Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Majaliwa alisema Hazina wanaume wamepiga 2B ndani ya siku 2 akaunda tume mpaka leo haijulikani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usitegemee jipyaAma kweli wanakula kwa urefu wa kamba zao😄
Ripoti ya CAG na mapendekezo yake hayatekelezwi kwa sababu ya udhaifu wa bunge.Matokeo yake ripoti ya CAG siku hizi imekuwa kama mchezo wa kuigiza, inasomwa kwa mbembwe kuonesha tulivyopigwa halafu wapigaji wanalindwa, huu umasikini wa hili taifa utaendelea kuwepo kwa miaka sana mingi ijayo.
Tukiibiwa mapesa mengi na marafiki zao wanakaa kimya, lakini tukiibiwa kidogo na wasio rafiki zao ndio wanawatoa sadaka, hili taifa chini ya utawala wa CCM linaongozwa kisanii sana.
Hatua zipi zinachukuliwa?Hatua zinachukuliwa
Kama huamini jaribu kufanya upigaji ama tafuta wahusika wa huo upigaji uone kama wako salama
Nadhani labda wawe wanatangaza ili umma ujue
Sawa BabaHatua zipi zinachukuliwa?
Usitugeuze sisi ni watoto wadogo, wa kuweza kutudanganya unavyotaka🥺
Ni jambo lilizoeleka kwa mkaguzi mkuu na mdhibiti wa pesa za Serikali (CAG) kuibuka na ripoti kila mwaka, inayoonyesha namna mabilioni ya pesa ya walipa zinavyotafunwa na "wajanja" wachache walioko Serikalini, pasipo kuchukuliwa hatua zozote.
Lakini tunashuhudia magereza yetu, yakiwa yamefurika wafungwa, wakiwa wamehukumiwa kwa vijikesi, vidogo vidogo, kama vile wizi wa kuku!
Ndiyo hapo ninapouliza, hivi kuna sababu gani ya kutusomea hadharani ripoti hizo za CAG, kama Serikali yetu, haina dhamira ya dhati kuwachukulia hatua za kisheria?
Tumeshuhudia, makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdrahman Kinana, eti akisema, atamshairi Rais Samia, aweze kuwachukulia hatua za kisheria, wale wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo ya CAG!
Hivi umewahi kuona wapi watu waliotenda makosa makubwa kama hayo ya kutafuna mabilioni ya pesa ya walipa kodi wa nchi hii, eti mpaka Rais ashauriwe Ili achukue hatua za kisheria?
Mbona hawa wanaotuhumia kwa vijikesi vidogo vidogo, kama vile wezi wa vibasikeli, wakiwa wamejazana magerezani, wakiwa wameshahukumiwa tayari, kutumikia vifungo vyao, je na hao Rais ameshauriwa kabla ya kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa' vifungo vyao??
Huu mtindo unaotumika na Serikali hii ya CCM, ni wa hatari Sana, unaofanya upendeleo wa wazi kabisa na "kubariki" kwa kuwaona wale wezi wa mabilioni ya Serikali, kama mashujaa na kuachiwa watembee kifua mbele, wakati wezi wa vitu vidogo vidogo, kama wale wanaowakwapua vipochi kwa abiria kwenye daladala, ndiyo wahukumiwe vifungo mahakamani na watuhumiwa wengine hata wakipoteza Maisha yao kwa "kuhukumiwa' vipigo na wananchi wenye hasira kali!
Ndiyo maana nchi hii kodi zinakuwa nyingi mno, kama vile tozo mbalimbali, kwenye miamala ya simu, ambazo zinawakamua watanzania wanyonge, kumbe pesa hizo, zinaliwa na watanzania wachache, tuliowaamini na kuwakabidhi madaraka ya juu, Katika nchi hii!
Tunaomba viongozi wetu wa Serikali hii ya CCM, wawe "serious" na wachukue hatua mara moja na tuone watuhumiwa wote waliotajwa na CAG kukwapua mabilioni ya pesa ya walipa kodi wa nchi hii wanafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.
Pascal Mayalla naona hawa mchwa toka uhuru wa taifa hili wapo na wanaendelea kula mbao ya taifa na wewe ulionyesha nia ya dhati kugombania ubunge kwenda kuwapa support au kuzima harakati zaoHilo ombi likitokea kukubaliwa na hatimaye kufanyiwa kazi ndio utakuwa mwisho wangu wakuja hapa Jamiiforums kuchachafya nisiyoyajua.
