Na cha Kushangaza zaidi kama Burundi inabebwa kwakuwa iliathirika na 1994 Genocide kwa Ripoti za UN zinasema kwamba Rwanda ndiyo iliathirika sana tu ila yenyewe wala haijikombi wala haijipendekezi kwa Mataifa makubwa ya Ukanda wake.
Naifananisha Burundi na Mtoto Mvivu na Mpumbavu pia anayependa Kudeka, Kuongozwa na asiyejitambua ila naifananisha Rwanda na Mtoto Yatima ila aliyejaaliwa Akili, Ushujaa, Mchapakazi, anayejiamini na asiyependwa Kupandwa Kichwani na Wapuuzi ( wanaojiita Wakongwe )
Mwanamume Afrika ni Paul Kagame tu.
#GENTAMYCINE!
Saa ingine huwa unaandika habari za mihemko kuliko uhalisia.
Kwanza sioni rasmi sababu ya wewe kusema Burundi inajikomba kwa Tanzania.
Wewe huyajui kwa undani mambo nyeti ya kiserikali hususan kiuchumi na kiusalama.
Huwezi jua burumdi kama land locked country,hujui inapitia changamoto gani kiuchumi na hivyo kuhitaji mazingira bora ya kuitumia bandari yetu na pia kushirikiana nasi kwenye ujenzi wa SGR ya msongati.
Pia kiusalama Tanzania na Burundi tuna pakana kwa karibu na kwa eneo kubwa la nchi kavu na tumekuwa na changamoto ya usalama.
Na tumemsikia Rais wa Burundi akitamka hadharani kwamba kuna kiongozi wa waasi Burundi anaisumbua serikali yake kwa sasa akishirikiana na waasi wa ADF.
Sasa wewe unawezaje kujua kama hiyo si agenda mojawapo iliyo mlazimu kuja nchini,huenda wao wana tetesi za waasi hao kuitumia ardhi yetu kinyemela kwa mafunzo yao na kuingia Burundi kufanya vurugu na kurudi.
Sio kila wanalolijadili faragha hawa marais iwekwe hadharani. Mengine huwa ni nyeti za kiusalama zaidi.
Wewe unamsifu Kagame yule msigina Demokrasia ambaye anawaua na kuwafunga wote wanaojaribu kumkosoa mpaka wanamuziki!
Huyu Kagame ambae anatajirika kwa kuiba raslimali za CONGO DRC Anazozichimba kimabavu akiwatumia kina Lauwrer Nkunda!
Huyu anaemtesa Victoir Ingabire!
Hebu nenda Rwanda uingie kigali na uingie mitaani kuanzia Lemela,Kimironko,Nyamirambo,Kichukiro na katikati Nyabugogo uingie na uongee na raia wa kawaida wakwambie (kama utawaondoa hofu ya Kagame).
Halafu ujuwe kinachoendelea!
Acha chuki zako kisa rais wa Burundi kuisifia serikali unayoichukia wewe.
Shame on you.
Pichani chini ndie mtu hatari kwa serikali ya Burundi.
Jina lake ni Alex's Sinduhije.anaishi uhamishoni ubelgiji kwa sasa
View attachment 1984011