Ni kwanini pamoja na ujio wa Magari mengi na mapya duniani lakini Gari za Mercedes Benz, Rolls Royce, Porsche na Lamborghini zitaheshimika Milele?

Ni kwanini pamoja na ujio wa Magari mengi na mapya duniani lakini Gari za Mercedes Benz, Rolls Royce, Porsche na Lamborghini zitaheshimika Milele?

Mzukulu

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2020
Posts
1,401
Reaction score
2,641
Leo hii sijui Mzukulu nimekumbwa na nini yaani similiki hata Baiskeli au Guta lakini nayazungumzia Magari ambayo sina hata Ubavu wa Kuyamiliki.
1591339257257.png

Lamborghin

1591339351866.png

Mercedes Benz

1591339450413.png

Porsche
1591339536116.png

Rolls Royce
 
Zinaheshimika hata huko Kwenu kwa Kindande? Kwetu Kerege, IST inapewa heshima kuzidi hizo Benz
 
mabeberu wanatuaminisha ujinga Sana ujue tuna gari zetu zinaitwa nyumbu Kama sijakosea nigari safi tuuh
Hahahah gari ni ile ile tu alimradi ikiwa na parts zote zinazohitajika. Kinachoongezeka ni cosmetics na new technologies ila msingi uko pale pale. Tukiweza kuboresha "Nyumbu" zikawa levels sawa na gari za mjapani mbona ni freshi tu.
 
Technology inayotumika kuyaunda haifanani na Japanese cars..
Its not about technology maana car architecture inahusisha components zile zile tu. Chassis, body, matairi, breki, suspensions, axle, gearbox, engine,usukani,gia, viti, infotainment sys,ac, taa n.k! Vyote unavipata katika gari zote iwe Germany au Mjapani.

Sema tu tofauti inakuwa ni additional safety features & cosmetics (e-controlled system za suspension,driving assist,combustion,braking kama abs,stability,lighting n.k) ambazo mjapani hajaziweka kwenye gari zake za bei rahisi. Ila ukiangalia gari za aghali ndio unazipata kama kawaida tu kama ilivyo kwa Benz japo engineering iko tofauti.

Kitu kinachotofautisha Benz ni branding & positioning tu. Jamaa wamejiposition kama Executive & super luxury vehicle manufacturers na wamekiplant hiko kitu kwenye akili ya wateja wao. Mercedes is all expensive because of that. Mercedes ime target specific type of customers mara nyingi ni CEO's na Executive personnels kama ma raisi.

Ila sio kama hamna gari zuri zaidi ya Merc toka makampuni mengine..nakataa!
 
Zamani Mercedes Benz zilikuwa zinatengenezwa kila baada ya miaka kumi ndio toleo jipya linatoka
Japan akawa anamzidi ujanja kwa kutoa model za aina nyingi kwa mfano Toyota za kila aina na bei tofauti
Mwisho nae MB akaona ajiongeze na kuanza kufyatua za aina nyingi kila mwaka
Lakini bado chuma cha mjerumani kinaongoza kwa uimara
Na hizo zingine ni mbwembwe tu na wanunuzi ni wachache na bei ni juu zaidi ila Benz siku hizi kila mtu anaweza kumiliki sio kama zamani
 
Kwanini Japanese cars ndio Zina soko kubwa afrika mashariki ukilinganisha na magari hayo
1. Kasumba ya watu kukariri kwamba toyota is everything.

2. Toyota walipata tenda kubwa serikali za E.A kusupply magari yao. Ndo ikasambaa mpaka kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom