Ni kwanini Viongozi Serikalini wakilazwa Mzena Hospital huwa tunafichwa, ila wakifa tu tunaambiwa Walilazwa hapo Mzena Hospital?

Suala la kuelezea ugonjwa, hususan wa viongozi, lina utata sana.

1. Suala la ugonjwa ni suala la faragha. Nje ya madaktari na familia ya karibu, mtu ana uhuru asiweke habari za ugonjwa wake hadharani. Nchi zilizoendelea kuna sheria maalum zimetungwa kuhakikisha faragha ya mgonjwa inatunzwa.

Mfano ninm shwria ya HIPAA ya Marekani.
Health Insurance Portability and Accountability Act of 1996.

Lakini pia

2. Mtu anapochagua kuwa kiongozi, anachagua kuacha kuishi maisha ya mwananchi wa kawaida na kuyatoa maisha yake yawe ya kuwahudumia wananchi. Kwa hivyo kuna dhana kwamba, kama moja ya nguzo za uongozi kimaadili ni uwazi, viongozi wanawajibika kuwataarifu wananchi pindi wanapopata matatizo ya kiafya. Ni haki ya wananchi kupata taarifa hizi.

Lakini pia.

3. Taarifa hizi, hususan kwa viongozi wa juu kabisa kitaifa, zikitolewa bila tahadhari, zinaweza kuleta matatizo mengine ya kiusalama katika jamii.

Ila, mwisho wa yote.

4. Waswahili walisema, mficha maradhi, mauti humfichua.
Me nimetaka nijue tu alikua anataka kwenda kumpelekea nani uji huko ndani?

Na anataka ajue ugonjwa wa mhusika ili iweje? Hapa nachokaga
 
Viongozi wana wajibu wa kuwapa wananchi taarifa kuhusu afya zao.

Hawa ni watu waliotoa maisha yao kutumikia wananchi, na hata matibabu yao yanatokana na kodi za wananchi, hivyo, kuuliza wananchi wanataka kujua ugonjwa wa muhusika ili iweje ni kama kumuuliza mtu "unataka kujua ugonjwa wa housegirl wako ili iweje?"

Akikwambia anataka kujua ugonjwa wa muhusika ili ajue kama muhusika anaweza kuendelea na kazi ya kuongoza au hawezi watu waanze kutafuta kiongozi mwingine ili mgonjwa asisumbuliwe na majukumu ya uongozi utasemaje?
 
Viongozi wanawajibu wa kuwapa wananchi taarifa kuhusu afya zao.

Hawa ni watu waliotoa maisha yao kutumikia wananchi, na hata matibabu yao yanatokana na kodi za wananchi, hivyo, kuuliza wananchi wanataka kujua ugonjwa wa muhusika ili iweje ni kama kumuuliza mtu "unataka kujua ugonjwa wa housegirl wako ili iweje?"

Akikwambia anataka kujua ugonjwa wa muhusika ili ajue kama muhusika anaweza kuendelea na kazi ya kuongoza au hawezi watu waanze kutafuta kiongozi mwingine ili mgonjwa asisumbuliwe na majukumu ya uongozi utasemaje?
Seriously? Seriously? Afya ya mtu binafsi?
 
Viongozi wana wajibu wa kuwapa wananchi taarifa kuhusu afya zao.

Hawa ni watu waliotoa maisha yao kutumikia wananchi, na hata matibabu yao yanatokana na kodi za wananchi, hivyo, kuuliza wananchi wanataka kujua ugonjwa wa muhusika ili iweje ni kama kumuuliza mtu "unataka kujua ugonjwa wa housegirl wako ili iweje?"

Akikwambia anataka kujua ugonjwa wa muhusika ili ajue kama muhusika anaweza kuendelea na kazi ya kuongoza au hawezi watu waanze kutafuta kiongozi mwingine ili mgonjwa asisumbuliwe na majukumu ya uongozi utasemaje?
Kiranga maswala ya ugonjwa yanataka faragha
Hata wewe hapo ukiumwa kwanza issue yako itabakia ndani ya familia

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kiranga maswala ya afya yanataka faragha
Hata wewe hapo ukiumwa kwanza issue yako itabakia ndani ya familia

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23] kiranga ana shida jaman. Afya ya mtu hataki kuelewa kama ni faragha. Kuna magonjwa mengine hata tu ukiwa si kiongozi watu hawataki muyajue magonjwa yao. Simply because wengine hawapendi kuhurumiwa. Mfano cancer. Kila saa aunapomuangalia kwa huruma na kumuambia masikin maskin maskin basi ndo unazidi mkatisha tamaa. Wanahitajo privacy kubwa na usalama kwao
 
Seriously? Seriously? Afya ya mtu binafsi?
Kiongozi si mtu binafsi, ni mtu aliyejivua haki zake za mtu binafsi na kuamua kuwa "public figure".

