Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?

Mkuu, mbona maelezo yamejitosheleza kbs. Na umeeleza vyema kbs. Kwamba kiongozi wako ajue tatizo na kusort out inapobidi. Lakini kiujumla hii ya kutaka tutangaziane afya zetu nyie mnataka tuanze mambo ya kubaguana sasa. Kwamfano huyu wa kukatwa vidole vya miguuni.. itapakoonekana sasa ni dhahiri afya yake haikidhi abadilishiwe kitengo. Or else ni kutafutiana kubaguana
 
Ila kuna level ya watu fulani lazima mambo yao yawe faragha siyo kuzungmza kila mtu ajue

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Nimeongelea complexity ya kutoa habari za maradhi ya viongozi hapo juu.

Kuna mambo ya national security.

Kwa mfano, vipi kama kutangaza rais anaumwa mahututi kutasababisha power struggle serikalini kwa sababu viongozi waandamizi wa serikali wanajua juu kabisa kuna power vacuum?

Lakini pia, kuna mambo ya accountability na transparency.

Je, serikali iendelee kuficha habari muhimu kuhusu maradhi ya kiongozi? Vipi kama kuficha habari huko kutamsababishia madhara yeye kiongozi na taifa?
 
Hii issue ya Mzena Hospital inazidi ku-trend sana hapa JF bila sababu ya msingi.
Kwani kiongozi akiumwa wewe binafsi unateseka na nini?
Si ndiyo hapo....lazima watu wakubali
Kuwa service anayopata kiongozi maalum mtu wa kawaida hiwezi ipata na hiyo ni kawaida tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 

Hizi ndo chumvi zinazoweza leta chuki Kwa serikali..
Kama ni best hivyo mbona Nyerere alipelekwa London?
 
Mbona watu wakiwa na ngwengwe aka ngoma
Hawajitangazi waanze basi hao wanaosema tujitangaze wajitangaze[emoji23][emoji23][emoji23]

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kama wanapokea bima zetu hizi basi ni ya wote
 
Ukishakuwa kuwa kiongozi na wa level fulani
Lazima maisha yako yawe na faragha kwa kila jambo
Kuhusu maradhi pia ni faragha mpaka kwa mtu wa kawaida home boy kiranga

Ova


Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nani kafa?
 
Hizi ndo chumvi zinazoweza leta chuki Kwa serikali..
Kama ni best hivyo mbona Nyerere alipelekwa London?
Imefanyiwa maboresho makunwa kipindi Cha JK nyerere alifariki 1999 ilikuwa bado haijawezeshwa.
 
Ukishakuwa kuwa kiongozi na wa level fulani
Lazima maisha yako yawe na faragha kwa kila jambo
Kuhusu maradhi pia ni faragha mpaka kwa mtu wa kawaida home boy kiranga

Ova


Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Hapana, you have it backwards.

Unavyozidi kupanda kwenye uongozi ndivyo haki yako ya kuwa na faragha inavyozidi kupungua.

Kuna kanuni za maadili ya uongozi zitataka upeleke list ya mali zako ziangaliwe, hapo huna faragha.Kuna kampeni za kuomba kura zitataka uelezee maisha yako yamekuwaje, hapo huna faragha, kuna waandishi wa habari watakuhoji, hapo huna faragha.

Mimi naweza kukaa maisha yangu yote sijapigwa picha na kuwekwa gazetini. Naweza kuilinda faragha yangu hivyo kwa sababu sina uongozi.

Rais wa nchi akikataa picha yake isiwekwe gazetini kwa sababu anataka kulinda faragha yake watu wataona kituko.

Kwa sababu kazi ya urais inaendana na kutokuwa na faragha, mtu anayependa faragha zake anatakiwa ajue kabla hajagombea urais kwamba, kama anataka faragha, asigombee urais.

Ukishagombea uongozi unakuwa "public property", huna faragha tena.
 


Ni kama unasema JK alikuwa na kifafa??
 
Tukizungumzia maradhi,ugonjwa ni faragha ya mtu home boy
Labda uamue wewe kutangaza na kuna level ya kiongozi mfano ukiumwa huwezi kutangaza tu maana italeta panic kwa raia,kwa hiyo suala la faragha lipo tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ni kama unasema JK alikuwa na kifafa??
I have not examined his medical records, ila alikuwa anaanguka kama mtu mwenye kifafa tangu akiwa waziri.

Kuna siku alianguka uwanja wa ndege Belgium, akiwa waziri, bado kidogo patokee diplomatic issue.

Halafu kaenda kugombe urais bila kuwaambia watu, akaanguka tena Jangwani.

