Ni Kwanini Watanzania tuna huu Ushamba sana na ambao umepitiliza?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kuna Watu Watatu kutokea Mbagala alipokuwa akiishi Mchezaji ' Mahiri ' kwa sasa wa Kitanzania Mbwana Ally Samata a.k.a Popa wamenifanya nianze Kuamini kuwa Watanzania tuna ' Nongwa ' na ' Uswahili / Upuuzi ' mno.

Ni kwamba kila mwana Mbagala sasa anajifanya alikuwa anamjua na aliweza Kumsaidia sana Samata Kipindi alipokuwa huko na kwamba na Wao pia wamechangia haya Mafanikio aliyoyapata sasa na kwamba wanaomba na Wao wakumbukwe kwa chochote Kitu a.k.a Mtonyo.

Mwana Mbagala #1
Namjua Mbwana Samata tokea akiwa Mdogo na Mimi ndiyo nilikuwa nikimpikia Chakula na Kumfichia chini ya Uvungu wa Kitanda na akitoka tu Kucheza anakikuta. Naomba asinisahau tafadhali.

Mwana Mbagala #2
Bila Mimi Kumuokoa basi enzi zake Mbwana Samata Siku moja alikimbizwa na Mbwa wa Polisi maeneo ya Kilwa na nilimuokoa kwa Kumbeba Begani huku na Mimi pia nikitoka Baru (nikikimbia) hadi nikajikwaa vingine yule Mbwa angeondoka na moja ya Kalio lake. Kama anasikiliza hii Interview yangu akiwa huko Uingereza naomba asinisahau tafadhali kwani Maisha yangu ni Magumu sasa.

Mwana Mbagala #3
Siku moja nilimkuta Samata anajisaidia haja Kubwa Kibarazani Kwao (alipokuwa bado Mdogo) na Mimi baada ya Kugundua Nyumbani Kwao kulikuwa hakuna Mtu na Msichana wa Kazi ametoka nilichukua Jukumu la Kumsafisha (Kumchamba) na nakumbuka kama Mwanamama na Mzazi nilikuwa nikifanya hivyo mara kwa mara hivyo kama atanikumbuka kwa Kuyasikia haya basi naomba Siku akija katika Mechi za Taifa Stars asinisahau kwa chochote Kitu.

Halafu wana Mbagala acheni Ushamba ( Umbwiga ) tafadhali Mbwana Samata ni wa Watanzania wote na siyo wenu tu pekee.
 
Hii yote ni shida ya kutokuwa na Elimu jumulisha umasikini.

Hakuna wanachowaza zaidi ya fursa ya kupiga vibomu. Watu hawa wako kila upande, kazi yao kuangalia waliopata na jinsi ya kujinufaisha katika mapato ya wenzao. watu hawa hawanaga bidii ya kutafuta cha kwao. wana midomo haooo, wanajua maisha ya kila mtu mtaani.

Kuwamaliza ni kuhakikisha kila mmoja anapata elimu na kupata cha kufanya.
 
tutaamini vipi hayo maelezo yametolewa na watu wa Mbagala, kama wameweza kudanganya kuwa walimsaidia Samatta wanaweza vilevile kudanganya wanatoka Mbagala kumbe wanatoka sehemu nyingine ya Dar pia si ajabu hata Samatta alipokuwa na umri huo si ajabu hata Dar es salaam walikuwa hawajakanyaga
 
hata me nilimpa demu wangu alale nae kipindi anapokuwa na genye, popote pale samatta ulipo naomba unisaidie chchte kitu.
 
tutaamini vipi hayo maelezo yametolewa na watu wa Mbagala, kama wameweza kudanganya kuwa walimsaidia Samatta wanaweza vilevile kudanganya wanatoka Mbagala kumbe wanatoka sehemu nyingine ya Dar pia si ajabu hata Samatta alipokuwa na umri huo si ajabu hata Dar es salaam walikuwa hawajakanyaga

Sasa kama hutaki Kuyaamini hayo maneno yangu unataka na Mimi niyaamini haya yako?
 
Kuna watu wana mawazo ya kimaskini na njaa imewajaa. Mtu ahangaike kupambana mwenyew leo afike alipofika then mtu anawaza kupewa hela tu as if hela anaokota.
 
