wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,432
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA kwa kuziweka kando shughuli zetu na tunashukuru kwa kujumuika pamoja kwenye shughuli za kuabudu ikiwa ni ishara ya shukran kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kuacha shughuli zako KUPUMZIKA.
Musa ndie Nabii alieteuliwa kwenda kuzichukua amri 10 za Mungu ikiwmo kuitakasa siku ya sabato, Musa alikuwa na ukaribu mkubwa sana na Mungu kiasi cha kujua iwe siku ipi, hata Yesu aliitambua na kuitetea na mpaka sasa ipo hivyo ukienda Israel, Wengi watajiuliza ni kwanini hakuna neno Jumamosi au Ijumaa jibu ni kwamba mfumo na majina ya siku tunayotumia sasa havikuwepo enzi hizo, kulikuwa na mfumo wa siku saba kisha inaanza siku ya kwanza, Kwa mfumo na majina ya siku tunaotumia sasa siku hio ina masaa 25, inaanzia ijumaa dakika chache kabla ya jua kuzama hadi kesho yake lisaa baada ya jua kuzama, Pia kabla ya ukristo dini iliyokuwepo ni Judaism ambayo Musa na Yesu walikuwa waumini na ipo mpaka sasa Israel na siku ya sabato kwa maelfu ya miaka ni hio hio, Yesu alikosoa Sheria zilizoongezwa na mafarisayo siku ya sabato lakini aliitambua siku ya sabato.
Hata Yesu aliikuta siku ya Sabato, aliiabudu, aliisifia na kuitetea (Marko 2) na alitamka hajaja kubadili amri yoyote (Mathayo 5:17), miaka nenda rudi hadi sasa ukienda Israel wanaendeleza huu utaratibu, siku ya jumamosi maduka hufungwa na shughuli nyinginezo husimama.
Yesu ni Pumziko letu kiroho hata tunapofanya kazi nzito tukiwa hoi taaban lakini siku ya sabato tunaweka kando shughuli hizo tunapumzisha na miili

Sabato ni zawadi aliyotupa Mungu kuturusu kupumzika kama yeye alivyopumzika siku ya saba katika uumbaji, Sabato isigeuke utumwa au mzigo wa kufuata sheria za wanadamu wengine kama za mafarisayo walizoanzisha mfano kukataza kuvunja masuke siku ya sabato, sheria za kunawa mikono, n.k. ndio maana Yesu akawaambia "Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato." Ni ishara tosha kwamba Yesu aliitambua na kunena kwamba yeye ni Bwana wa sabato.
Akamalizia kwa kusema "Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia." Mwana wa Adamu ni neno limetumika zaidi ya mara 80 agano jipya pekee likimaanisha Yesu, hivyo kuiheshimu sabato ni kumtukuza Yesu.
Pia bila kusahau, Yesu alishaweka wazi hajaja kuzibadili amri 10.