Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,663
Tusubiri wataalamu
Sawa Mkuu
Nitasubiri kama ulivyonipa subra!!
Tusubiri wataalamu waje
Tarehe n 30 mpk 2 then inakuja kwenye 8 mpk 10.
Kitu ambacho nilishauriwa mm, ni kuacha stress kabisa...
Yamkini hata ukiijua tarehe lkn ww au mwenza wako hamjatulia vzr mimba inakua ngumu kushika...
Mkuu punguza stress kbs.Kushika kwa ujauzito haiitaji uwe na stress.Relax wewe na shemeji.Kingine cheki tym nenda kwa tabibu wewe na shemeji.Thn eleza tatizo kwa watalaam watakupa majibu mazuri.Na pia check afya yako na ya shem kwenye ability ya kushika ujauzito.Kutokushika ujauzito kuna sababu nyingi saana...ikiwamo kuwepo na stress kati yenu,magonjwa mf U.T.I,S.TD haswaa syphilis,kuna lishe nzuri inahitajika ktk kurutubisha sperms ziweze kuwa na ability ya kufanya jambo wkt zkutanavyo na yai,pia lishe inahitajika kwa mwanamke ktk kuweka yai kuwa active,pia kuna matatizo ya mirija ya uzazi kuziba kwa kusababishwa na magonjwa hasa S.T.D,kuna mabo ya hormones etc,so kuna mambo mengi ya kucheki bro ktk kupata ujauzito ktk familia yak😵nana na specialists watabaini tatizo nini kati ya haya niliokueleza.Ni hayo tu.
Mshirikishe Mungu
^^
Inawezekana ni kweli na hofu yako isiwe ya msingi wowote!
Maumbile ya wanawake hutofautiana sana hasa ktk mifumo ya ufanyaji kazi wa mwili ktk uzazi.
Na linapokuja suala la mimba ni haki yake kuwa tofauti kwa mabadiliko ya nje au ndani ya mwili.
La msingi, nenda hospitali mupata ushauri wa kitaalam.
Wala hutakiwi kuhofu ndio maana mimba hazitungwi siku moja kuepuka tabia za aina moja kwa watu duniani.
^^
Uwezekano wa mimba kutungwa huongezeka kama tendo la ngono litafanyika kati ya siku ya 12 hadi 16 ya mzunguko wa hedhi ya mwanamke. Hata hivyo, ili uhakika wa kutunga mimba uwepo, na ni lazima kila kimoja ya hatua zifuatazo kikamilike bila dosari:
(1) Mbegu za kiume zilizokomaa na zisizo na ulemavu
(2) Yai la kike lililokomaa na limetoka kwenye Ovary kuanza safari kuja kwenye fallopian tubes
(3) Tendo la ngono linalofanikishwa na uume uliosimama na unaoweza kuingia katika via vya uzazi vya mwanamke
(4) Mbegu za kiume kumwagwa na kusafiri katika via vya uzazi vya mwanamke hadi kwenye fallopian tubes
(5) Kukutana kwa mbegu za kiume na yai la mwanamke katika fallopian tubes
Mleta mada, tumia hii checklist ujue ni wapi mnapata changamoto
No(1)Sasa unaposema Mbegu za Kiume ziluzokomaa unamaanisha nini wakati mtu yeyote mwenye umri wa Miaka 18, Huwa amekomaa.
Kwako Mama Mdogo
Unadhani wanaume walioko katika kundi hili wafanye nini ili waweze kuwa sperm zilizojitosheleza Mama MdogoKufikisha umri wa miaka 18 si hoja. Shahawa alizozalisha mwanaume aliye na umri wa miaka 18 au zaidi zaweza zisikomae kutokana na upungufu wa vichocheo (hormones), kupigwa mionzi (radiation), urithi (genetic), matumizi ya dawa za kulevya au pombe, busha, kuvimba tezi za kooni ukubwani (adult mumps), athari za dawa za kuua wadudu na lishe hafifu. Upo hapo??? Hivyo mwanamme waweza kuwa unazunguka wee na sruali yako kumbe mbegu zako hazikomai, majanga!!
Unadhani wanaume walioko katika kundi hili wafanye nini ili waweze kuwa sperm zilizojitosheleza Mama Mdogo
Mungu ni jambo la kwanza mkuu!
Sidhani kama kuna mtu atambui uwepo wa Mungu