa juu kidogo.Huyu Mama bila shaka ni mke wa marehemu na huyu wa pili bintiye.
Hawa wanajiandaa kupakia mwili wa ndugu yao,ni marehemu.Maafisa wa Uhamiaji wanatazama passport zao za kusafiria na kuona ni pass za kidiplomasia.Wanatakiwa kuusafirisha mwili wa ndugu yao kuja Dsm.Wamekodi ndege ndogo aina ya C208.Yenye uwezo wa kubeba watu wanne tu.Lakn wale wanawake wakiwa na ndugu wengine wanakubaliana kubeba maiti na wao kuja Dsm.
Ndege ndogo,ktk ubanano na majonzi ya msiba wale wamama wanabanana na maiti ikiwa ndani ya mkeka kuileta Dsm.Ndege ya C206 ni ndogo sana kwa umbali wa Nairobi to Dsm,tena ukiwa na maiti,na hasa kwa wanawake.Kuuliza kwa ndugu waliobaki pale Uwanjani kufanya mpango wa kwenda Jomo Kenyatta ili waje Dsm,wanasema huyo alipata kuwa mpigania uhuru wa Tz,balozi mashuhuri na mwanadiplomasia mbobezi.
Pale pale wanaanza kung'aka kuwa hawa ni wapigania uhuru waliosahaulika na nchi,ndio maana wanabebwa na ndege ndogo aina ya C206 kurudi kwao.Ni malalamiko tu ya "kusahauliwa" muda wote wa maongezi yao.
Akija humu Mzee wangu Mohamed Said,atakutajia kina Mshume Kiyate(?),atataja kina Dosa,mara kina Tewa Said Tewa na wengine wengi kuwa hawa nao hawakufaidi matunda ya Uhuru.Hivi kwani huyu Julius alikuwa na ujanja kiasi gani hawa wote akawaingiza "mjini" wakati wao ndio waliompokea?
Nilitembelea Kilwa,kule kuna Kilwa ya Kivinje na Kilwa Kipatini.Huku Kilwa Kipatini ndio kwao na Kingunge.Huku kuna Kanisa kongwe sana la miaka mingi walijenga Wajerumani.Kanisa hili ndipo alibatizwa Kingunge N. Mwiru.Wengi hudhanj Kingunge hakuwahi kuwa na dini kabisaaa...Kumbe huyu ni mbatizwa ktk Kristo,kabla ya kwenda Usoviet na kuachana na dini.Lkn kwa kubatizwa huyu anaitwa "Ambrose Ngombare Mwiru".
Huku Kivinje kuna watu nao wanasema "Julius alituzidi ujanja"...Hivi huu "ujanja" waliozidiwa hawa wote ni kwa sbb ya nini?Ni kwanini walimpokea na kumpa uongozi halafu baadae walalamike?Kwanini wasingemnyima?Je baada ya Uhuru hawa "walalamishi" wote walitaka Julius afanye nini ili walidhike?
Leo ninaomba majibu,nijue,ni wapi Julius,kijana wa Kizanaki aliwazidi "ujanja" hawa vijana wa mjini wa K'koo??
Cc Ngongo UncleBen Barbarosa Ritz
Jiwe...Nyerere alikua kichwa na smart sana,kuunganisha watanzania sio suala dogo.
JKs wote akili kubwa sanaNyerere alikuwa mwanamikakati hodari sana.
Yoda,Nyerere alikuwa mwanamikakati hodari sana.
Huyu Julius alikuwa mjanja sana kupata madaraka na kuweza kuyalinda ndio maana alitawala mpaka akachoka.Ni wapi Julius Nyerere aliwazidi "ujanja" wazee wa mjini,born town na Watoto wa K'koo? Wazee wake na gwiji wetu wa historia Mohamed Said
Ukifuatilia historia na harakati za Uhuru,unaona kuwa huyu kijana wa Kizanaki,mtoto wa Chief na "mvaa kaptula" alikuja baadae sana Dsm wakati wenzake wakiwa mjini kitambo na harakati za kumuondoa Mkoloni.Wakati Julius anakuja Dsm tayari harakati za Uhuru zilikuwa zimepamba moto.