Lakini kwa sasa, niulize tu, hiyo Serikali yenye uthubutu wa kufanya hivyo itaongozwa na Chama gani?
ACT, pwaa
CHADEMA, pwaa
CCM, pwaa
...na vile vyama vingine, vivuli, vya hao juu...only time will tell.
Ninayojua hizi Ripoti zikitokea hakuna 'kuu' linalotokea zaidi ya kuimarishwa kwa Vyama vya Kisiasa. Porojo, mihemeko, na vijembe.
Hata Kipanya ana Vijembe! Madenge naye yumo, huko twitani ndiyo usiseme, hata miye Nimo!
CAG,wala, na sintoshangaa nikasikia eti anajiuzulu, kabadilishwa na fedheha wakati hao waliotajwa(kama wametajwa) wanaendelea kupiga ramli za 'kusingiziwa' 'kuonewa'.. kadhalika na kadhalika
Binafsi nitajiuzulu kuingia hapa Jamiiforums na kwenda kuwekeza kilimo cha mihogo Chanika pale tu kuna mtu au watu watafikishwa mahakamani, na kumaliza mchakato huo, halafu kupigwa miaka stahiki Keko. Nitajiuzulu.
Ripoti za CAG ni getesha tu ni mpango mwingine wa kutafuna helaNi jambo lilizoeleka kwa mkaguzi mkuu na mdhibiti wa pesa za Serikali (CAG) kuibuka na ripoti kila mwaka, inayoonyesha namna mabilioni ya pesa ya walipa zinavyotafunwa na "wajanja" wachache walioko Serikalini, pasipo kuchukuliwa hatua zozote.
Lakini tunashuhudia magereza yetu, yakiwa yamefurika wafungwa, wakiwa wamehukumiwa kwa vijikesi, vidogo vidogo, kama vile wizi wa kuku!
Ndiyo hapo ninapouliza, hivi kuna sababu gani ya kutusomea hadharani ripoti hizo za CAG, kama Serikali yetu, haina dhamira ya dhati kuwachukulia hatua za kisheria?
Tumeshuhudia, makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdrahman Kinana, eti akisema, atamshairi Rais Samia, aweze kuwachukulia hatua za kisheria, wale wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo ya CAG!
Hivi umewahi kuona wapi watu waliotenda makosa makubwa kama hayo ya kutafuna mabilioni ya pesa ya walipa kodi wa nchi hii, eti mpaka Rais ashauriwe Ili achukue hatua za kisheria?
Mbona hawa wanaotuhumia kwa vijikesi vidogo vidogo, kama vile wezi wa vibasikeli, wakiwa wamejazana magerezani, wakiwa wameshahukumiwa tayari, kutumikia vifungo vyao, je na hao Rais ameshauriwa kabla ya kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa' vifungo vyao??
Huu mtindo unaotumika na Serikali hii ya CCM, ni wa hatari Sana, unaofanya upendeleo wa wazi kabisa na "kubariki" kwa kuwaona wale wezi wa mabilioni ya Serikali, kama mashujaa na kuachiwa watembee kifua mbele, wakati wezi wa vitu vidogo vidogo, kama wale wanaowakwapua vipochi kwa abiria kwenye daladala, ndiyo wahukumiwe vifungo mahakamani na watuhumiwa wengine hata wakipoteza Maisha yao kwa "kuhukumiwa' vipigo na wananchi wenye hasira kali!
Ndiyo maana nchi hii kodi zinakuwa nyingi mno, kama vile tozo mbalimbali, kwenye miamala ya simu, ambazo zinawakamua watanzania wanyonge, kumbe pesa hizo, zinaliwa na watanzania wachache, tuliowaamini na kuwakabidhi madaraka ya juu, Katika nchi hii!
Tunaomba viongozi wetu wa Serikali hii ya CCM, wawe "serious" na wachukue hatua mara moja na tuone watuhumiwa wote waliotajwa na CAG kukwapua mabilioni ya pesa ya walipa kodi wa nchi hii wanafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.
Hamna kitu kitakachofanyikaWala rushwa wakubwa ni viongozi wa CCM unategemea nini?
HahahaaKiuahalisia hawa wakaguzi /wathibiti wetu inabidi nao kuthibitiwa,kukaguliwa na kuhojiwa na Bunge letu. Bunge lenyewe liliondolewa spika na likabaki kimya kabisa.
Naona wanaidhalilisha tu hii ofisi sababu hawaonekani wakiwa serious zaidi ya kutumika kisiasa, maigizo.