Wawekeze kwenye teknolojia, watu siku hizi wanatumia graphics za maana kutengenezea picha kama yale madude ya kijani sijui yanaitwaje.
Halafu waache kurekodia kamera za kiduwanzi, wakaazime hata zinazotumiwa na kina Kiba na Mondi.
Waigizaji na watengeneza muvi waingie darasani kusoma ili walete vitu vya kijanja, vyenye ufikiri mkubwa na sio kila siku mapenzi na komedi. Watupe radha tofauti kama ujasusi, utawala na siasa, wizi kama money heist n.k
Natambua hali zetu kipesa sio nzuri sana lakini muvi kali uwekezaji wa kifedha haukwepeki. Hatutaki kuona mnavunja glasi na sahani, muharibu hata harrier tako la nyani mnalitia kiberitiš
.
Watambue ushirikiano na wengine ni muhimu, wajitahidi kujimix na wanaijeria au waghana waliofanikiwa labda watatuambukiza harufu ya mafanikio katika tasnia ya bongo muvi.