Kuna dogo yuko under 20, anacheza na akina mess, juzi katupia goli 2, nchini mwao watu kimya tu, lakini angekua mbongo!!!

Nchini kwao wapi? Spain? Yeye sio wa kwanza wala wa mwisho kufanya hivyo Usifananishe spain na Tanzania. Halafu kama unamaanisha Guinea Bissau walishamtoa akilini dogo hawana time naye tena.
 
sio wana mbagala, ni wanadarisalam tena washabiki wa simba ndio washamba kupitiliza, ndio maana samata kawaponda, wana simba wote wanajifanya mashabiki wa aston villa

IMG_1777.JPG

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nchini kwao wapi? Spain? Yeye sio wa kwanza wala wa mwisho kufanya hivyo Usifananishe spain na Tanzania. Halafu kama unamaanisha Guinea Bissau walishamtoa akilini dogo hawana time naye tena.
Guinea.
 
Kuna dogo yuko under 20, anacheza na akina mess, juzi katupia goli 2, nchini mwao watu kimya tu, lakini angekua mbongo!!!
Sitaki kutukana nchi yangu wala wananchi wake lakini kusema ukweli %kubwa ya watz hatujaSTARABIKA.
N hili lknajionyeaha wazi kwenye page ya aston villa kule insta, maneno ya wadau hapo juu kama alivyoainisha mtoa uzi.
 
Waswahili aisee ni noma, mtu unapo kuwa una-struggle kwenye maisha yako ili yakae sawa kila mtu atakuona takataka,
Ukisha tusua kwenye maisha kila mtu atajifanya anakujua, walikuwa wapi ulivyo kuwa una-struggle?
 
Kuna Watu Watatu kutokea Mbagala alipokuwa akiishi Mchezaji ' Mahiri ' kwa sasa wa Kitanzania Mbwana Ally Samata a.k.a Popa wamenifanya nianze Kuamini kuwa Watanzania tuna ' Nongwa ' na ' Uswahili / Upuuzi ' mno.

Ni kwamba kila mwana Mbagala sasa anajifanya alikuwa anamjua na aliweza Kumsaidia sana Samata Kipindi alipokuwa huko na kwamba na Wao pia wamechangia haya Mafanikio aliyoyapata sasa na kwamba wanaomba na Wao wakumbukwe kwa chochote Kitu a.k.a Mtonyo.

Mwana Mbagala #1
Namjua Mbwana Samata tokea akiwa Mdogo na Mimi ndiyo nilikuwa nikimpikia Chakula na Kumfichia chini ya Uvungu wa Kitanda na akitoka tu Kucheza anakikuta. Naomba asinisahau tafadhali.

Mwana Mbagala #2
Bila Mimi Kumuokoa basi enzi zake Mbwana Samata Siku moja alikimbizwa na Mbwa wa Polisi maeneo ya Kilwa na nilimuokoa kwa Kumbeba Begani huku na Mimi pia nikitoka Baru (nikikimbia) hadi nikajikwaa vingine yule Mbwa angeondoka na moja ya Kalio lake. Kama anasikiliza hii Interview yangu akiwa huko Uingereza naomba asinisahau tafadhali kwani Maisha yangu ni Magumu sasa.

Mwana Mbagala #3
Siku moja nilimkuta Samata anajisaidia haja Kubwa Kibarazani Kwao (alipokuwa bado Mdogo) na Mimi baada ya Kugundua Nyumbani Kwao kulikuwa hakuna Mtu na Msichana wa Kazi ametoka nilichukua Jukumu la Kumsafisha (Kumchamba) na nakumbuka kama Mwanamama na Mzazi nilikuwa nikifanya hivyo mara kwa mara hivyo kama atanikumbuka kwa Kuyasikia haya basi naomba Siku akija katika Mechi za Taifa Stars asinisahau kwa chochote Kitu.

Halafu wana Mbagala acheni Ushamba ( Umbwiga ) tafadhali Mbwana Samata ni wa Watanzania wote na siyo wenu tu pekee.
Naona unatafuta Kick za kipumbavu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom