FAJES
JF-Expert Member
- Oct 29, 2017
- 720
- 644
Juzi nikasema nimpigie rafiki yangu mmoja ambaye sijazungumza naye kwa miezi kadhaa sasa. Mingoni mwa mazungumzo yetu ilikuwa kama ifuatavyo:
Mimi: Mambo vipi kaka, habari za siku?
Yeye: Salama kaka, vipi unaendeleaje na mishemishe huko ya maisha?
Mimi: Salama tu kaka, Mungu anajalia uzima, vipi shughuli yako ya ufugaji wa kuku unaendeleaje?
Yeye: Ahh, kaka sina hamu kabisa!
Mimi: Vipi kulikoni?
Yeye: Wale kuku wangu 50 wa kienyeji wote walikufa, yaani pamoja na jitihada zote za kuwapa chanjo na kufuata taratibu zote lakini nimeishia kupata hasara. Kuku walikufa mmoja baada ya mwingine wala sikuamini kabisa.
Mimi: Pole sana kaka.
Hiyo ni sehemu ya maongezo yetu hapo juzi. Feedback aliyoitoa imenifanya kufikiri sana juu ya changamoto za ufugaji na kilimo nchini kwetu. Pamoja na watu wengi kufuata taratibu za kitaalamu juu ya ufugaji na kilimo, ni kwa nini sekta ya kilimo imekuwa ikikumbwa na changamoto nyingi zinazosababisha ufukara badala ya mafanikio? Utasikia kila mtu anakuelezea changamoto hizohizo za hasara kila mahali. Je, katika watu 10 wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji, ni wangapi hufanikiwa? Jitihada zipi tunachukuwa kutatua changamoto hizi maana kilimo ni sekta inayotegemewa na asilimia kubwa ya watu nchini?
Miaka kama minne iliyopita, nilisema nilime mahindi ya kumwagilia, hasara niliyoipata sitaki kuikumbuka. Mahindi yalishambuliwa na wadudu hatari. Nikasema nilime viazi mbatata, nako nikaambulia kipigo cha mbwa koko. Siyo kwamba nilikuwa sifati taratibu za kitaalamu, nilifuata taratibu ila bado nikapigwa na kupotezwa. Ikabidi niwe mpole.
Hapo tunaongelea changamoto za mashambani. Bado zile za masokoni ndio usiseme kabisa. Ni lini mkulima atakuwa na nafuu ya maisha kutokana na kilimo? Pamoja na wataalamu wengi tulionao, ni kwa nini bado kilimo kimekuwa ni tatizo hasa kwa watu wa hali ya chini?
Naomba kujua kama kuna mtu ambaye katika miaka mitano mfululizo, amefanikiwa kupata faida kuanzia shambani hadi sokoni bila ya kukumbana na hizi changamoto? Je, wapo watu hawa? Ni asiliamia ngapi katika wote wanaojihusisha na kilimo?
Naomba kuishia hapa. Nasikia uchungu moyoni!