Ni kweli Adam na Hawa waliishi miaka takribani 900?

Ni kweli Adam na Hawa waliishi miaka takribani 900?

huyu mungu anawashughulikia wasiomwamini, lakini anashindwa kuwalinda wanaomwamini?? aisee.

hebu angalia kifo cha angela chibalonza.. mwanamama mashuhuri kabisa kwa kumsifu mungu, mwisho wa siku amekufa kwa ajali... halafu wanasema mungu amempenda zaidi???

mungu akikupenda zaidi anakuchukua mapema au anakuongezea maisha ili uzidi kumsifu? zile baraka za kuishi miaka mingi na heri duniani zimetoweka au?

hatari sana.
Hawa wafia dini walisha waokota sana.
 
kheri mtu mwenye mapungufu ya nguvu za kiume kuliko hawa wakristo.. ni bure kabisa..

waasisi wa hio dini wanafanya matendo yote ya kishetani ila mbongo hashtuki.. ila itafikia pahala tu.. kama ulipofikia ukomo wa mapenzi ya mashabiki wa Arsenal kwa Wenger.
Kwani kwenye uislam hakuna mashehe wanaofanya mambo ya kijinga
 
Nyie vijana angalieni; msije mkawa mnajipalia makaa ya moto. Hivi hamjui kuwa vitabu vya awali vyote ndivyo vinavyoitwa Torati !! Vitabu hivyou vipo katika Kuruhani (Qoran) na Biblia, tofauti ni majina na tafsiri ndogo ndogo za waandishi hawa wa sasa; kumbe dini zote na vitabu vyote vinasema maneno yale yametamkwa na biniadam lakini ni maneno yake Mungu Mwenyewe. Sasa leo umevuta sijui nini unasema kwa jeuri kabisa kuwa eti biblia imesema uongo. Unadiriki kusema kwa maana hiyo Mungu kasema uwongo !!!! Tafadhali tubu na uikane kauli hiyo ya hatari haraka sana. Hunijui nami sikujui lakini Mungu Anakujua.
Labda ww nikulize umevuta nini hadi ikafikia hatua ya kukubali vitu ambavyo ni vya uongo wa mwendo kasi.
 
Lakini ubishi wako utakufikisha mahala ambapo sipo. Enzi za Lutu na Nuhu Mungu alionyesha mpambano kwa mwanadamu lakini baadae akasema sitabishana na mwanadamu tena. Rejea maandiko Mwanzo 6:3. Na hapo ndipo aliposema umri huyu mwanadamu utakuwa miaka 120 badala ya ile ya wakati wa akina Nuhu
kwanza kabisa umepotosha kwa kusema mungu alionyesha mpambano na alibishana na mwanadamu, hakuna maandiko yanayosema hivyo..

mungu alipunguza umri wa binadamu kutokana na kitendo cha malaika (wana wa mungu) kufanya mapenzi na kuzaa na wanadamu. na matokeo ya kungonoka huko ndo wale wanawake wakazaa hao WANEFILI, ambao mungu aliona ni kama THREAT kwake kutokana na kwamba hao wanefili walikua na uwezo mkubwa na wangeishi kwa muda mrefu sana (muda utakaoshindana na mungu) kutokanana na wao kuwa mbegu ya malaika (watoto wa malaika).

MWANZO 6:2-3

"WANA WA MUNGU waliwaona hao BINTI ZA WANADAMU ya kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wowote waliowachagua. Bwana akasema roho yangu haitashindana na wanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama, basi siku zake zitakua miaka mia na ishirini."

kitabu cha Enoki kimeelezea kwa undani >>> The Book of Enoch: The Book of Enoch: Chapter VI.
 
hii thread ni maalum kwa kuelimishana kuhusu utata wa biblia na utata wa imani ya kikristo kwa ujumla.. tustoke nje ya mada.
Ok kwa kifupi Biblia ndio kitabu kilichosheheni kila kitu imegusa kila sehemu ya maisha ya mwanadamu.. Kuhusu uchumi biblia imemaliza maisha ya kawaida.. Siwezi kueleza yote maana nitajaza ukurasa ila biblia imejaa hekima zipitazo hekima za wanadamu!
 
