Ni kweli Adam na Hawa waliishi miaka takribani 900?

Hawa wafia dini walisha waokota sana.
 
Kwani kwenye uislam hakuna mashehe wanaofanya mambo ya kijinga
 
Labda ww nikulize umevuta nini hadi ikafikia hatua ya kukubali vitu ambavyo ni vya uongo wa mwendo kasi.
 
kwanza kabisa umepotosha kwa kusema mungu alionyesha mpambano na alibishana na mwanadamu, hakuna maandiko yanayosema hivyo..

mungu alipunguza umri wa binadamu kutokana na kitendo cha malaika (wana wa mungu) kufanya mapenzi na kuzaa na wanadamu. na matokeo ya kungonoka huko ndo wale wanawake wakazaa hao WANEFILI, ambao mungu aliona ni kama THREAT kwake kutokana na kwamba hao wanefili walikua na uwezo mkubwa na wangeishi kwa muda mrefu sana (muda utakaoshindana na mungu) kutokanana na wao kuwa mbegu ya malaika (watoto wa malaika).

MWANZO 6:2-3

"WANA WA MUNGU waliwaona hao BINTI ZA WANADAMU ya kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wowote waliowachagua. Bwana akasema roho yangu haitashindana na wanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama, basi siku zake zitakua miaka mia na ishirini."

kitabu cha Enoki kimeelezea kwa undani >>> The Book of Enoch: The Book of Enoch: Chapter VI.
 
hii thread ni maalum kwa kuelimishana kuhusu utata wa biblia na utata wa imani ya kikristo kwa ujumla.. tustoke nje ya mada.
Ok kwa kifupi Biblia ndio kitabu kilichosheheni kila kitu imegusa kila sehemu ya maisha ya mwanadamu.. Kuhusu uchumi biblia imemaliza maisha ya kawaida.. Siwezi kueleza yote maana nitajaza ukurasa ila biblia imejaa hekima zipitazo hekima za wanadamu!
 
Ok kwa kifupi Biblia ndio kitabu kilichosheheni kila kitu imegusa kila sehemu ya maisha ya mwanadamu.. Kuhusu uchumi biblia imemaliza maisha ya kawaida.. Siwezi kueleza yote maana nitajaza ukurasa ila biblia imejaa hekima zipitazo hekima za wanadamu!
unaamini biblia imezungumzia slave trade / biashara ya utumwa?
 
Nini chanzo cha dhambi? na kama ni shetani je ni nani wa kulaumiwa
Kati ya mungu binadamu na shetani?
Kwasababu mungu yeye ndio alimuumba adui shetani.
tusitoke kwenye mada mkuu, mie nimejibu swali linalomtatiza mleta hoja. hata akilaumiwa mmoja wao; MUNGU au shetani haitusaidii kitu kwa sasa kwa kuwa tayari tumeikuta dunia imeshauzwa mikononi mwa shetani na Adamu.
 
Sasa inakuwaje mungu anaumba kitu ambacho kinaingiwa na tamaa harafu baadaye kinakuja kumuudhi mwenyewe.
Si kwamba MUNGU hakujua, MUNGU alitoa Uhuru kwa viumbe wake wachague, upendo kwa kutii amri zake, au uasi, jambo la msingi aliwaeleza madhala ya uasi na faida ya utii. Kama vile alipomaliza kazi ya muumbaji akamletea Adam kila kiumbe ili aone Adam atawaitaje. Na jina alilolitamka Adam ndio likawa jina lake
 
Kama mungu yupo kweli. kwanini mungu unamuongelea ktk wakati ulio pita?
 
tusitoke kwenye mada mkuu, mie nimejibu swali linalomtatiza mleta hoja. hata akilaumiwa mmoja wao; MUNGU au shetani haitusaidii kitu kwa sasa kwa kuwa tayari tumeikuta dunia imeshauzwa mikononi mwa shetani na Adamu.
Tuko pamoja 7spirits.
 
naamini Yohana alimjua Yesu kama ndugu ila alishindwa kuelewa jambo moja tu ikiwa ni kweli Yesu alikuwa yule aliyetabiriwa kuwa atakuja. sidhani kama hakujua kwa dhana ya wao kuwa ndugu ila ile manifestation ya Yesu kama mwana wa Mungu ndiyo iliyokuwa inachanganya kwa kuwa tu ni kama walitegemea Yesu angekuwa na tofauti ambayo ingewafanya wao wamtambue kwa haraka lakini yeye Yesu aliishi kama mwanadamu wa kawaida(ila hakutenda dhambi).
na labda Yohana alitegemea Yesu angekomesha mateso ya yeye Yohana kuwekwa jela...lakini naamini pia kuwekwa jela kwa Yohana ni kama kumlichanganya (asili ya binadamu kufadhaika anapopitia wakati mgumu) kwa kuwa alipotuma watu wakaulize kwa Yesu ili hali alimtabiria Yesu wakati anambatiza.
 
Doh!! Hata kwenye qurani kuna watu waliishi miaka mingi joh..usikashifu dini yao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…