Sasa kwanini tu kwakuwa mmeamua Kutuficha Watanzania kuhusu Kulazwa Kwao hapo Mzena Hospital basi hata Wakifa ( Wakifariki ) msiendelee pia Kutuficha kwa Kutotujajia hiyo Hospitali na badala yake muendelee tu na Ratiba zenu za Maziko nyie nyie kama nyie pamoja na Wauguzi wa Mzena Hospital na wale Walinzi Wanoko wenye Maswali ya Kukomoa pale Getini Makumbusho? Tumeivumilia hii tabia tumechoka na badilikeni!
Suala la kuelezea ugonjwa, hususan wa viongozi, lina utata sana.
1. Suala la ugonjwa ni suala la faragha. Nje ya madaktari na familia ya karibu, mtu ana uhuru asiweke habari za ugonjwa wake hadharani. Nchi zilizoendelea kuna sheria maalum zimetungwa kuhakikisha faragha ya mgonjwa inatunzwa.
Mfano ninm shwria ya HIPAA ya Marekani.
Health Insurance Portability and Accountability Act of 1996.
Lakini pia
2. Mtu anapochagua kuwa kiongozi, anachagua kuacha kuishi maisha ya mwananchi wa kawaida na kuyatoa maisha yake yawe ya kuwahudumia wananchi. Kwa hivyo kuna dhana kwamba, kama moja ya nguzo za uongozi kimaadili ni uwazi, viongozi wanawajibika kuwataarifu wananchi pindi wanapopata matatizo ya kiafya. Ni haki ya wananchi kupata taarifa hizi.
Lakini pia.
3. Taarifa hizi, hususan kwa viongozi wa juu kabisa kitaifa, zikitolewa bila tahadhari, zinaweza kuleta matatizo mengine ya kiusalama katika jamii.
Ila, mwisho wa yote.
4. Waswahili walisema, mficha maradhi, mauti humfichua.