Ni kwanini serikali imewachagulia wanafunzi wa sayansi kusoma art 'A' level ilihali wanapenda sayansi!?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Ndugu wanabodi nimekutana na huu mkanganyiko hasa kwa wahitimu wa jinsia ya kiume, ambao katika uchaguzi wao wa masomo walichagua kusoma sayansi, isitoshe wamepata credit zinazokidhi kuendelea na masomo ya sayansi.
Kwa mshtuko na mshangao wengi wao wamechaguliwa wakasome masomo ya art Kwa ngazi ya A level.

Kwa mtazamo wangu naona ni kama serikali imeamua kuua ndoto za maelfu ya vijana Kwa makusudi Kwa kuwalazimisha kusoma vitu ambavyo hawakuchagua kuvisoma.
 
Mfumo wetu wa elimu ni mbovu kupindukia. Haiwezekani mtu achaguliwe cha kusoma hata ambacho asingependa.

Mfano eti chuo una apply TCU ndio wakupangie ukasome nini na chuo gani.

Ifikie mahali hiyo TCU iwe tu inasimamia vyuo na sio kupangia watu programme na vyuo vyakusoma. Mtu achague chuo na degree anayotaka mwenyewe.
 
Wamewasaidia. Mziki wa sayansi A level sio wa kitoto.
Ukienda na makalai yako kufeli six nje nje
 
Ndugu wanabodi nimekutana na huu mkanganyiko hasa kwa wahitimu wa jinsia ya kiume, ambao katika uchaguzi wao wa masomo walichagua kusoma sayansi, isitoshe wamepata credit zinazokidhi kuendelea na masomo ya sayansi.
Kwa mshtuko na mshangao wengi wao wamechaguliwa wakasome masomo ya art Kwa ngazi ya A level.

Kwa mtazamo wangu naona ni kama serikali imeamua kuua ndoto za maelfu ya vijana Kwa makusudi Kwa kuwalazimisha kusoma vitu ambavyo hawakuchagua kuvisoma.

Ingekuwa vyema ungeleta ushahidi wa hicho unachokisema kwamba yupo aliyeomba kusoma maybe pcm/pcb/cbg/pgm kwenye machaguo yake na hakuomba hkl ama hgl lakini akapangiwa hkl ambayo haikuwa chaguo lake!!!
Ipo tendency unakuta mwanafunzi alichagua hkl kama chaguo la tatu ama la mwisho kisha anapelekwa hiyo hkl, halafu anakuja kulia eti hkl haikuwa chaguo lake, na watu kama wewe mleta uzi mnaanza kukurupuka kwamba kapelekwa chaguo lisilokuwa la kwake!
Uzuri mmoja kwa sasa bila shaka mfumo unaruhusu mwanafunzi kufanya machaguo baada ya matokeo!!
Hivyo ili kujiridhisha unachosema hakina magumashi, naomba uanike ushahidi humu kwa kuonyesha machaguo ya hao unaowasemea walichoomba kusoma kabla na walichopangiwa!
 
Kwa sababu walikua wamefweli, ila ni Serikali hiyohiyo Kwa sababu za Siasa, ikawaongezea ufaulu waonekane wamefaulu sana kumbe hamna kitu
 
Mfumo wetu wa elimu ni mbovu kupindukia. Haiwezekani mtu achaguliwe cha kusoma hata ambacho asingependa.

Mfano eti chuo una apply TCU ndio wakupangie ukasome nini na chuo gani.

Ifikie mahali hiyo TCU iwe tu inasimamia vyuo na sio kupangia watu programme na vyuo vyakusoma. Mtu achague chuo na degree anayotaka mwenyewe.

Tcu walimfanyia hivyo nani?
Kuna kijana mmoja alichaguliwa chuo kimoja kusomea fani flani, sasa ile fani ni kama aliichagua kwa majaribio ama kwa kutokujua!
Alipoulizwa akajibu kuwa hakuichagua, tukamwambia atuonyeshe profile na machaguo, baada ya kumbana akakubali, tukaangalia machaguo ile fani aliyochaguliwa tukakuta ilikuwa ya tatu kwenye machaguzi, lakini mwanzo kuna watu waliamini kapangiwa kitu ambacho hakukichagua!!
So na wewe kama unasema TCU inapangia watu machaguo yasiyo ya kwao, unaweza kuleta ushahidi hapa ili kama upo ufafanuzi utolewe!
 
