Ugonjwa ni siri haijalishi ni nani ivi utajisikiaje nkikutangza unaumwa Haemorrhoids au rectal prolapse ni kwamba mnataka ikitokea Raisi anaumwa muambiwe Raisi ana maralia wadudu watatu?
Ugonjwa ni siri ya mtu binafsi. Hilo sijakataa.
Lakini, unapogombea urais, unakubali kujivua haki zako nyingi sana za mtu binafsi, unakuwa "public figure".
Unapangiwa ratiba nyingi sana ambazo huzitaki, lakini ni sehemu ya kazi.
Unapangiwa sheria nyingi sana za maadili za kutimiza. Watu binafsi hawajazi fomu za kuorodhesha mali zao. Rais na viongozi wengine wa umma kama wabunge wanatakiwa kufanya hivyo. Hawatakiwi kusema "haya ni mambo yetu ya faragha".
Kama unapenda sana faragha zako zisiingiliwe na watu, usigombee uongozi wa umma.
Hapo mtu akitaka kujua afya yako wakati hujachaguliwa kuongoza kitu, hutumii kodi ya watu kuhudumiwa, kuwa na faragha zako itakuwa haki.
Ukishaomba kupigiwa kura na kulipwa kwa kodi ya umma, tayari ushajivua ubinafsi. You become a public person.
Waingereza wanasema "with great power, comes great responsibility". Wafaransa wanasema "Noblesse oblige". Kwenye Biblia kuna mfano Yesu aliwapa watu tofauti talanta, aliyepewa talanta zaidi alidaiwa zaidi. Sasa wewe unataka mtu apewe talanta zaidi ya wengine, halafu kwenye kudaiwa adaiwe sawa na wengine?
Haya si maneno ninayoandika mimi tu.
Soma katiba ya Tanzania utaona kuna mchakato maalum wa kuangalia afya ya rais na kuichunguza kama rais anaweza kufanya kazi, na kama hawezi nini kifanyike.
Jamani someni katiba kabla ya kuketa ubishi usio na msingi hapa JF.
Rais angekuwa na haki ya faragha ya ugonjwa wake kutojulikana, kusingekuwa na vifungu vya katiba vya kuongelea afya ya rais kuchunguzwa na akionekana hawezi kazi mchakato gani ufuatwe kumpa mtu mwingine kazi za rais.
Let's argue facts. Not just made up stories.
Fact.
Katiba ina mchakato maalum wa kuchunguza afya ya rais na ku declare kama rais anafaa kuendelea kuongoza ama la, hivyo, afya ya rais si jambo la faragha isiyoweza kuchunguzwa.