Angetaka kuwa na faragha ya "mtu binafsi", asingegombea uongozi tungetetea haki zake za faragha.

Waingereza wanasema "You can't eat your cake and have it too".

Yani watu wana uchaguzi wa kuamua, ama wanataka maisha ya faragha, bila ya kuwa viongozi, au wanataka maisha ya uongozi, yasiyo na faragha.

Haitakiwi mtu agombee uongozi na kutoa maisha yake yawe ya huduma kwa wananchi, huduma ambayo inategemea afya yake kuwa nzuri, halafu akipata matatizo ya kiafya atake kufanya faragha afiche.

That is like eating your cake and expecting it to be there. Kama unataka maisha ya faragha, usigombee uongozi.

Ndiyo maana Rais Mstaafu Kikwete alipopata matatizo ya tezi dume aliutangazia ulimwengu. Bila aibu. Namuheshimu sana Kikwete kwa hilo, ingawa kuna matatizo yake mengine ya kuangukaanguka tangu zamani hakuyasema wazi, kwa sababu za kisiasa.

Kama kawaida, viongozi wetu wanajifunza mambo baada ya kutoka madarakani.

Sasa wewe ungependa mtu mwenye kifafa kwa mfano, anayeangukanguka kila mara, agombee urais bila ya kuwaambia watu kwamba ana kifafa na muda wowote anaweza kuanguka jukwaani? Utaona mtu ana haki ya kugombea urais bila kuwataarifu wananchi kwamba ana kifafa? Kwa sababu ni suala la binafsi?

Unapokuwa kiongozi wa nchi, suala la afya binafsi ni suala la usalama wa taifa.

Nyerere aliwahi kusema hili, rais akikohoa tu watu wanaulizana, kile kikohozi cha kawaida au ana kifua kikuu yule?
 
Aisee, yaani pamoja na ufafanuzi wote huo hujaelewa?

Naongeza mfano:

Wewe kama mwajiriwa, unaugua, unapewa mapumziko ya muda say week, unarudi unaugua tena ndani ya muda mfupi, unahitaji mapumziko zaidi.

Mwajiri wako atahitaji kujua tatizo linalokusumbua ili kuona kama kuna umuhimu wa kukupunguzia majukumu, unaweza kuta chanzo ni hizo kazi.

Au ikibidi kukubadilishia kitengo, au kuleta mtu wa kusaidiana naye ili kazi zisilale.

Wananchi wana haki na wajibu wa kujua maendeleo ya afya kwa viongozi ambao wanalipwa kutokana na Kodi za wananchi. As wananchi ndo waajiri.
 
Kiranga maswala ya ugonjwa yanataka faragha
Hata wewe hapo ukiumwa kwanza issue yako itabakia ndani ya familia

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Sawa, lakini mimi si kiongozi.

Hutakiwi kunifananisha mimi na kiongozi.

Mimi nikifariki kwa ugonjwa huo ni msiba wa familia na ndugu jamaa na marafiki, hakuna impact ya kitaifa.

Suala la afya ya kiongozi ni suala la usalama wa taifa.

Kiongozi akifariki kuna impact ya kitaifa.

Kwa hiyo, unafananisha mambo ambayo hayafanani.
 
Hii hospital ni kubwa na ya kisasa kuliko zote Tanzania inatibu viongozi wa serikali. Hata jakaya alipodondoka kwenye kampeni za uchaguzi pale jangwani Mara mbili alikimbizwa na kuletwa pale DMMH pia ina underground basement. Kimsingi huduma za pale ni Kama za John Hopkinson.

Eti kama Johns Hopkins. Unaleta mzaha wewe.
 
@Kiranga tena wanatakiwa kuwa wanatangaza kwenye magazeti ya serikali kama taarifa kwa umma hasa the citizen na daily news ili tuwe tunaona kabisa
 
Aisee, yaani pamoja na ufafanuzi wote huo hujaelewa?

Naongeza mfano:

Wewe kama mwajiriwa, unaugua, unapewa mapumziko ya muda say week, unarudi unaugua tena ndani ya muda mfupi, unahitaji mapumziko zaidi.

Mwajiri wako atahitaji kujua tatizo linalokusumbua ili kuona kama kuna umuhimu wa kukupunguzia majukumu, unaweza kuta chanzo ni hizo kazi.