Sasa hapo unaweza kuona umuhimu wa viongozi kuwa wawazi katika afya zao.

Naona alivyostaafu kaji redeem kwa kutangazia ulimwengu ana tezi dume.
 
Aha sasa hapo ni yeye mwenyewe alikuwa hajawahi kufanya chekup ya mwili wake

Ova


Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Sisi tukiugua tunaambiwa twende mwananyamala..hehehehehe
Ujamaa tuliukataa siku nyingi na tukaambiwa soko huria ndiyo mwelekeo. Lakini ikija kwenye mambo mengine tunadai ujamaa ndiyo mwelekeo mzuri. Nadhani kitu muhimu na haki cha kudai ni hospitali zetu za chini na juu ziwe na madakaktari na matibabu yanayolingana na hadhi na ngazi ya hospitali. Lakini hili la kudai wote tutibiwe huko wanakotibiwa sidhani itatokea.

Kwanza, kuna sheria, ngazi, na taratibu za matibabu kwa waajiriwa wa serkali wa serkali kufuatana na ngazi zao. Hili halikuanza leo au kesho. Kwa hiyo siyo kila mgonjwa anaweza kuwekwa daraja la kwanza au la pili. Hiyo ni ndoto ambayo ilithibitishwa kutowezekana (some kitabu kiitwacho: Animal Farm kilichoandikwa na George Orwell).

Najua kila siku tunalalamika kutafuta usawa. Malalamiko mengine yana haki, kwa sababu yale tunayoyalalamikia yanadumaza maendeleo. Kwa mfano, malalamiko juu ya watu wengi hasa viongozi kutibiwa nje, kulileteleza kudumaza huduma za afya za hospitali zetu maana pesa ya kuwapeleka viongozi kutibiwa India na nje kwingineko ingeweza kutumika kuborosha hospitali etu na kuziwezesha kutoa matibabu yanayofuatwa nje. Ukweli ni kwa katika kipindi cha miaka mitano, tumeweza kuziboresha hospitali zetu na kutoa huduma nyingi zilizokuwa zinafuatwa nje.

Sasa hili la viongozi kutibiwa hospitali ya hapa ndani sioni tatizo lake. Hao wanatibiwa huko kwa sababu inaruhusiwa na hii ni hospitali ya kwetu. Sku zote tunatetea kuendeleza sekta binafsi, sasa serkali ikipeleka pesa sekta binafsi kuna tatizo gani. Au ndiyo yale ya kulaumu na kufananisha kila kitu. Lakini tunapojaribu hiyo bado kuna matatizo. Najua walalamikaji siku zote wanalinganisha kila kitu na Ulaya. Demokrasia Ulaya. Haki za binadamu Ulaya. Uchaguzi Ulaya. Uhuru Ulaya. Lakini ikija huduma za jamii, tunataka Ujamaa na siyo Ulaya! Hivi mnajuwa kuna Wamarekani zaidi ya millioni 20 ambao hawana huduma za afya kwa sababu ni maskini na hawana bima ya afya! Hizo zote ni changamoto za dunia na TZ pia zipo changamoto. Hatuwezi kulaumu viongozi kwa kudhani serkali itatoa kila kitu. Serkali itatoa kulinganisha na pato lake na kwa kugawa hilo pato kwa wizara ili kutoa huduma, na huduma ni nyingi mno.
 
Nimeandika yote hayo hapo juu, kirefu.

Kimsingi.

1. Magonjwa ni faragha ya mtu binafsi, tunakubaliana.
2. Ukiingia kwenye uongozi, unajivua haki nyingi za faragha ya mtu binafsi
3. Watu wana haki ya kujua afya za viongozi, kwa sababu afya ya kiongozi si suala la kiongozi binafsi, ni suala la usalama wa taifa
4. Kuna nuance za ku balance security concerns na transparency concerns kwenye kutangaza afya za viongozi kiasi kwamba usitengeneze panic/ power struggle on the one hand, na usiwanyime wananchi habari muhimu on the other hand.

Ila, overall, the overriding factor hapa ni kwamba, wananchi wana haki ya kujua afya za viongozi wao kama vile muajiri anavyokuwa na haki ya kujua afya ya muajiriwa wake.

Kimsingi viongozi ni waajiriwa wa wananchi, sasa, hakuna mantiki muajiriwa kukataa kueleza hali ya afya yake kwa muajiri, kwa sababu hata ufanisi wa utendaji wake unategemea hali ya afya. Muajiri ana haki ya kujua hali ya afya ya muajiriwa ili ajue kama muajiriwa anahitaji msaada au ataweza kumudu kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…