Maelezo mengi ya Wazee yanaonyesha Julius aliaminiwa mapema sana na kupewa madaraka ndani ya chama na hatimaye baadae kuja kuwa Rais wa TAA/TANU na hatimaye nchi.Vijana wenzake waliompokea mjini wakebaki kuwa wao wao watoto wao na wajukuu wao kuwa Julius baada ya Uhuru "aliwasahu"
Wazee wengi wanahisi Julius aliwazidi ujanja na kuwaweka kando baada ya kuchukua nchi.Mitaa ya Kata ya Ng'ambo Tabora,miaka kumi iliyopita nilipata kuwaona wazee wawili,wajanja wa mjini waliompokea Nyerere ktk harakati zake mkoa wa Tabora.Mzee mmoja akiitwa Pacha,akiishi eneo la "filter" pembeni ya kilabu moja maarufu ya pombe mjini Tabora.Mzee mwingine akiitwa Rehani.Huyu kwa heshima kuna mtaa Tabora uliopewa jina lake.Unaitwa mtaa wa Rehani.Kuna Rehani A na Rehani B.
Hawa wote ukikaa nao watakuambia "Julius ni mjanja sana,alituzidi maarifa".Ukija K'koo kuna wazee wengi wapo na malalamiko na wengine wamekufa nayo.Sikumbuki ni Sykes yupi kati ya hao naowasikia.Lkn miaka miwili au mitatu iliyopita...Jijini Nairobi,kwenye Uwanja mdogo wa ndege wa maarufu kama "Wlison Airport" majira ya adhuhuri kuelekea alasiri.Nakutana na Wanawake wawili.Moja Mama wa makamo na mwingine mdada wa umri wa juu kidogo.Huyu Mama bila shaka ni mke wa marehemu na huyu wa pili bintiye.
Hawa wanajiandaa kupakia mwili wa ndugu yao,ni marehemu.Maafisa wa Uhamiaji wanatazama passport zao za kusafiria na kuona ni pass za kidiplomasia.Wanatakiwa kuusafirisha mwili wa ndugu yao kuja Dsm.Wamekodi ndege ndogo aina ya C208.Yenye uwezo wa kubeba watu wanne tu.Lakn wale wanawake wakiwa na ndugu wengine wanakubaliana kubeba maiti na wao kuja Dsm.
Ndege ndogo,ktk ubanano na majonzi ya msiba wale wamama wanabanana na maiti ikiwa ndani ya mkeka kuileta Dsm.Ndege ya C206 ni ndogo sana kwa umbali wa Nairobi to Dsm,tena ukiwa na maiti,na hasa kwa wanawake.Kuuliza kwa ndugu waliobaki pale Uwanjani kufanya mpango wa kwenda Jomo Kenyatta ili waje Dsm,wanasema huyo alipata kuwa mpigania uhuru wa Tz,balozi mashuhuri na mwanadiplomasia mbobezi.
Pale pale wanaanza kung'aka kuwa hawa ni wapigania uhuru waliosahaulika na nchi,ndio maana wanabebwa na ndege ndogo aina ya C206 kurudi kwao.Ni malalamiko tu ya "kusahauliwa" muda wote wa maongezi yao.
Akija humu Mzee wangu Mohamed Said,atakutajia kina Mshume Kiyate(?),atataja kina Dosa,mara kina Tewa Said Tewa na wengine wengi kuwa hawa nao hawakufaidi matunda ya Uhuru.Hivi kwani huyu Julius alikuwa na ujanja kiasi gani hawa wote akawaingiza "mjini" wakati wao ndio waliompokea?
Nilitembelea Kilwa,kule kuna Kilwa ya Kivinje na Kilwa Kipatini.Huku Kilwa Kipatini ndio kwao na Kingunge.Huku kuna Kanisa kongwe sana la miaka mingi walijenga Wajerumani.Kanisa hili ndipo alibatizwa Kingunge N. Mwiru.Wengi hudhanj Kingunge hakuwahi kuwa na dini kabisaaa...Kumbe huyu ni mbatizwa ktk Kristo,kabla ya kwenda Usoviet na kuachana na dini.Lkn kwa kubatizwa huyu anaitwa "Ambrose Ngombare Mwiru".
Huku Kivinje kuna watu nao wanasema "Julius alituzidi ujanja"...Hivi huu "ujanja" waliozidiwa hawa wote ni kwa sbb ya nini?Ni kwanini walimpokea na kumpa uongozi halafu baadae walalamike?Kwanini wasingemnyima?Je baada ya Uhuru hawa "walalamishi" wote walitaka Julius afanye nini ili walidhike?
Leo ninaomba majibu,nijue,ni wapi Julius,kijana wa Kizanaki aliwazidi "ujanja" hawa vijana wa mjini wa K'koo??