Au ikibidi kukubadilishia kitengo, au kuleta mtu wa kusaidiana naye ili kazi zisilale.

Wananchi wana haki na wajibu wa kujua maendeleo ya afya kwa viongozi ambao wanalipwa kutokana na Kodi za wananchi. As wananchi ndo waajiri.
Sielewi kwa nini point hii inakuwa ngumu kueleweka.
 
Kiongozi si mtu binafsi, ni mtu aliyejivua haki zake za mtu binafsi na kuamua kuwa "public figure".

Angetaka kuwa na faragha ya "mtu binafsi", asingegombea uongozi tungetetea haki zake za faragha.

Waingereza wanasema "You can't eat your cake and have it too".

Yani watu wana uchaguzi wa kuamua, ama wanataka maisha ya faragha, bila ya kuwa viongozi, au wanataka maisha ya uongozi, yasiyo na faragha.

Haitakiwi mtu agombee uongozi na kutoa maisha yake yawe ya huduma kwa wananchi, huduma ambayo inategemea afya yake kuwa nzuri, halafu akipata matatizo ya kiafya atake kufanya faragha afiche.

That is like eating your cake and expecting it to be there. Kama unataka maisha ya faragha, usigombee uongozi.

Ndiyo maana Rais Mstaafu Kikwete alipopata matatizo ya tezi dume aliutangazia ulimwengu. Bila aibu. Namuheshimu sana Kikwete kwa hilo, ingawa kuna matatizo yake mengine ya kuangukaanguka tangu zamani hakuyasema wazi, kwa sababu za kisiasa.

Kama kawaida, viongozi wetu wanajifunza mambo baada ya kutoka madarakani.

Sasa wewe ungependa mtu mwenye kifafa kwa mfano, anayeangukanguka kila mara, agombee urais bila ya kuwaambia watu kwamba ana kifafa na muda wowote anaweza kuanguka jukwaani? Utaona mtu ana haki ya kugombea urais bila kuwataarifu wananchi kwamba ana kifafa? Kwa sababu ni suala la binafsi?

Unapokuwa kiongozi wa nchi, suala la afya binafsi ni suala la usalama wa taifa.

Nyerere aliwahi kusema hili, rais akikohoa tu watu wanaulizana, kile kikohozi cha kawaida au ana kifua kikuu yule?
Nakubaliana na wewe kabisaaa kabisaa kabisaa. Kama kuumwa kila mtu huumwa. Na hawa wanaoongoza pia ni taasisi. Wako.wengi watendaji zaidi yao nyuma yao hivyo naamini hakuna la kusimama.

Jk ukikmtaja roho inauma sana. Kuhusu kuanguka anguka wazee wa Ruangwa watakua wanajua zaidi[emoji28]
 
Hospitality yao,cha ajabu stroke yeye haifahamu
Waanze tuu[emoji28][emoji23][emoji23][emoji23] mafiiii. Hao ni kusugua soli. Kuna naowajua wamesugua soli tola nasoma miaka 10 ilopita leo ndo wametoboa wanapata teuzi tena za chini huku
 
Sawa, lakini mimi si kiongozi.

Hutakiwi kunifananisha mimi na kiongozi.

Mimi nikifariki kwa ugonjwa huo ni msiba wa familia na ndugu jamaa na marafiki, hakuna impact ya kitaifa.

Suala la afya ya kiongozi ni suala la usalama wa taifa.

Kiongozi akifariki kuna impact ya kitaifa.

Kwa hiyo, unafananisha mambo ambayo hayafanani.
Ila kuna level ya watu fulani lazima mambo yao yawe faragha siyo kuzungmza kila mtu ajue

Ova
 
Sasa kwanini tu kwakuwa mmeamua Kutuficha Watanzania kuhusu Kulazwa Kwao hapo Mzena Hospital basi hata Wakifa ( Wakifariki ) msiendelee pia Kutuficha kwa Kutotujajia hiyo Hospitali na badala yake muendelee tu na Ratiba zenu za Maziko nyie nyie kama nyie pamoja na Wauguzi wa Mzena Hospital na wale Walinzi Wanoko wenye Maswali ya Kukomoa pale Getini Makumbusho? Tumeivumilia hii tabia tumechoka na badilikeni!
Hii issue ya Mzena Hospital inazidi ku-trend sana hapa JF bila sababu ya msingi.
Kwani kiongozi akiumwa wewe binafsi unateseka na nini?
 
Back
Top Bottom