Ok kwa kifupi Biblia ndio kitabu kilichosheheni kila kitu imegusa kila sehemu ya maisha ya mwanadamu.. Kuhusu uchumi biblia imemaliza maisha ya kawaida.. Siwezi kueleza yote maana nitajaza ukurasa ila biblia imejaa hekima zipitazo hekima za wanadamu!
unaamini biblia imezungumzia slave trade / biashara ya utumwa?
 
Nini chanzo cha dhambi? na kama ni shetani je ni nani wa kulaumiwa
Kati ya mungu binadamu na shetani?
Kwasababu mungu yeye ndio alimuumba adui shetani.
tusitoke kwenye mada mkuu, mie nimejibu swali linalomtatiza mleta hoja. hata akilaumiwa mmoja wao; MUNGU au shetani haitusaidii kitu kwa sasa kwa kuwa tayari tumeikuta dunia imeshauzwa mikononi mwa shetani na Adamu.
 
Sasa inakuwaje mungu anaumba kitu ambacho kinaingiwa na tamaa harafu baadaye kinakuja kumuudhi mwenyewe.
Si kwamba MUNGU hakujua, MUNGU alitoa Uhuru kwa viumbe wake wachague, upendo kwa kutii amri zake, au uasi, jambo la msingi aliwaeleza madhala ya uasi na faida ya utii. Kama vile alipomaliza kazi ya muumbaji akamletea Adam kila kiumbe ili aone Adam atawaitaje. Na jina alilolitamka Adam ndio likawa jina lake
 
Si kwamba MUNGU hakujua, MUNGU alitoa Uhuru kwa viumbe wake wachague, upendo kwa kutii amri zake, au uasi, jambo la msingi aliwaeleza madhala ya uasi na faida ya utii. Kama vile alipomaliza kazi ya muumbaji akamletea Adam kila kiumbe ili aone Adam atawaitaje. Na jina alilolitamka Adam ndio likawa jina lake
Kama mungu yupo kweli. kwanini mungu unamuongelea ktk wakati ulio pita?
 
tusitoke kwenye mada mkuu, mie nimejibu swali linalomtatiza mleta hoja. hata akilaumiwa mmoja wao; MUNGU au shetani haitusaidii kitu kwa sasa kwa kuwa tayari tumeikuta dunia imeshauzwa mikononi mwa shetani na Adamu.
Tuko pamoja 7spirits.
 
mfano unaweza kutwambia ilikuaje yohana mbatizaji atume watu wakamuulize yesu iwapo ndie,wakati tayari walikuwa wamekutana na yesu na akambatiza?,

how come yohana anaonekana kutomjua yesu wakati pia ni ndugu kwa maana ya ukoo mmoja na mamake na yesu na mamake yohana walikuwa wakitembeleana
naamini Yohana alimjua Yesu kama ndugu ila alishindwa kuelewa jambo moja tu ikiwa ni kweli Yesu alikuwa yule aliyetabiriwa kuwa atakuja. sidhani kama hakujua kwa dhana ya wao kuwa ndugu ila ile manifestation ya Yesu kama mwana wa Mungu ndiyo iliyokuwa inachanganya kwa kuwa tu ni kama walitegemea Yesu angekuwa na tofauti ambayo ingewafanya wao wamtambue kwa haraka lakini yeye Yesu aliishi kama mwanadamu wa kawaida(ila hakutenda dhambi).
na labda Yohana alitegemea Yesu angekomesha mateso ya yeye Yohana kuwekwa jela...lakini naamini pia kuwekwa jela kwa Yohana ni kama kumlichanganya (asili ya binadamu kufadhaika anapopitia wakati mgumu) kwa kuwa alipotuma watu wakaulize kwa Yesu ili hali alimtabiria Yesu wakati anambatiza.
 
Doh!! Hata kwenye qurani kuna watu waliishi miaka mingi joh..usikashifu dini yao..
 
Back
Top Bottom