Ni kwanini waliosomea Ujasusi ( Unjagu ) nchini Israeli 'wanaogopeka' sana kuliko waliosomea nchi zingine?

Ni kwanini waliosomea Ujasusi ( Unjagu ) nchini Israeli 'wanaogopeka' sana kuliko waliosomea nchi zingine?

Kama kawaida najua hapa JamiiForums kuna Watu Wajuvi ( Pundits ) kabisa wa Mambo haya na mbalimbali hivyo hamtoshindwa 'Kunielimisha' Mimi Ngumbaru ( Layman ) niliyetukuka.

Sina uhakika sana ila nimewahi kuona mahala ( katika Bandiko ) kuwa Majasusi ( Manjagu ) wa nchi ya Rwanda 'wanaogopeka' mno Ukanda huu kwakuwa Rwanda imeingia Makubaliano 'Maalum' ya kupeleka huko Watu wake ili 'wakapikwe' na 'wakaivishwe' vyema na Wayahudi ambao inasemekana kuwa ndiyo 'Mama' wa Sekta hii duniani.
Wewe ulivyo na Shobo sizani kama una marinda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kabisa mkuu miaka ya nyuma niliwai sima bandiko kuhusu "Mosadi" unaambiwa kati ya watu 100 mmoja tu huwa anakuwa amefaulu vizuri!

Pia unaambiwa kuna Ugaidi ulifanywa pale Club moja Israeli na watu wengi kupoteza maisha lakini unaambiwa Mosadi walituma watu wao wawili tu kuingia Lebanon,aaah siku tatu jamaa kibao wamedakwa!
Huo ni uongo ugomvi wa bar ukashike watu kibao kwa watu wawili tena nchi ya watu acheni chai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kabisa mkuu miaka ya nyuma niliwai sima bandiko kuhusu "Mosadi" unaambiwa kati ya watu 100 mmoja tu huwa anakuwa amefaulu vizuri!

Pia unaambiwa kuna Ugaidi ulifanywa pale Club moja Israeli na watu wengi kupoteza maisha lakini unaambiwa Mosadi walituma watu wao wawili tu kuingia Lebanon,aaah siku tatu jamaa kibao wamedakwa!
Comment yako imejaa neno "Unaambiwa" umelirudia sana, sasa tuambie unaposema "Unaambiwa" una maanisha tunaambiwa na nani?

Ukisha ona comment ina maneno kama "Unaambiwa" "Inasemekana" "Ina aminika" "Huenda" "Nadhani" "Nasikia" .....Ujue ni porojo tu hizo.
 
Israel wao wanawekeza mno kwenye Human Inteligency(human intel) wakati FBI,CIA na Scotland yard wanatumia sana IT systems.Israel wanaanza na Vijana wao wakiwa na miaka 16,Vijana hawa wanakuwa awajaanza pata stress za Piskali au sijui mama anataka hela anaumwa etc.pia makampuni makubwa ya technology yana research labs Israel hii inawapelekea pia kuwa wabobezi kwenye sector ya IT na Mawasiliano.Mfano mpaka leo ni Israel pekee ndo wenye uwezo wa ku unlock Iphone.
 
Imekataa Kufunguka nihadithie tu nijue.
Wanasema ni mazingira yao hasa ndio chanzo cha wao kuwa na akili kubwa... wamezungukwa na maadui kila kona... Hitler aliwapa funzo lililowafanya watumie akili za ziada kujikomboa toka maadui zao... documentary hiyo imejaa na imesheheni majasusi wa kiisrael wakihojiwa namna walivyowatafuta, kuwadhibiti, kuwakamata na kuwauwa maadaui zao...
Wanasema kwamba wako kila nchi humu duniani na wanasimulia pia jinsi walivyoiiba Ndege vita ya mig25 na mengineyo mengi...
Ni nzuri sana kuiangalia ukiweza..
 
Mkuu. mi nimetaja tu mwaka ambao Taifa la Israel limeanzisha, ni 1948.

Au nimesema uongo ndugu yangu?

Au Taifa la Israel halijaanzishwa mwaka 1948 kwa msaada wa Beberu Uingereza..?!
Kuna mambo mawili hapa, kuanzishwa kwa Israel na kuanza kwa ujasusi ni mambo mawili tofauti, je kipi kilianza?


Mfano, kuna mambo yaliyokuwa yafanyika ama yalikuwapo Tanzania/ Tanganyika kabla hata ya Tanzania/Tanganyika kuanza...
 
OK sasa hao wayaudi walitokea wapi

Tanzania ilianzishwa mwaka 1964.Kwa hiyo kabla ya hapo hawakuwepo watu Dar, Mbeya, Arusha, Morogoro na Lindi

Kwa hiyo kabla ya 1964,Hao Taifa jipya la Tanzania walitokea wapi?


Kuna vituko sana JF, Taifa likiundwa jipya kwa hiyo wale waliokuwepo sio wa asili ile tena

Mkuu, statement yangu umeielewa kweli..?

Na, unajua niliye quote alikuwa ameandika nini..?

Umeelewa muktadha wa hii thread..?
 
Back
Top Bottom