Bado nazidi kuona utupu wenu kwenye mambo msiyoyajua anyway let me put right at least.
Mathayo 1
1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;
3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;
4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;
5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;
6 Yese akamzaa mfalme Daudi.
7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;
8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;
9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;
10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;
11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.
12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;
13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eli-akimu; Eli-akimu akamzaa Azori;
14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eli-udi;
15 Eli-udi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;
16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
Kwanza ujue jinsi wayahudi wanavyopeana majina ukuangalia hapo bolded nimeweka Eli hilo ni jina kamili hata kabla hujaongeza hudi au akimu hivyo enzi hizo na hata saivi mtu anaweza kuitwa let's say Michael lakini pia akitwa Mike au Elisifa lakini akaitwa Eli au Elly that's normal that's perfect.
Pili mtu anaweza kuwa na majina hata nane au saba au matano yanayoambatana la kwake la baba yake la baba mzaa baba yake la baba mzaa babu yake mpaka la ukoo ameyaunganisha pamoja kama majina yake.
Mfano mtu anaweza kuitwa Michael Jonathan Reuben Abraham Naton.
Huyu mtu anaweza pia kuitwa kwa kifupi Michael Naton au Michael Jonathan Naton au hata Michael Abraham it's normal it's accurate it's also very perfect.
Okay nipeni hoja yenu kuna ajabu gani Joseph au Yusufu kutumia jina la Jacob au Yakobo kama baba yake au Eli-azari au Eliazari au Hakimu kama baba yake?
Au Yesu kutumia Eli au Jacob mbona pia ametupia Mwana wa Adam au Simba wa Yuda isiwe tabu?
Am watching.