The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Nimejaribu kufanya uchunguzi na kugundua kwamba watanzania wana mapenzi sana na vyama vyao kuliko mapenzi kwa taifa lao.
Ukitaka kulielewa hili kirahisi ni pale utakapoweka hapa mjadala wote wote wenye maslahi mapana ya kitaifa, huo mjadala utatekwa na kuwa malumbano ya kivyama.
Hivi vyama badala ya kuwa chombo cha kuwafanya watu walitumikie taifa lao vimegeuka kuwa magenge ya kuteteana.
Unakuta hata kama mtu angekuwa mchafu vipi au afanye maovu kiasi gani lakini maadamu ni mwanachama wa chama unachokipenda basi utamtetea Kwa nguvu zoote.
Hii tabia inaua taifa wako watu ambao wangeanza kuzodolewa tangu kwenye vyama vyao huenda wangeona haya na kubadili mienendo yao, lakini Kwa sababu wanaona kuna mazuzu wafia chama watawatetea wanarelax.