Ni kwanini game ya Yanga imeahirishwa lakini ya Simba haikuahirishwa?

Ila bongo mpira bado sana.
MFano epl kule man city anacheza leo ligi, after 3 days ana uefa na huoni akilalamika wala mechi kuw postponed.
Vitu vingine sijui mnawaza kwa kutumia nini. Wewe unaona mazingira ya ulaya ni sawa na Africa? Ulaya kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine ni masaa tu iwe kwa ndege ya abiria au kwa treni au hata kwa basi na kwa ukwasi walio nao timu za ulaya kutumia ndege ya kukodi ni rahisi tu tofauti na afrika miundombinu na logistics za usafiri si rafiki fikiria kwa mfano simba akisema asafiri kwenda Angola tu hapo kwa ndege ya abiria atalazimika kweda nairobi, addis ababa then ndo watue Angola au Congo tu hapo jirani kwa ndege ni lazima uende mpaka Ethiopia kwanza au kwenda Morocco wanalazimika kwenda mpaka dubai au spain (nje kabisa ya Africa) ndo waingie morocco hii ni kwasababu hakuna route ya moja kwa moja kwa baadhi ya nchi.
Hiyo ni mifano tu kwa uchache
 
Maandishi mengi lakini hayana mantiki,inachukua siku ngapi Yanga kwenda uwanja wa KMC kucheza na Fountain Gate? au hujui kuwa Yanga wapo nyumbani?
 
Simba ina Kikosi Kipana! NI Kipana kiuHALISIA sio Kipana Jina Kama wale wa madimbwini!
 
Point ni ile ile bongo bado sana means ( UKI combine yoote uliyoyaongea).
 
Mechi za shirikisho hata Tabora utd anaweza kucheza kesho asubuhi! Ndiyo maana huko kuna vitimu vya ajabu ajabu sijui Bravos sijui supersport 😀😀😀
 
Utopolo game dhidi ya FG alikua home pale KMC na Game dhidi ya AL Hilal yupo home pale kwa Mkapa

Haitaji kusafiri kwenda nje ya nchi kama maelezo yako marefu yanavyosema, game zote alikua Home
 
Huu upuuzi kauleteza yanga mwenyewe baada ya kuruhusu makolo waongoze ligi.
 
Simba iliposajili kabla ya kupata Kocha uto walichonga Sana SASA huyu Mjerumani vipi mbona karithi wachezaji ambao hawajui? Cha ajabu timu imejaa wastaafu Hadi wanalala uwanjani😂😂
 
Usilinganishe champions league na kombe la loosers! Hapo ni sawa na kulinganisha mbingu na ardhi! Unafikri Simba mechi ya ingekuwa na Azam wangeiomba? Thubutuuu!!
 
Utopolo game dhidi ya FG alikua home pale KMC na Game dhidi ya AL Hilal yupo home pale kwa Mkapa

Haitaji kusafiri kwenda nje ya nchi kama maelezo yako marefu yanavyosema, game zote alikua Home
Unafikri game za champions league zinaangaliwa kwa urahisi wa kufika uwanjani? Tunaangalia na afya za wachezaji.
 
Mimi ni shabiki lialia wa Simba, huu ushabiki umevuka kiwango. Kutuhumu wachezaji wa timu pinzani eti wanatumia dawa za kusisimua misuli sio sahihi. Na kama ni kweli, basi tatizo lipo TFF na CAF! Tuache ushabiki wa kishamba!
Mwanayanga mwenzangu umehamia Simba lini tena?
 
Mechi za team zote mbili ziliahirishwa isipokuwa simba wenyewe baade ndo waliomba wacheze mechi yao na pamba kama ilivyokuwa kwenye ratiba ya awali.
Nashangaa mleta swali hili, eti alikuwa hajui kuwa hata mchezo wa Simba na pamba, nao uliahirishwa, na ni Simba wao ndiyo walioomba huo mchezo uwepo!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Yanga anasafiri kwenda wapi na mechi inachezwa hapa hapa dar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…