Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?

Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?

Sasa kwanini tu kwakuwa mmeamua Kutuficha Watanzania kuhusu Kulazwa Kwao hapo Mzena Hospital basi hata Wakifa ( Wakifariki ) msiendelee pia Kutuficha kwa Kutotujajia hiyo Hospitali na badala yake muendelee tu na Ratiba zenu za Maziko nyie nyie kama nyie pamoja na Wauguzi wa Mzena Hospital na wale Walinzi Wanoko wenye Maswali ya Kukomoa pale Getini Makumbusho? Tumeivumilia hii tabia tumechoka na badilikeni!
Hiyo Hosptal nadhani kuna mapungufu ya maarifa ni vyema ubakie kuitwa zahanati tu kuliko kupewa sifa za Hosptal hi hali wengi hukariki hata kwa magonjwa ambayo siyo Hatari kama alivyofariki mkapa kwa njia ya kutatanisha
 
Kiongozi si mtu binafsi, ni mtu aliyejivua haki zake za mtu binafsi na kuamua kuwa "public figure".

Angetaka kuwa na faragha ya "mtu binafsi", asingegombea uongozi tungetetea haki zake za faragha.

Waingereza wanasema "You can't eat your cake and have it too".

Yani watu wana uchaguzi wa kuamua, ama wanataka maisha ya faragha, bila ya kuwa viongozi, au wanataka maisha ya uongozi, yasiyo na faragha.

Haitakiwi mtu agombee uongozi na kutoa maisha yake yawe ya huduma kwa wananchi, huduma ambayo inategemea afya yake kuwa nzuri, halafu akipata matatizo ya kiafya atake kufanya faragha afiche.

That is like eating your cake and expecting it to be there. Kama unataka maisha ya faragha, usigombee uongozi.

Ndiyo maana Rais Mstaafu Kikwete alipopata matatizo ya tezi dume aliutangazia ulimwengu. Bila aibu. Namuheshimu sana Kikwete kwa hilo, ingawa kuna matatizo yake mengine ya kuangukaanguka tangu zamani hakuyasema wazi, kwa sababu za kisiasa.

Kama kawaida, viongozi wetu wanajifunza mambo baada ya kutoka madarakani.

Sasa wewe ungependa mtu mwenye kifafa kwa mfano, anayeangukanguka kila mara, agombee urais bila ya kuwaambia watu kwamba ana kifafa na muda wowote anaweza kuanguka jukwaani? Utaona mtu ana haki ya kugombea urais bila kuwataarifu wananchi kwamba ana kifafa? Kwa sababu ni suala la binafsi?

Unapokuwa kiongozi wa nchi, suala la afya binafsi ni suala la usalama wa taifa.

Nyerere aliwahi kusema hili, rais akikohoa tu watu wanaulizana, kile kikohozi cha kawaida au ana kifua kikuu yule?
Yes, a presidency is a public position and one who occupies is a public figure. But there is no law that requires a president to reveal her/his sickness to the public. Since it is not required by law, if one does not report well and good but if one reports it even better.
 
Viongozi na viongozi wakubwa wakiumwa hutibiwa hapo mbona kitambo sana tu
Nashangaa sahv watu wanaona big deal
"Ila watu wajitahidi wawe na connection na kujuana na watu fulani mambo kama haya huwezi kukosa jua"

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Karibu mtataka Viongozi wote wapande daladala kwenda kazini Akili za hovyo kabisa. Wewe unatambua heshima kubwa na hadhi za Viongozi pamoja na heshima hizo na wenyewe ni binadamu wanamadhaifu yao inamaana wanahitajika Watu wenye taaluma ya Siri nje ya taaluma ya Udaktari .Hivyo basi tegemea siku zote Viongozi kutibiwa mahali pa Hivyo .Kumbuka kuwa hapo Muhimbili au. Mwananyamala akija kiongozi akifika mpaka baadhi ya huduma huwa zinasimama kwa muda kwa sababu za kiusalama Sasa Leo unataka tulazwe naye Mwananyamala huo ni upeo finyu wa kufikiri.Yaani hata kiongozi akijisikia mafua akaenda zahanati nchi nzima itajua kuwa kiongozi anayo mafua.Hivyo taarifa za matibabu kwa Viongozi kuwa siri kwa Viongozi ni muhimu Sana kuondoa taharuki na hofu kwa wafuasi wao itatolewa tu pale itakapokuwa lazima. Pia nakukumbusha kuwa siyo kila sehemu za Siri ni bora Sana bali Kinachofuatwa ni Usiri tu.
 
nafikiri kwa suala la usalama wa viongozi kulingana na majukumu yao ya kazi, kivipi? mfano kiongozi ametatua mgogoro wa mtu maskini na tajiri, na tajiri akawa ameshindwa kesi lakini hajafurahisha na adui yake hapo namba moja ni huyo kiongozi msuluhishaji...sasa tajiri anao uwezo wa kumdhuru kiongozi kwa njia tofauti, hivyo usalama elekezi ni muhimu kwa viongozi hasa wa afya zao.

Nachakata tu...
Tajiri hupenya popote kwa kutumia pesa zake hata huko akitaka kufika anapenyeza rupia wanafanya atakavyo,‘mwenye pesa hashindwi kwa lolote
 
Hiyo Hosptal nadhani kuna mapungufu ya maarifa ni vyema ubakie kuitwa zahanati tu kuliko kupewa sifa za Hosptal hi hali wengi hukariki hata kwa magonjwa ambayo siyo Hatari kama alivyofariki mkapa kwa njia ya kutatanisha
Wewe! Kwa hiyo unataka niambia Mzena haina hadhi ya Hospitali bali kituo cha afya na majengo yote yale
 
Yes, a presidency is a public position and one who occupies is a public figure. But there is no law that requires a president to reveal her/his sickness to the public. Since it is not required by law, if one does not report well and good but if one reports it even better.
The Social Contract of leadership is not limited to law. It extends to matters of leadership ethics.

For example, the president, as the last custodian of the land, has the last say in distributing vast tracts of land to whomever he desires. The law gives him that authority.

But, does that mean it is OK for him to give all the national parks to his uncle? Even if legally he is allowed to do so?

Just because there is no law against that, does that mean he should do that?
 
Embu taja idadi ya visiki waliotibiwa hapo ili tuone kama tumefichwa!
 
Kama makao makuu ya mehamia Chamwino, naona watakua mbioni kujenga tawi la Mzena Dom, naomba hii waiite Mapank. Mfugale sasa ana mbili. 😛 😛 😛
 
Back
Top Bottom