Ni kwanini serikali imewachagulia wanafunzi wa sayansi kusoma art 'A' level ilihali wanapenda sayansi!?

Wamewasaidia. Mziki wa sayansi A level sio wa kitoto.
Ukienda na makalai yako kufeli six nje nje
Wacha ujinga. Kufeli ni kuamua tu hakuna cha mziki wala dance. Mwache mtu achague anachoona kinamfaa
 
Waje kusoma vyuo vya Afya waachane na form five
 
Mikakati ya Mashoga itakuwa
 
Mkiawmbiwa mchangie ujenzi wa Shule mnakataa mnasema ni kazi ya Serikali. Na Sasa Serikali inasema haina nafasi za kutosha kuweka wanafunzi wote waliofaulu masomo ya kutosha. Unataka Serikali ifanyeje? Iwape wakasome masomo ya art au wasubiri mpaka nafasi zitakspopatikana?
 
Hizi hoja zako zina maudhi sana au wewe ndo mkenda mwenyewe!?
Kila siku serikali inahamasisha watoto wasome sayansi kama walijua miundombinu hawana si wangefuta hiyo kampeni!?

Sijawahi kumsikia hata kiongozi mmoja kuwatia moyo wanafunzi wapende masomo ya art now Kwa nini kuwavunja moyo waliosoma sayans?
 
Elimu ya bure haina maana, alisikika Ney wa Mitego
 
Mimi nimekupa "a point blank" answer. Yaliyobaki juu yako.
 
Wamewasaidia. Mziki wa sayansi A level sio wa kitoto.
Ukienda na makalai yako kufeli six nje nje
Kabisa Mimi Nina mdogo wangu alikuwa anapenda science sana matokeo ya form four alikuwa ana two alilia sana alipopangwa kusoma masomo ya Arts lakini form six alitoka na division one nzuri wakati rafiki zake wote walioenda science walipata four na zero ....Huwa anawashukuru sana Kwa kumpanga masomo ya Arts
 
Hoja ya msingi si kupata one hoja ni mtu kusoma anachokipenda na ndoto ya maisha yake
 
Wengi tuatoto
 
Wacha ujinga. Kufeli ni kuamua tu hakuna cha mziki wala dance. Mwache mtu achague anachoona kinamfaa
Mtu kapata zake ccc PCM au PCB Form four. Alienda six huyo four au kutaga nje nje. Labda serikali iingilie kati iwaonee huruma
 
Sasa kama akienda kusoma science A level akapata zero hizi ndoto zake atazitimizaje
Mtu akipata ccc kama ana hofu ya jufeli huko mbele anatakiwa kutafuta chuo cha ujuzi anaoutaka na sio kumwambia akasome art
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…