Ni kwanini waliosomea Ujasusi ( Unjagu ) nchini Israeli 'wanaogopeka' sana kuliko waliosomea nchi zingine?

Ni kwanini waliosomea Ujasusi ( Unjagu ) nchini Israeli 'wanaogopeka' sana kuliko waliosomea nchi zingine?

Israel ilianza ujasusi toka miaka 4000 kabla ya Yesu[KK] hivi, pale Musa alipomtuma Caleb na wenzie kuipeleleza Canaan [ Hesabu 13 ; 1]. Leo [ 2021] MOSSAD wana miaka 6000 hivi ya uzoefu, na damu yao ina vinasaba vizuri sana kwenye upelelezi. Hao FBI, Scotland Yard, KBF, na wengine, wanaheshimu na kufuata hatua zao ili wawe bora zaidi.

Yoshua aliwatuma watu wawili kwenda kuupeleleza mji wa Yeriko, wakafikia kwa Rahabu yule kahaba (soma kitabu cha Yoshua 2:1-24). Musa alituma watu kwenda kuipeleleza nchi ya Kanaani na alichagua katika kila kabila mtu mmoja. Kumbuka kuna makabila 12 ya wana wa Israel ambayo yapo hata hivi leo(soma kitabu cha Hesabu 13:1-33). Ila inasadikika watu wa kabila la Asheri ndo wengi wako katika taaluma ya upelelezi huko kwao. Na wanawake nasikia wako njema mno katika sekta hii, wamejaa huko Mossad na CIA.
Israel ndo mwanzilishi wa taaluma ya upelelezi duniani. Ndio maana yuko njema mno kwenye eneo hili
 
Nchi ya Israel imeanzishwa mwaka 1948 kwa hisani ya Uingereza.
OK sasa hao wayaudi walitokea wapi

Tanzania ilianzishwa mwaka 1964.Kwa hiyo kabla ya hapo hawakuwepo watu Dar, Mbeya, Arusha, Morogoro na Lindi

Kwa hiyo kabla ya 1964,Hao Taifa jipya la Tanzania walitokea wapi?

Kuna vituko sana JF, Taifa likiundwa jipya kwa hiyo wale waliokuwepo sio wa asili ile tena
 
Kama kawaida najua hapa JamiiForums kuna Watu Wajuvi ( Pundits ) kabisa wa Mambo haya na mbalimbali hivyo hamtoshindwa 'Kunielimisha' Mimi Ngumbaru ( Layman ) niliyetukuka.

Sina uhakika sana ila nimewahi kuona mahala ( katika Bandiko ) kuwa Majasusi ( Manjagu ) wa nchi ya Rwanda 'wanaogopeka' mno Ukanda huu kwakuwa Rwanda imeingia Makubaliano 'Maalum' ya kupeleka huko Watu wake ili 'wakapikwe' na 'wakaivishwe' vyema na Wayahudi ambao inasemekana kuwa ndiyo 'Mama' wa Sekta hii duniani.
Mabingwa wa hiyo sekta, utake ustake ni Pakistan. Wengine watakaa Sana..
 
kwa sababu waliweza ,walimuua Yesu bila kosa😉 halafu pia Israel ndio ina satelaiti maalumu kwa ajili ya intellejensia tu
kuna uzi humu aliuleta habib au da vinci aliupembua vzr sana kumuhusu jizas.kwamba aliuliwa kwa sababu za kisiasa na watawala wa kiroma.
 
Tanzania [Tanganyika then], ilipata uhuru 1961, lakini haimaanishi ya kwamba haikuwai kuwepo huko nyuma[ Kumbuka Chifu Mangungo wa Msovero morogoro alivyoiuza nchi kwa Carl Peters wa Ujerumani miaka ya 1884]. China ilipata Uhuru 1944, toka kwa Wajapani lakini China ilikuwepo toka miaka mingi nyuma. Hivyo hivyo kwa Israel, Miaka 4000 BC walikuwa {Israel}Canaan, alafu wakaenda Misri, then wakarudi { Israel} Canaan, alafu Wakachukuliwa na kutawaliwa na Babuloni na Waamedi[ Iraq, kuwait na Iran], Alafu wakarudi Israel {Canaan}, Alafu wakatawaliwa na kuchukuliwa na Warumi hadi Ulaya ya leo. Hao Waingereza mwaka 1948 walipiga muhuri tu Zion {Sayuni} arudi pale Israel. Kama Waingereza wasingefanya hivyo basi, Mungu mwenyewe angewarudisha hata kwa unyakuo. USICHEZE NA BARAKA ZA MUNGU NDUGU YANGU.
Kaka shikamoo. [emoji119][emoji119] [emoji23].
 
kwa sababu waliweza ,walimuua Yesu bila kosa😉 halafu pia Israel ndio ina satelaiti maalumu kwa ajili ya intellejensia tu
Nina Askari Mmoja ( JWTZ ) sasa yuko katika Mission huko Lebanon anakuambia ukiwa na Simu nchini Israeli ni kama tu uko Uchi.

Anasema hakuna ambacho utakifanya na usijulikane ndani ya muda mfupi na kwamba Jamaa Kijasusi hawana Mpinzani.

Akaendelea kusema kuwa mpaka ndani ya Maji ya Bahari ya Mediterranean Waisraeli wameweka Mpaka na Mitambo.

Ulichokiandika nakubaliana nawe 100%.
 
Ni kweli kabisa mkuu miaka ya nyuma niliwai sima bandiko kuhusu "Mosadi" unaambiwa kati ya watu 100 mmoja tu huwa anakuwa amefaulu vizuri!

Pia unaambiwa kuna Ugaidi ulifanywa pale Club moja Israeli na watu wengi kupoteza maisha lakini unaambiwa Mosadi walituma watu wao wawili tu kuingia Lebanon,aaah siku tatu jamaa kibao wamedakwa!
Kama kawaida najua hapa JamiiForums kuna Watu Wajuvi ( Pundits ) kabisa wa Mambo haya na mbalimbali hivyo hamtoshindwa 'Kunielimisha' Mimi Ngumbaru ( Layman ) niliyetukuka.

Sina uhakika sana ila nimewahi kuona mahala ( katika Bandiko ) kuwa Majasusi ( Manjagu ) wa nchi ya Rwanda 'wanaogopeka' mno Ukanda huu kwakuwa Rwanda imeingia Makubaliano 'Maalum' ya kupeleka huko Watu wake ili 'wakapikwe' na 'wakaivishwe' vyema na Wayahudi ambao inasemekana kuwa ndiyo 'Mama' wa Sekta hii duniani.
 
Nina Askari Mmoja ( JWTZ ) sasa yuko katika Mission huko Lebanon anakuambia ukiwa na Simu nchini Israeli ni kama tu uko Uchi.

Anasema hakuna ambacho utakifanya na usijulikane ndani ya muda mfupi na kwamba Jamaa Kijasusi hawana Mpinzani.

Akaendelea kusema kuwa mpaka ndani ya Maji ya Bahari ya Mediterranean Waisraeli wameweka Mpaka na Mitambo.

Ulichokiandika nakubaliana nawe 100%.
Angalia documentary yao hapa ujue ni kwa nini :
 
Back
Top Bottom