Ni Kwanini Watanzania hufurahia mtu akipatwa na matatizo au kuyumba kiuchumi au kutumbuliwa?

Sababu kubwa ni kwamba anapokuwa madarakani haoni shida za wengine.
 
Sio watanzania tu.hii ni kwa dunia nzima.
MUNGU na mazuri yote aliyofanya bado kuna watu wanamchukia sembuse binadamu kwa binadamu?
hyo ni dhambi ya asili ilianza kwa cain na abil itadumu vizazi na vizazi
 
Sababu kubwa ni kwamba anapokuwa madarakani haoni shida za wengine.
Hujaona watu wakisaidia Watu kwa hali na mali na kuwa na marafiki wengi lakini wakitoka tu madarakani unaona marafiki wote wanapotea na kuanza kupiga Majungu.
 
Kwa sababu bado tunaamini methali ya kitapeli ya wahenga 'Aliye juu mngoje chini'

Wahenga walioleta hiyo methali walikuwa wavivu sana. Kucha kushinda kwenye mchezo wa bao.
 
Achana na watu kuambiwa fulani ana roho mbaya au yuko hivi (na pengine ukafuata mkumbo wao tu) ilhali huyo mtu humjui.

Vinginevyo kwa watu unaowajua wewe na wenye kuonewa wivu na wengine kwa kuwasemwa vibaya. Kati yao kuna hata mmoja mwisho wa siku hakufanikiwa (dua la kuku uwa, alimpati mwewe).

Hakuna mtu anaweza zuia mipango ya mungu. Maskini tu ndio wanaweza sherehekea kuanguka kwa tajiri.

Sasa maskini ni mtu ambae keshajimianisha kupata ni bahati. Maana yake umaskini ni fikra tu.

Hao watu wanao ombewa mabaya kawaida uwa hawajali, kwa sababu wanajitambua kwa kuelewa vita ni mbinu (maana yake m wana mipango ya kufikia wanapotaka) sasa kuna ajali kazini. Kuna kupanda na kushuka kabla ya kufika kileleni ni kawaida.

But then aina maana tuache kuyasema mafisadi haya ni majizi tu ya hela za walipa kodi. Kama kweli waelevu watajirike kwa ubunifu wao wa kuzalisha au akili zao kuacha impact either serikalini au kwenye private sector.
 
Hizo ni dalili za uvivu na umasikini. By nature watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri na hata kufanya kazi, ndio maana utashangaa kuona nchi kubwa kama hii yenye mito na maziwa ya kutosha bado kuna watu wanaishi kwenye lindi la umasikini wa kutupwa na wakisumbuliwa na njaa.
 
Shida yenu ni civil services very weak.

Sasa civil services 70% ni usalama wa taifa.

Kwa katiba ya Tanzania ambayo raisi anaweza teua makada kwa nafasi ambazo azawaizi kuzifikia inataka succession planning and performance appraisal (meritocracy) yeye anaamua tu.

Mna safari ndefu sana ya maendeleo, kilichopo ni unga unga tu. Tusizanie hao walioendelea nchi zao zinaendeshwa kwa mzaha kama Tanzania.

Usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili tu
 
Siyo watanzania, hiyo ni sifa ya binadamu duniani.

Kumbuka Biblia inasema Lucifer alifukuzwa na Mungu huko kwao, na akamtupa Duniani, na Adama na Hawa walipomkosea Mungu muumba wao aliye muumba adam kwa mfano wake, nao aliwafukuzwa huko kwao Eden akawatupa Duniani.

Maana yake dunia hii ni mahala wanapokaa waovu, kwa maneno mengine hii dunia ni kama Gereza la wakosefu. Hatufahamu Lucifer ana umbo gani, ila tuna mfahamu mwanadamu wa kike na wa kiume yani adama na Hawa.

Inaelekea wapo viumbe ambao hawajawahi kumuasi muumba wao wanaishi huko tusiko kufahamu, lakini hao watatu biblia inasema walifukuzwa kwao kutokana na utukutu wao, au kutokuwa wasikivu, na wasiotii masharti ya muumba wao.

Yani kwa maana nyingine Duniani ni mahala ambako Mungu anatupa taka taka zake. Maana kuna sayari zingine hatuju huko wanaishi viumbe gani wana maumbo gani, wanaishi vipi, na pia sayansi inatuambia kuna galax zingine na sayari nyingi tu lakini hatufahamu Mungu anaishi wapi, Juu ya uso wa jua au Jua ndiyo Jehanam kwenyewe, kunako waka moto usiozimika, ambako tunaambiwa Mungu huchoma taka zinapozidi humu duniani.


Kama na-wewe unaishi humu duniani, kumbuka kwamba unaweza kuwa ama ni Lucifer, Hawa au Adam, sasa kwa sifa ya uovu unategemea nini kitokee?

Tujikubali tu, we in this together.
 
Kuna wakati najiuliza kama hapa nilipo ni duniani au KUZIMU.

Watu ni wachawi aiseee, ni vile tu hawapai na matunguli lakini ni wachawi konki.

Nashukuru Mungu Matunguli yamepanda bei maana wangetumaliza.

Wivu ni mkali, hata ukivaa shati jipya wanatamani wakumalize khaaa
 
Umenena ukweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…