Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Kuwadharau walimu ni ujinga coz hata humu tunaandika coz ni hao hao Walimu ndio waliotufundisha,

Ukimuona Mwalimu yeyote ana shida na una uwezo wa kumsaidia ni vizuri zaidi ukamsaidia kuliko kuanza kumsema au kumdharau.
ni kweli

asa hivi walimu wanalamba sukari wanampunga mrefu hatarii
 
Watanzania hatueleweki,Kazi mbaya mnaomba ya nn?
Screenshot_20220627-001935.jpg
 
Nimekwambia nilikuwa nawasaidia wadogo zangu kuapply ivi huelewi mkuuu??
Kwa kifupi wewe ni zaidi ya kichaa, ila laana na nuksi unayoitafuta utakuja hapa kuomba radhi kwa huu utoto wako.
Hakuna mtu smart duniani kote akashinda kubishana kutwa nzima wakat ushahidi upo kuwa wewe bado hujui kitu kwa jinsi tu ulivyokuwa ukihangaika kuulizia mambo.
Ukiwa muongo basi jitahidi kuwa na kumbukumbu, subiri maisha yakupige kwanza utakuja kutia adabu
 
Anayedharau walimu, alikuwa anahangaika sana kuomba kazi hiyo anayodharau.

Sijui huwa mnafaidika nini yaani, nawaza nakosa jibuView attachment 2273387View attachment 2273389View attachment 2273390View attachment 2273391View attachment 2273392
Asichokijua kuna mpaka namba ya simu iliyotumika baina yake na mtu mwingine, Sasa anataka tufanye jambo tule ban ila mtakaobaki mtamjua huyo mlemavu wa akili. Bahat yake sheria haziruhusu ila leo angejutia hii mada yake.
 
Hili sio uongo lipo wazi kabisa moja ya watumishi wa serikali wanaodharaulika kwenye jamii ni hili kundi la walimu. Hata muonekano wao umekuwa ni too primitive huku wakijidifence eti ni dressing code ya mwalimu lakini nguo zao huwa ni zilezile Shati kubwa ndefu na suruali iliyopwalaruka. Hata wakiwa wanatembea wamejawa na msongo wa mawazo wananuka madeni kila kona utakuta wanadaiwa kila duka mala kakopa dagaa, kakopa sukari, kakopa Unga, kakopa Mchele, mafuta na kila aina ya takataka dhamana yake ni kazi aliyonayo kwahiyo mda wote anaangalia tarehe ya mshahara ikifika tu ndowanakuwa wa kwanza kujazana benki yani siku hiyo panakuwa hapatoshi ni kero tupu, siku za mshahara almost zipo sawa kwa kila mtumishi wa umma ila walimu ikifika net day of salary yupo benki nadhani ni kutokana na madeni aliyonayo pamoja na ukata wa nyumbani maana hawa watu wanalisha Familia kubwa, ya kwake na ndugu zake.

Hii tabia imekuwa ikinifanya nakwazika nakuwaonea huruma pia. Fedheha nyingine nikuwa walimu wengi wanaenda wenye hakili ndogo au waliofeli hili hata Samia alilisema zanzibar, hali hii imekuwa ikipelekea ongezeko kubwa la walimu mitaani wasionaajira bahati mbaya hawana skills zakujiajiri kutokana na low IQ waliyonayo kwahiyo matazamio yao ni kusaka huruma za watawala ili wawaajiri.

Mifano iko wazi, hizi ajira za juzi zilizotangazwa na tamisemi za afya na walimu, idadi kubwa ya walioomba ni walimu, waliomba zaidi ya laki moja wakigombania nafasi elfu tisa lakini afya hawakuzidi elfu thelasini kwa nafasi elfu saba. Hapo unaweza ukaona urahisi una gharama zake, ualimu ni ajira za watu wenye level ndogo ya uelewa darasani lakini udaktari sio program ya kitoto hiyo wanaoenda ni PCB smart hakuna matapitapi ya HKL wala wenye four za form six.

Njaa za walimu zimezidi mipaka. Kwanza hawana subira, angalia tu hizi ajira walizotoa tamisemi, walimu wanasumbua hadi aibu naona mimi, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii wanatia huruma hadi kinyaa. Utasikia toeni pdf, mda wote utasikia toeni majina hawajui wizara Ina kazi nyingi za kufanya halafu majina yakitoka siku hiyo hiyo kero inaanza wa naanza kuuliza ajira za walimu mnatoa lini.

Mimi nadhani hii sekta ya walimu kama wizara mnaidekeza sana ndio mana mnawageuza kama cheap labor kwenye kazi za kitaifa kama sensa na uchaguzi mkuu maana mnajua wanalipika kwa pesa ya mrenda. Mbona hamuwachukui madaktari na watu wa TRA au TPDC tuone kama watakubali viajira vya sensa. Sasa mtazamo wangu walimu waanze kwenda wenye ufaulu mzuri kama kada zingine, hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya walimu wenye njaa njaa wanalia saaana,

Walimu waanze kupigwa interview kama kada zingine za utumishi ili kubaini vilaza na smart. Hii hali itapunguza mlundikano wa hawa watu kwenye competition za ajira. Wapigwe oral na written interview ili akili ziwakae sawa. Mbona tuliosoma kada zingine tunakaa mitaani miaka zaidi ya minne nahatusikii ajira zimetangazwa na hata zikitoka hatuanzi kero za kudai majina kwa haraka kama tunakimbizwa. Walimu hawana uvumilivu.

Sina Nia mbaya ila haya mawazo niliyotoa kama yatafanyiwa kazi basi walimu wataanza kuheshimika kama wafanyakazi wengine wa serikalini. View attachment 2271988
Labda watu wachache kama wewe,ilahawa wanakazi kweli kweli karibia sawa na manesi,mtoto anaenda shule akilamba Kamasi,mara kapuuu,mara hajui kuoga ,kuvaa na hatakuongea.Halafu umdharau teacher,utapata laana wewe 🏋️
 
Labda watu wachache kama wewe,ilihawa wanakazi kweli kweli karibia sawa na manesi,moto anaenda shule akilamba Kasi,mara kapuuu,mara hajui kuoga ,kuvaa na hatakuongea.Halafu umdhatau teacher,utapata laana wewe [emoji2484]
Kajifunze kuandika kwanza, sijui umeandika lugha gani
 
Mkuu mpwayungu village labda nikwambie vitu viwili ambavyo vitakusaidia kama mwanaume

1-Acha shobo kwa mambo yasiyokuhusu.Kama hii issue ya walimu umeona inakukera unaweza kufanya jambo katika kuleta mabadiliko

2-Acha utoto na tabia za kishamba.Labda Kama hujui jaribu kupitia threads zote unazoandika humu jukwaani pamoja na comments zitolewazo kukulenga utagundua ni kwa namna gani watu wanakuchukulia hapa JF japo una uhuru wa kuwasilisha chochote hapa ila angalia sana namna unavyojenga hoja ili kujilindia heshima yako kama member wa JF

NB:Mimi sio mwalimu ila ni mtazamo wangu juu ya hoja zako tuu
 
Asichokijua kuna mpaka namba ya simu iliyotumika baina yake na mtu mwingine, Sasa anataka tufanye jambo tule ban ila mtakaobaki mtamjua huyo mlemavu wa akili. Bahat yake sheria haziruhusu ila leo angejutia hii mada yake.
Mkuu HesabuKali fanya majamboz dogo ajutie ujinga aliobandika humu
 
Back
Top Bottom