Cc Ngongo UncleBen Barbarosa Ritz
Hizi mada zinazomhusu Mwalimu na hili kundi maalum huwa najaribu sana kuiepa nisishiriki kwa sababu najua msukumo wa mijadala hii ni nini hasa.Huyu Julius alikuwa mjanja sana kupata madaraka na kuweza kuyalinda ndio maana alitawala mpaka akachoka.
Huenda hata mabeberu waliupenda ujanja wake wakati mwingine
Ila kuistawisha nchi kiuchumi hakuwa na huo ujanja kabisa.
Pascal Mayalla JokaKuu zitto junior Kalamu Mohamed Said brazaj
Lakini nikushukuru mkuu'Proved', kwa kuniita hapa. Hii mada ya Mkuu Barafu nilikuwa sijaiona hapa jukwaani ilipoletwa.Huyu Julius alikuwa mjanja sana kupata madaraka na kuweza kuyalinda ndio maana alitawala mpaka akachoka.
Huenda hata mabeberu waliupenda ujanja wake wakati mwingine
Ila kuistawisha nchi kiuchumi hakuwa na huo ujanja kabisa.
Pascal Mayalla JokaKuu zitto junior Kalamu Mohamed Said brazaj
Ante...Najiuliza! Mkakati huu wa kuhakikisha mashujaa na wapambanaji hawa wa tanganyika yetu, wanafichwa kabisa hata wasisomwe popote kama moja ya watu muhimu katika harakati za uhuru, ni nan aliekuwa anaushughulikia? Mana yote waliokuwa wakiyafanya wao pamoja na nyerere, hayakufanyika gizani wala mafichoni..! Mpaka miaka ya 80's, 90's na mwanzoni mwa 2000's naamini bado palikua na wazee wengi sana waliopata kuyashuhudia yote haya! Sasa nguvu kubwa ya kuwafumba midomo wote hawa ilitoka kwa nani na lengo hasa likiwa ni nin? Yani, lengo la kuwaziba vinywa kiasi asipatikane hata mmoja wa kuyanena haya nin? Ni kitu gan kilihofiwa kutokea endapo history hii ingeachwa wazi? Je kitu hicho ni positive au negative kwa taifa?
Kalamu,Hizi mada zinazomhusu Mwalimu na hili kundi maalum huwa najaribu sana kuiepa nisishiriki kwa sababu najua msukumo wa mijadala hii ni nini hasa.
Sasa unaniita nijadili jambo ambalo ni wazi kabisa kwamba hao wazee wa Kariakoo dunia yao iliishia Magomeni, zaidi ya hapo hawakujuwa uwepo wa Tanganyika nzima na waTanganyika huko kwingine?
Hata hapo Kariakoo penyewe, unaweza kupata nyaraka na kumbukumbu za mikutano walizozifanya kuwa ushahidi wa kupigania uhuru wa Kariakoo?
Hizi nilishazisoma mara ya kwanza ulipoziweka humu JF; kwa hiyo siyo ngeni kwangu.Kalamu,
Soma makala hapo chini:
KUTOKA MAKTABA: MKUTANO WA SIRI KATI YA ABDUL SYKES NA JOMO KENYATTA NAIROBI 1950
Siku moja katika mazungumzo na Ahmed Rashad Ali akanambia kuwa mwaka wa 1950 yeye akiwa Nairobi wakati wa mashindano ya Gossage Cup Abdul Sykes alifika Nairobi na akawa anakaa Railway Hotel.
Ahmed Rashad alikuwa nahodha wa timu ya Zanzibar.
Abdul alimfuata kwenye kambi yao akamwambia amekuja Nairobi kuonana na Jomo Kenyatta na akamtaka amsindikize.
Leo asubuhi katika pitapita yangu Maktaba nimeikuta taarifa ya Special Branch kuhusu mktano wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta nami nakuwekeeni hapa barzani:
Kalamu,Hizi nilishazisoma mara ya kwanza ulipoziweka humu JF; kwa hiyo siyo ngeni kwangu.
Mimi nimejibu kwa niaba yangu, hayo ya wengine siyajui.Kalamu,
Kwako si mageni haya lakini kuna wengine ndiyo hii leo kwa mara ya kwanza anasoma kuwa Abdul Sykes alikutana na Jomo Kenyata na viongozi wengine wa KAU Nairobi 1950 na anaona kwa macho yake ushahidi wa mkutano ule kutoka taarifa za kikachero za Special Branch.
Kalamu,Mimi nimejibu kwa niaba yangu, hayo ya wengine siyajui.
Kwa bahati mbaya umeniwekea mimi hapo ulipoiweka.Kalamu,
Mimi ninapoweka somo hapa huikusudia dunia nzima.