Ni Kwanini Watanzania hufurahia mtu akipatwa na matatizo au kuyumba kiuchumi au kutumbuliwa?

Ni Kwanini Watanzania hufurahia mtu akipatwa na matatizo au kuyumba kiuchumi au kutumbuliwa?

Ndugu zangu Watanzania,

Mimi Lucas Mwashambwa nikiri kwa moyo wa dhati kabisa pasipo unafiki wa aina yoyote ile ya kuwa ni mtu ambaye hufurahia mafanikio ya mtu,kupanda kwa mtu kiuchumi,kupata mafanikio katika maeneo mbalimbali.mimi nikiona mtu wa karibu yangu au niliyekuwa namfahamu au kusoma naye amepata kazi au ajira au kuinuka kiuchumi au kupata mafanikio katika eneo fulani au amekua na kuimarika kibiashara.

Huwa ninafurahi sana na kumuombea sana.huwa naona kabisa kumbe inawezekana kabisa mtu yeyote kufanikiwa ikiwa tu utafanya kazi kwa bidii, juhudi, maarifa na kujituma kwa hali ya juu sana pasipo kuleta ujuaji au kuchagua kazi. Huwa nina kuwa na imani kuwa unaweza kuwa yeyote yule na uchumi wa aina yoyote ile au kumiliki kitu chochote kile au kuwa na mali za halali kabisa za kiasi chochote kile wakati wako ukifika.

Sasa huwa nashangaa sana na kuumia sana na kusikitika sana na kuwaza mengi sana na kujisikia vibaya sana na kusononeka sana napoona watanzania wenzangu wakifurahia na kuchekekelea pale wanapoona mtu fulani aliyekuwa ni tajili au mwenye uchumi mkubwa na wa halali ameshuka na kuyumba.

Unakuta mtu alikuwa anasaidia sana Watu na kujitolea vizuri sana kwa watu mbalimbali wenye shida na matatizo bila kujali ni ndugu au siyo ndugu, lakini siku akifirisika tu unaanza kuona watu walewale waliokuwa wanasaiidiwa wanaanza kumcheka pembeni na kumsema vibaya Majungu ya kila aina.unajiuliza shida ni nini?

Je mtu akifirisika inanifanya vipi mimi Lucas Mwashambwa na umasikini wangu kuwa tajiri na kuinuka kiuchumi ikiwa sifanyi kazi na kujituma? Wewe mtanzania mwenzangu mwingine unayefurahia kushuka kiuchumi kwa mtu mwingine unafaidika vipi na anguko lake?

Unakuta pia leo mtu anaondolewa leo kwenye nafasi yake ya uteuzi halafu watu wanajitokeza na kuanza kushangilia na kufanya sherehe ,halafu mtu yule yule akirudishwa tena kesho unakuta watu walewale wanaanza kujipendekeza na kujiuma uma kwa aibu na unafiki. Shida yetu nini watanzania wenzangu?

Kwanini hatuombeani mema? Kwanini hatuombeani baraka na neema?kwanini tunaombeana mabaya? Ndugu zangu ikiwa kwa maombi yako mimi nitasimama tena basi niombee na siyo kunicheka au kumcheka mtu.

Imefika wakati naona watu mitaani wanaona wivu hata mtu akiona Binti wa jirani yake amepata mchumba na kuolewa.utasikia mama mzima na akili yake na mwenye watoto akitamka kuwa huyo haendi kudumu kwenye ndoa yake na ni lazima ataachika. Ukiangalia nini shida unakuta ni wivu tu wa kijinga jinga tu kwa sababu yeye watoto wake hawajaolewa.

Inafika wakati unasikia watu mpaka wanakwenda na kujiingiza kwenye imani za kishirikina ili tu kumharibia maisha mtu au biashara yake au kazini kwake ili tu asiendelee kuwepo katika nafasi aliyopo.tuacheni kabisa tabia hizo ndugu zangu. Tuwe na mioyo ya kupendana na kuombeana mema na heri. Tuache mioyo ya wivu na chuki za kijinga jinga.nimekutana na haya mambo ndio maana naandika kwa uchungu mkubwa sana juu ya jambo hili.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Sababu kubwa ni kwamba anapokuwa madarakani haoni shida za wengine.
 
Sio watanzania tu.hii ni kwa dunia nzima.
MUNGU na mazuri yote aliyofanya bado kuna watu wanamchukia sembuse binadamu kwa binadamu?
hyo ni dhambi ya asili ilianza kwa cain na abil itadumu vizazi na vizazi
 
Kwa sababu bado tunaamini methali ya kitapeli ya wahenga 'Aliye juu mngoje chini'

Wahenga walioleta hiyo methali walikuwa wavivu sana. Kucha kushinda kwenye mchezo wa bao.
 
Achana na watu kuambiwa fulani ana roho mbaya au yuko hivi (na pengine ukafuata mkumbo wao tu) ilhali huyo mtu humjui.

