Ni kwa namna gani ndoa itakuwa chachu ya mafanikio katika maisha hasa kwa vijana.

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Moja ya taasisi kongwe saana duniani ni "familia". Familia ndiyo kiunganishi cha kwanza cha jamii. Jamii iliyoungana siku zote hufanikiwa kwa kila jambo lifabyikalo.

Hivyohivyo, Familia/wanandoa walioamua kuungana na kuishi pamoja mafanikio watakayo pata ni makubwa tofauti na ambavyo wasingekuwa wameunganisha nguvu zao.

Wote tunajifunza hapa, hasa mimi. Tunajua kuna changamoto nyingi kwenye familia/ndoa. Lakini leo dhumuni la uzi wangu ni----

"Ningejua ningeoa mapema walau nikiwa na miaka 23" Haya ni maneno yaliyoungwa mkono na watu wazima tulipokuwa tunajadili mafanikio ya ndoa kijiweni kwetu. Yalinifikirisha saana.

-Je, nyie wakongwe wa ndoa ni kwa namna gani mnaziona ndoa zenu zimewafanya mkafanikiwa katika maisha tofauti na msingekuwa ndani ya ndoa.

-Ni mara nyingi mnatushauri vijana hata wasio na ajira kuoa kisha mambo yatajiset tukiwa kwenye ndoa, limekaaje hili tunahitaji ufafanuzi.

-Vijana wengi tunaamini tutaoa siku tukifanikiwa kwenye maisha. Msitushangae hili linatokana na aina ya wanawake tulionao siku hizi wataki tutafute wote.

hoja kuu "Ni kwa namna gani ndoa itakuwa chachu ya mafanikio kwa vijana wanao anza maisha"

Lengo la uzi limejificha kutokana na aina ya uandishi wangu ila kwa watu wazima watapata hoja yangu.
 
Ndoa ni kuwa marafiki mlio shibana... ...kuheshimiana...kusameheana..... Na kuvumiliana sana.....hivyo vitu kwa upande wangu ndo vinaleta na kudumisha upendo.
 
Nisaidie kuwaambia hawa wadogo zako mtoa mada anachokihitaji.

Labda unamwandiko mzuri unaoeleweka.

espy
Hahahaaaa!! Umenichekesha sana. Sidhani kama watakuwa wamesoma hadi mwisho.

Mi si nilikwambia acha uoga oa ukawa unambwela mbwela. Unaona sasa unatamani ungenisikiliza mapema😜

Enjoy mdogo wangu, ndoa ni baraka, baraka nyingi zizidi kuambatana nawe.
 
Tunapozungumzia mafanikio ni neno pana kidogo kwa maana kuna kufanikiwa kwa namna tofaut tofauti

Kiuchumi
Inawezekena mara baada ya kuoa huyu mtu wakaongeza nguvu kutokana na vipato vyao kwa maana kama kila mmoja wao alikua anapokea tsh 1 wakiwa wawil kutakua na tsh 2 so nguvu ya kufanya vitu vikubwa zaid ikaongezeka,

Pia inawezekana kwenye biashara unapokuwa na mwenza wako inawezekana ukapata msimaz mzur wa miradi yako au bishara so kutokana na hilo ki uchumi mnakuwa mnanufaika kwa namna moja au nyengine

Kijamii
Hulka yetiu watu wengi mtu anaeheshimika na yule ambae yuko kwenye ndoa tukiamn kwamba ana uwezo wa kutoa maamuzi ya busara zaid kuliko ambae hayupo so ile heshima yako kwa jamii husika kwa kipind hiko inaweza kuongezeka na kuonekana kkama ni moja ya watu ambao mnaweza kufatwa kwa ajili ya ushauri wa namna mbali mbali kutokana na mienendo yenu kwa wakati huo

Kiimani
Wanaume weng wetu maswala ya kiimani kidogo yako kando linapokuja swala la makanisani na misikitini ila kupitia ndoa unaweza ukabadilishwa mienendo yako ya kiimani kama ulikua sio mtu wa ibada ukaanz kuwa mtu wa ibada na kushiriki maswala ya Mungu kwa ukarbu zaid.

So ki uhalisia kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kupimwa kama chachu ya mafanikio ya vijana weng kutokana na kuingia kwenye hii dunia ya ndoa ila pia its not necessary ikawa kipimo cha moja kwa moja kwa mana kuna watu hawajafanikiwa na ndoa zao na wengne wamefanikiwa kwa kutokuwa kwenye ndoa.

Embu nipe maksi zangu kwanza.
 
You won't get everything on a single plate, marriage doesn't give you everything you need, you ought to give your all to achieve what you need.

However, everyone has his own ways of acknowledging a successful marriage. I would think creating a bond with my family (wife and kids) makes it a successful marriage, while you'd think success in terms of material things you gain.

Kupata mtu mtakayeenda nae juu na kurudi wote chini, mkaanza wote chini na kupanda juu pamoja ni changamoto kubwa, lakini success ya ndoa ina vigezo vingi mno.
 
Ni kweli lakini wengi wanawake wameishi kuridhika na zakuhongwa na kuharibu mimba huku wakijidanganya eti Raha jipe mwenyewe ndo unakuta apetite ya ndoa[emoji10][emoji10]
 
Hoja yangu kubwa ipo hapo nilipobold.

Chukulia hali ya huyu jamaa Nina miaka 28 lakini similiki kitu chochote (Asset) tofauti na liability ambayo ni smart phone yangu tu. Hata mke sina - JamiiForums

-Atafanikiwa vipi na ndoa yake kiuchumi kama mlivyokuwa mnashauri tuache woga tuoe mambo yatajiseti mbele ya safari.

-Ninalojua unapopata majukumu ya ziada uchakarikaji nao unaongezeka. Lakini nadhani zaidi ukiwa na hali hiyo unaweza kuathirika kisaikolojia badala ya kuishia kufanikiwa ukapoteza zaidi.

Cc Edzone

-ulivyooa ulikuwa na hali kama ya jamaa?
 
Hoja zako ni fikirishi mkuu, ni ngumu sana kutengeneza mjadala mkubwa. Japo tunahitaji sana mada za hivi ili tusiogope maisha.
 
You won't get everything on a single plate, marriage doesn't give you everything you need, you ought to give your all to achieve what you need.

However, everyone has his own ways of acknowledging a successful marriage. I would think creating a bond with my family (wife and kids) makes it a successful marriage, while you'd think success in terms of material things you gain.

Kupata mtu mtakayeenda nae juu na kurudi wote chini, mkaanza wote chini na kupanda juu pamoja ni changamoto kubwa, lakini success ya ndoa ina vigezo vingi mno.
Nina miaka 28 lakini similiki kitu chochote (Asset) tofauti na liability ambayo ni smart phone yangu tu. Hata mke sina - JamiiForums

"Financial and material benefits"

Is it possible for this young man to make it in marriage. ???

-Labda wazee mnasahau mlivyopita pita hadi mkaoa na mkafanikiwa kwenye maisha.

I wouldn't advise such man to get married before he settles.
 
Ni kweli lakini wengi wanawake wameishi kuridhika na zakuhongwa na kuharibu mimba huku wakijidanganya eti Raha jipe mwenyewe ndo unakuta apetite ya ndoa[emoji10][emoji10]
Je, na tunapooa huwa tunaangali tunaenda kufaidika vipi na huyo mwanamke au tupo obsessed na mapenzi tu?
 
Back
Top Bottom