Ingekuwa vyema ungeleta ushahidi wa hicho unachokisema kwamba yupo aliyeomba kusoma maybe pcm/pcb/cbg/pgm kwenye machaguo yake na hakuomba hkl ama hgl lakini akapangiwa hkl ambayo haikuwa chaguo lake!!!
Ipo tendency unakuta mwanafunzi alichagua hkl kama chaguo la tatu ama la mwisho kisha anapelekwa hiyo hkl, halafu anakuja kulia eti hkl haikuwa chaguo lake, na watu kama wewe mleta uzi mnaanza kukurupuka kwamba kapelekwa chaguo lisilokuwa la kwake!
Uzuri mmoja kwa sasa bila shaka mfumo unaruhusu mwanafunzi kufanya machaguo baada ya matokeo!!
Hivyo ili kujiridhisha unachosema hakina magumashi, naomba uanike ushahidi humu kwa kuonyesha machaguo ya hao unaowasemea walichoomba kusoma kabla na walichopangiwa!
Sijajua uanapotaka nilite ushahidi unataka nilete nini. Maana ninachokisema Nina kifahamu mimi ni muhanga nina nina vijana wangu watatu ambao hawakuwahi kuchagua art kabisa lakni wamepangiwa wakasome art mimi nimewakatalia ni heri wakasome certificate ya taaluma kuliko kutekeleza huu uharamia
 
Tatizo ni Hilo nloliandika hapo, wasichana wamebebwa ivoivo kisiasa.
Na hapa ndo naona Kuna tatizo kubwa huwezi beba wasichana Kwa gharama ya kuwakandamiza wanaume huku ni kuhujumu maisha ya watu kwa makusudi. Ni heri umchezee mtu kwenye ajira lkni sio kwenye elimu inauma sana yaani.

Mtu kajipinda miaka yote minne anahangaika na ma bombastic ya sayansi alafu from no where umuambie aende art!?
 
Mfumo wetu wa elimu ni mbovu kupindukia. Haiwezekani mtu achaguliwe cha kusoma hata ambacho asingependa.

Mfano eti chuo una apply TCU ndio wakupangie ukasome nini na chuo gani.

Ifikie mahali hiyo TCU iwe tu inasimamia vyuo na sio kupangia watu programme na vyuo vyakusoma. Mtu achague chuo na degree anayotaka mwenyewe.
Upo sahihi sana Hoja yako ni nzito hv ulimwengu wa sasa unamchagulia mtu cha kusoma kweli!??
Hayo ni mambo ya miaka ya sabini huko
 
Mfumo wetu wa elimu ni mbovu kupindukia. Haiwezekani mtu achaguliwe cha kusoma hata ambacho asingependa.

Mfano eti chuo una apply TCU ndio wakupangie ukasome nini na chuo gani.

Ifikie mahali hiyo TCU iwe tu inasimamia vyuo na sio kupangia watu programme na vyuo vyakusoma. Mtu achague chuo na degree anayotaka mwenyewe.
Nakumbuka ummy alipokuwa tamisemi na ndalichako elimu waliwahi kusema hawatawachagulia tena wanafunzi nini cha kusoma nimeshangaa sana kwani waliposema vile walikusudia kufumua huo mfumo au walikusudia wafanye miujiza gani!?
 
Hii ya TCU umeitoa wapi? Mbona wanafunzi wanaomba vyuo na course wanazotaka au ulimaanisha TAMISEMI.
 
Sijajua uanapotaka nilite ushahidi unataka nilete nini. Maana ninachokisema Nina kifahamu mimi ni muhanga nina nina vijana wangu watatu ambao hawakuwahi kuchagua art kabisa lakni wamepangiwa wakasome art mimi nimewakatalia ni heri wakasome certificate ya taaluma kuliko kutekeleza huu uharamia
Anayekubishia achana naye aendelee na Imani yake. Mimi ni shuhuda na mhanga matokeo ya mwaka Jana Mtoto wa Kaka yangu alichagua PCB, PCM na CBG. matokeo ya chini kwenye hizo comb alikuwa na BCC lakini matokeo yake alipelekwa HKLalikokuwa na CBB Sawa kabisa na matokeo yake ya PCM.
 
Afadhali mkuu maana huyu naye sijui wa wapi hili jambo lipo wazi kabisa yeye analeta ubishi wake
 
Nakumbuka ummy alipokuwa tamisemi na ndalichako elimu waliwahi kusema hawatawachagulia tena wanafunzi nini cha kusoma nimeshangaa sana kwani waliposema vile walikusudia kufumua huo mfumo au walikusudia wafanye miujiza gani!?
Tamisemi na uhuru wa mtu kujichagulia vina uhusiano gani?
 
Back
Top Bottom