Vinginevyo kwa watu unaowajua wewe na wenye kuonewa wivu na wengine kwa kuwasemwa vibaya. Kati yao kuna hata mmoja mwisho wa siku hakufanikiwa (dua la kuku uwa, alimpati mwewe).

Hakuna mtu anaweza zuia mipango ya mungu. Maskini tu ndio wanaweza sherehekea kuanguka kwa tajiri.

Sasa maskini ni mtu ambae keshajimianisha kupata ni bahati. Maana yake umaskini ni fikra tu.

Hao watu wanao ombewa mabaya kawaida uwa hawajali, kwa sababu wanajitambua kwa kuelewa vita ni mbinu (maana yake m wana mipango ya kufikia wanapotaka) sasa kuna ajali kazini. Kuna kupanda na kushuka kabla ya kufika kileleni ni kawaida.

But then aina maana tuache kuyasema mafisadi haya ni majizi tu ya hela za walipa kodi. Kama kweli waelevu watajirike kwa ubunifu wao wa kuzalisha au akili zao kuacha impact either serikalini au kwenye private sector.
 
Hizo ni dalili za uvivu na umasikini. By nature watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri na hata kufanya kazi, ndio maana utashangaa kuona nchi kubwa kama hii yenye mito na maziwa ya kutosha bado kuna watu wanaishi kwenye lindi la umasikini wa kutupwa na wakisumbuliwa na njaa.
 
Hizo ni dalili za uvivu na umasikini. By nature watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri na hata kufanya kazi, ndio maana utashangaa kuona nchi kubwa kama hii yenye mito na maziwa ya kutosha bado kuna watu wanaishi kwenye lindi la umasikini wa kutupwa na wakisumbuliwa na njaa.
Shida yenu ni civil services very weak.

Sasa civil services 70% ni usalama wa taifa.

Kwa katiba ya Tanzania ambayo raisi anaweza teua makada kwa nafasi ambazo azawaizi kuzifikia inataka succession planning and performance appraisal (meritocracy) yeye anaamua tu.

Mna safari ndefu sana ya maendeleo, kilichopo ni unga unga tu. Tusizanie hao walioendelea nchi zao zinaendeshwa kwa mzaha kama Tanzania.

Usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili tu
 
Siyo watanzania, hiyo ni sifa ya binadamu duniani.

Kumbuka Biblia inasema Lucifer alifukuzwa na Mungu huko kwao, na akamtupa Duniani, na Adama na Hawa walipomkosea Mungu muumba wao aliye muumba adam kwa mfano wake, nao aliwafukuzwa huko kwao Eden akawatupa Duniani.

Maana yake dunia hii ni mahala wanapokaa waovu, kwa maneno mengine hii dunia ni kama Gereza la wakosefu. Hatufahamu Lucifer ana umbo gani, ila tuna mfahamu mwanadamu wa kike na wa kiume yani adama na Hawa.

Inaelekea wapo viumbe ambao hawajawahi kumuasi muumba wao wanaishi huko tusiko kufahamu, lakini hao watatu biblia inasema walifukuzwa kwao kutokana na utukutu wao, au kutokuwa wasikivu, na wasiotii masharti ya muumba wao.

Yani kwa maana nyingine Duniani ni mahala ambako Mungu anatupa taka taka zake. Maana kuna sayari zingine hatuju huko wanaishi viumbe gani wana maumbo gani, wanaishi vipi, na pia sayansi inatuambia kuna galax zingine na sayari nyingi tu lakini hatufahamu Mungu anaishi wapi, Juu ya uso wa jua au Jua ndiyo Jehanam kwenyewe, kunako waka moto usiozimika, ambako tunaambiwa Mungu huchoma taka zinapozidi humu duniani.


Kama na-wewe unaishi humu duniani, kumbuka kwamba unaweza kuwa ama ni Lucifer, Hawa au Adam, sasa kwa sifa ya uovu unategemea nini kitokee?

Tujikubali tu, we in this together.
 
Kuna wakati najiuliza kama hapa nilipo ni duniani au KUZIMU.

Watu ni wachawi aiseee, ni vile tu hawapai na matunguli lakini ni wachawi konki.

Nashukuru Mungu Matunguli yamepanda bei maana wangetumaliza.

Wivu ni mkali, hata ukivaa shati jipya wanatamani wakumalize khaaa
 
Kuna wakati najiuliza kama hapa nilipo ni duniani au KUZIMU.

Watu ni wachawi aiseee, ni vile tu hawapai na matunguli lakini ni wachawi konki.

Nashukuru Mungu Matunguli yamepanda bei maana wangetumaliza.

Wivu ni mkali, hata ukivaa shati jipya wanatamani wakumalize khaaa
Umenena ukweli kabisa
 
Back
Top Bottom