Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ofisi ya Rais.Hivi hiyo hospital ni kwa ajili ya kina nani??
GoodViongozi wana wajibu wa kuwapa wananchi taarifa kuhusu afya zao.
Hawa ni watu waliotoa maisha yao kutumikia wananchi, na hata matibabu yao yanatokana na kodi za wananchi, hivyo, kuuliza wananchi wanataka kujua ugonjwa wa muhusika ili iweje ni kama kumuuliza mtu "unataka kujua ugonjwa wa housegirl wako ili iweje?"
Akikwambia anataka kujua ugonjwa wa muhusika ili ajue kama muhusika anaweza kuendelea na kazi ya kuongoza au hawezi watu waanze kutafuta kiongozi mwingine ili mgonjwa asisumbuliwe na majukumu ya uongozi utasemaje?
Kudos broKiongozi si mtu binafsi, ni mtu aliyejivua haki zake za mtu binafsi na kuamua kuwa "public figure".
Angetaka kuwa na faragha ya "mtu binafsi", asingegombea uongozi tungetetea haki zake za faragha.
Waingereza wanasema "You can't eat your cake and have it too".
Yani watu wana uchaguzi wa kuamua, ama wanataka maisha ya faragha, bila ya kuwa viongozi, au wanataka maisha ya uongozi, yasiyo na faragha.
Haitakiwi mtu agombee uongozi na kutoa maisha yake yawe ya huduma kwa wananchi, huduma ambayo inategemea afya yake kuwa nzuri, halafu akipata matatizo ya kiafya atake kufanya faragha afiche.
That is like eating your cake and expecting it to be there. Kama unataka maisha ya faragha, usigombee uongozi.
Ndiyo maana Rais Mstaafu Kikwete alipopata matatizo ya tezi dume aliutangazia ulimwengu. Bila aibu. Namuheshimu sana Kikwete kwa hilo, ingawa kuna matatizo yake mengine ya kuangukaanguka tangu zamani hakuyasema wazi, kwa sababu za kisiasa.
Kama kawaida, viongozi wetu wanajifunza mambo baada ya kutoka madarakani.
Sasa wewe ungependa mtu mwenye kifafa kwa mfano, anayeangukanguka kila mara, agombee urais bila ya kuwaambia watu kwamba ana kifafa na muda wowote anaweza kuanguka jukwaani? Utaona mtu ana haki ya kugombea urais bila kuwataarifu wananchi kwamba ana kifafa? Kwa sababu ni suala la binafsi?
Unapokuwa kiongozi wa nchi, suala la afya binafsi ni suala la usalama wa taifa.
Nyerere aliwahi kusema hili, rais akikohoa tu watu wanaulizana, kile kikohozi cha kawaida au ana kifua kikuu yule?
😎😎Sisi tukiugua tunaambiwa twende mwananyamala..hehehehehe
Kama ingesemwa kabla ya kufariki sawa tu...Why watu Wana obsession na hii hospital?
Mngeambiwa alilazwa St Thomas London mngesemaje??
Si kweli Ndugu mbona Mama Maria Nyerere (Mjane wa Baba wa Taifa) huenda Kutibiwa na Kulazwa hapo hata kwa Wiki Mbili na hutoka salama na Kupona pia?Halafu wengi wakipelekwa hapo hawaponi!
Both of the twoIko wapi hiyo hospital
Ya Serikali au Private
Watu ni waongoo[emoji119][emoji119]Si kweli Ndugu mbona Mama Maria Nyerere ( Mjane wa Baba wa Taifa ) huenda Kutibiwa na Kulazwa hapo hata kwa Wiki Mbili na hutoka salama na Kupona pia?
Hivi hiyo hospital ni kwa ajili ya kina nani??
Suala la kuelezea ugonjwa, hususan wa viongozi, lina utata sana.
1. Suala la ugonjwa ni suala la faragha. Nje ya madaktari na familia ya karibu, mtu ana uhuru asiweke habari za ugonjwa wake hadharani. Nchi zilizoendelea kuna sheria maalum zimetungwa kuhakikisha faragha ya mgonjwa inatunzwa.
Mfano ninm shwria ya HIPAA ya Marekani.
Health Insurance Portability and Accountability Act of 1996.
Lakini pia
2. Mtu anapochagua kuwa kiongozi, anachagua kuacha kuishi maisha ya mwananchi wa kawaida na kuyatoa maisha yake yawe ya kuwahudumia wananchi. Kwa hivyo kuna dhana kwamba, kama moja ya nguzo za uongozi kimaadili ni uwazi, viongozi wanawajibika kuwataarifu wananchi pindi wanapopata matatizo ya kiafya. Ni haki ya wananchi kupata taarifa hizi.
Lakini pia.
3. Taarifa hizi, hususan kwa viongozi wa juu kabisa kitaifa, zikitolewa bila tahadhari, zinaweza kuleta matatizo mengine ya kiusalama katika jamii.
Ila, mwisho wa yote.
4. Waswahili walisema, mficha maradhi, mauti humfichua.
Halafu wengi wakipelekwa hapo hawaponi!
Ilikuwa zamani wakati ikijaza tu Interns watupu bila Msaada wa Specialist Doctors ila kwa sasa wameshajirekebisha Ndugu. Nenda hutokufa.Kama mloganzila vile ukishalazwa ndo bas tena imekula kwako.
Makumbusho ndio Area 51 yetu 😀Itakuwa maarufu zaidi ya ilivyokuwa.Why watu Wana obsession na hii hospital?
Mngeambiwa alilazwa St Thomas London mngesemaje??
Nafikiri ni kwa sababu za kiusalama ndio maana wakubwa wanalazwa Mzena. Kwani wewe una bifu na nani mpaka uogope kulazwa Mwananyamala?Sisi tukiugua tunaambiwa twende mwananyamala..hehehehehe