Hii mechi ilipangwa Jumapili Mkwakwani Stadium Tanga lakini imeahirishwa. Je nini hakijaenda kama ilivyopangwa?
GENTAMYCINE ufafanuzi tafadhali.
Kama kweli imeahirishwa baai itakuwa ni Mbunu / Janja ya Yanga SC kwa Kushirikiana na Kiongozi wa Bodi ya Ligi ( TPLB ) Almasi Kassongo kwa Kushirikiana na Watendaji wa TFF wenye Uyanga mwingi.
Na nahusi hapa sababu Kuu zitakuwa Mbili tu....
1. Yanga SC ( kama ilivyokuwa Kwetu Simba SC tulivyotaka kucheza na Kagera Sugar ) Wamechungulia ( Kushirikiana ) na Kugundua kuwa Coastal Union FC Wameroga sana na hata wafanyeje Yanga SC watafungwa / wangefungwa tu.
2. Yanga SC wameamua nao kufanya Makusudi ama kwa kutoa sababu za Uwongo TPLB na TFF kwa kutumia Pesa chafu za GSM Kushawishi huu Mchezo uhairishwe nao wafanane kwa kuwa na Kiporo kama cha Simba SC na kwamba watataka Wacheze Michezo yao Kiidadi ( sawa ) na Wapambane Kuuchukua Ubingwa.
Na najua isingekuwa ile performance Kubwa iliyoonyeshwa na Simba SC Mapinduzi Cup Kisiwani Zanzibar hadi Kutawazwa Mabingwa rasmi Jana na kwa Kiwango cha Mchezaji Pape Ouamane Sakbo na huu Ujio wa Kiungo Fundi Clatous Chama ni kama vile Yanga SC wamechanganyikiwa na wameocopa wakihisi huenda Simba SC ikawapiku na kuwa Bingwa tena..
Ukiona Yanga SC inenda Mikoani kucheza Ligi Kuu halafu ukamuona Injinia Hersi na Msemaji Manara jua 90% ya uwsspo wao ( huko ) ni kwa kwa Kuwahonga Wachezaji au Waamuzi ( Referees ) Pesa ili Wabwebwe au Wapendelewe mpaka Washindwe wenyewe.
Na kama ni kweli Mechi hii imeahirishwa ( japo siamini bado ) watakaoathirika zaidi ( hasa Kisaikolojia ) ni Wachezaji na Watendaji kwa Klabu ya Coastal Union FC ya Tanga kwani nimeambiwa na Mtu kuwa Coastal Union Wameroga kiasi cha Kukufuru na kwamba Yanga SC ingedungwa Goli kuanzia 3 na kuwa Aibu Kubwa Kwao hali ambayo ingeleta Mgogoro mkubwa Klabuni hapo.
TPLB na TFF wameamua Kuibeba Yanga.